Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sam alibaki anashangaa uwezo wa mapigo aliokuwa nao RPC kwani mapigo aliyoyapata hajawahi kuyaona, nguvu alizokuwa nazo wakati anamshika ilikuwa ni kama amebanwa na koleo huku akiwa amenyanyuliwa juu kama karatasi.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Wakati anatafakari na kusikilizia maumivu alinynyuliwa tena na kusukumwa hadi kwenye gari kisha akazamishwa ndani gari likawashwa mpaka ofisini kwa RPC.
Aliachwa ndani ya gari kwa muda kisha akarudi afande miraji na maaskari wengine wawili ambao walimchukua mpaka hospitali.
Pale hoapitali Sam alipewa huduma za majeraha aliyoyapata kichwani kisha akarudishwa nyumbani akiwa amefungwa mabandeji kichwani alipojigonga ukutani.
Sam hakutaka maongezi na mtu yeyote, aliingia ndani akaangalia fedha zake alizopewa baada ya kushinda mechi kisha akaanza kupanga namna ya kutoroka kwani alikuwa na fedha za kutosha.
Alipanga atoroke usiku huo huo na hivyo hakutaka hata kutoka sebeleni wala kuongea na mtu yeyote.
Mda wote Rafiki alikuwa akitamani kumuona Sam lakn alikuwa amejifungia ndani, alitaka kuingia lakini aliogopa kumponza Sam kwani alimjua baba yake na alijua kuwa mda wowotw atarudi.
Alivumilia sana akisubiri lakini sio sam aliyetoka nje wala kukaa tu sebuleni.
Verity alikuwa amenyong’onyea ndani kwake akiogopa kumfwata Sam kwani aliona A -Z alichofanyiwa Sam hivyo alijua wakati wowote nae yatamkuta.
…………………..
Saa nane usiku Sam alikuwa mlangoni anasikilizia kama kuna mtu yeyote anaetembea kwenye korido ili atoroke zake, wakati huu alikuwa anatiririsha machozi kwa yale aliyokuwa anakumbana nayo lakini alivyovuta kumbukumbu jinsi ambavyo amewala watoto wa RPC alijiona anastahili chochote. Aliguta machozi akanyonga mlango.
Owa tahadhari kubwa alikuwa anaelekea nje na tayari alishafungua milango na yuko kwenye uwanja wa garden, alimtaimu mlinzi akakanyaga ukuta na kujirusha hadi nje “tii”.
“Unakwenda wapi usiku huu na kwanini unatoroka?”
Sam hakuamini alichokuwa anakiona,
Kwa mara nyingine alikuwa mikononi mwa RPC, Sam alidhani huyu jamaa ni mchawi lakini kumbe kila alicholuwa anapanga kukifanya kilishajulikana mapema.
Sam alibebwa usiku huohuo hadi kituoni na kisha kukabidhiwa kwa afande Miraji.
” Huyu mtashinda nae humu mpaka usiku mumpeleke nyumbani kulala, apangiwe kazi ngumu”
“Sawa afande, waliitikia akina Miraji”
Kwa mara nyingine Sam alikuwa mikononi mwa Afande miraji.
Mkokola Saidi, Stellah Francis, Mery Sadock Maureen Junior, Tom Mwambs, Cecilya Cecil,
Kwa mara nyingine Sam alikuwa mikononi mwa Afande Miraji, hakujua kitakachoendelea lakini aliisikia amri ya RPC kwamba apewe kazi ngumu na awe anarudishwa nyumbani usiku.
…………………..
Ratiba ya Sam ilibadilika na akawa ni mtu wa kurudishwa nyumbani kila siku usiku na asubuhi anachukuliwa.
Kazi zilikuwa ngumu sana kwani kila asubuhi alikuwa anapelekwa kufagia maofisini kisha jikoni, alikuwa anafyeka maeneo mbalimbali ya kituoni hadi inafika usiku anakuwa amechoka sana.
