KITABU CHA SHETANI (9) Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA TISA TULIPOISHIA... “Sasa itakuwaje na umeshasema kila mwanaume anayejaribu kufanya naye mapenzi ni lazima afe?” Edmund aliuliza huku akionesha kuwa na shauku kubwa ya kutaka majibu. Licha ya yote yaliyotokea, alishindwa kuuficha ukweli uliokuwa ndani ya moyo wake kwamba anampenda sana msichana huyo. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... “Jiandae kufa,” alisema mganga huyo huku akiangua kicheko cha kizee, Edmund akajiinamia chini. “Ipo njia moja tu ya kuwasaidia wote wawili lakini ni ya hatari sana, hata mimi sipendi kumuona akiendelea kuua watu wasio na hatia, natamani nimuone akiwa na mume anayempenda, ajenge familia na hatimaye atulie lakini siyo rahisi,” alisema mganga Shiwinga , kauli iliyomfanya Edmund ainuke pale alipokuwa amejiinamia na kumsogelea mganga akitaka kujua ni mbinu gani hiyo ya kuwasaidia. “Inabidi Samantha atolewe nguvu za giza na tego aliloingiziwa mwilini …