Kwa amri ya RPC ilikuwa Sam apewe kazi ngumu lakini awe anapewa chakula cha kutosha, lakini mambo yalikuwa kinyume mno, kwakuwa Afande Miraji alikuwa na chuki nae alikuwa anampa kazi ngumu bila kumpa chakula.
Hii ilimfanya Sam achoke sana, haikupita hata wiki Sam alikuwa amedhoofu mwili na kuwa mwembamba, alikuwa anaunda mikakati ya kutoroka kila siku lakini mazingira yalikuwa magumu sana.
Ulinzi kwake ulikuwa wa hali ya juu na nikama vile afande Miraji hakupangiwa kazi nyingine kwani kila siku na kila mda alikuwa na Sam pekee.
…………………………..
RPC alikuwa na hasira sana juu ya Sam, kuna wakati alikuwa anakaa mwenyewe ofisini na kukagua simu yake kisha laptop yake na kisha anajikuta hasira zinampanda kiasi cha kutaka kuua.
Hasira zilipompanda sana alinyanyua simu yake na kuitafuta namba ya afande Miraji na kuanza kumpigia simu…
“Eeenh Afande”
“Shkamoo”
“Shkamoo nini…huyo kima uko nae hapo hadi sasa?”
“Ndio niko nae”
“Leo mzidishie dozi mara kumi”
“Hahahaaaa SAWA AFANDE!”
Hakuna kitu kilimfurahisha afande Miraji kama kuambiwa azidishe dozi ya Mateso kwa Sam.
Alichokifanya alimuita rafiki yake mkubwa
“Oyaa Gwakisa njoo unisaidiie kazi”
“Kazi gani tena wewe”
“Wewe njoo tu ila uje na Msuba”
“Poa”
Ndani ya dakika chache afande Gwakisa alikuwa amefika pale alipokuwa Miraji…
Walichukua misokoto ya Bhangi kisha wakaanza kuvuta huku wanapiga story kadhaa.
Miraji alimuelezea Gwakisa kuhusu kazi iliyoko mbele yake na kumuomba Gwakisa amsaidie lakini Gwakisa hakuamini.
“Huamini nini sasa”
“AAGH siamini aisee, isije tukatoa dozi hapa alafu tukapata matatizo”
“Subiri nimpigie umsikie mwenyewe”
“Haloo Afande”
“Unapigapiga nini wakati nimesema utoe dozi na uizidishe mara kumi, ina maana hujaanza mpaka saivi, au nikugeuzie kibao”
“Hapana afande nilitaka tu kukujulisha kwamba ndio naanza”
“Haya toa Dozi kamili sitaki ushoga shoga mimi”
“tii tiii” simu ilikuwa imeshakatwa!
…………………….
Dozi aliyokuwa anapata Sam ilikuwa ni ya kumtoa mtu roho, alikuwa amening’inizwa juu chini, yaani kichwa chini miguu juu kisha analowanishwa na maji na kusindiliwa mangumi.
Kama ungebahatika kumuona Sam kwa wakati huu ungeweza usile nyama tena, alikuwa amechakaa kama mfuko wa nailoni uliotoka mdomoni mwa Ng’ombe.
Ilikuwa ni ngumi, viboko, mateke, na kila aina ya vipigo. Walipoona wameridhika na kipigo walimfungulia kamba bila kumshikilia na kumfanya aanguke chini kama mzigo huku akiwa katanguliza kichwa.
…………………………
RPC alikuwa ofisini anakunywa Viroba Vya Konyagi ili kuondoa mawazo lakini kila alipokuwa anarudia kuangalia video alizokuwa nazo kwenye simu yake na kwenye laptop hasira zilikuwa zinazidi.
Aliumia sana kuona kuwa kijana aliyemfadhili ndani ya nyumba yake leo hii ametembea na watoto wake wote wawili
Katika mambo ambayo hakuna aliyekuwa anayajua pale nyumbani ni kwamba nyumba nzima ya RPC ilikuwa imefungwa na kamera za CCTV kuanzia ndani mpaka nje, hakuna mtu eyote aliyejua isipokuwa yeye mwenyewe.
Nikweli kuwa kuna wakati alikuwa anaangalia matukio ya nyumbani na hata kuwaona mabinti zake wakiwa uchi lakini kwakuuwa ni watoto wake hakuona shida yeyote, siku aliyoona wakifanya mapenzi na Sam tena wote wawili roho ilimuuma sana.
Alikuwa anajisemea mwenyewe kwenye kichwa chake kuwa ni heri mara mia angekuwa anatembea na mmoja kati ya wale mabiniti zake lakini kitendo cha wote wawili kuwa wanatembea na Sam aliona ni fedheha kubwa sana.
Alirudi tena akaona jinsi mwanae RAFIKI alivyokuwa anatolewa bikra na Sam huku akitokwa damu nyingi akahisi kuwa mwanae alikuwa anatendewa isivyo haki na kusahau kuwa hata yeye aliwatoa Bikra wasichana wengi tu!
Alivyoendelea kuangalia ilifika hatua akamuona Sam akiwa amesimama na mkewe huku akionekana anamshika eneo la kitovu na kusugua sugua.
Kwa RPC kumuona mkewe anamshika Sam eneo la kitovu huku Sam akiwa kifua wazi ilikuwa ni uzalili uliozidi kiwango.
Moja kwa moja aliamini kuwa Sam kala watoto wake wote na mke wake pia, alirusha ngumi akavunja meza ya kioo ‘aaaaaaaarrrrrrggggh’!
Alichukua bastola yake akatoka nayo kwa lengo la kwenda kumfumua Sam ubongo.
Alitembea kwa kasi hukua akiwa ameshikilia bastola yake tayari kwa kuua, alipokuwa anatembea huku bastola iko nje nje Afande mwingine ambaye alikuwa na cheo chini ya RPC alianza kumuita lakini mawazo ya RPC hayakusikia sauti hata kidogo.
RPC aliendelea na safari mpaka akafika pale waliko akina Afande Miraji….
Alitupa macho huku nakule lakini hakumuona Sam, akawauliza “Yuko wapi huyu nguruweeeeeeee?”
Hakuweza kumtambua Sam kwasababu alikuwa amechakaa na mwili wote ulikuwa umeloa damu huku akiendelea kukohoa damu pale chini alipo.
“Huyu hapa”
Afande Miraji alionyesha kwa kidole.
RPC alionekana kushtuka alipomuona Sam vile lakini alivyokumbuka aliyoyafanya hasira za viroba zikampanda tena akaanza kumfwata Sam huku amenyoosha bastola yake….
“paaaaaa…paaaaa….paaaaaa” Milio ya risasi ilisikika!
Kila mtu alikuwa ameelekeza kichwa chake pembeni asione jinsi ambavyo ubongo wa Sam ulikuwa unamwagika chini.
Pamoja na mateso ambayo Miraji alikuwa anatoa kwa Sam lakini hakuwa na uthubutu wa kuweza kumuua.
Aliogopa kuua japo alikuwa askari, moyo wake ulikuwa unadunda kwa kasi sana kwani hakuwahi kumuona mtu anakufa na hakudhani kuwa angeona mtu anauwawa mbele yake.
Mtu pekee aliyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua alikuwa ni Afande Mbaruku ambaye alikuwa na cheo chini ya cheo cha RPC, alivyoona hali aliyokuwa nayo RPC alijua kuwa hakukuwa na usalama hivyo aliamua kumfwata nyuma nyuma.
Alipomuona anamfyatulia Risasi mtu aliyelala chini amechakaa na kutapakaa damu ilibidi aushike mkono wa RPC na kuuelekezea ukutani ambapo risasi zote ziliishia ukutani hadi Bunduki ikabaki haina kitu.
Walianza kunyang’ang’anyana Bunduki, Afande Mbaruku hakujali kuwa Yule ni bosi wake yeye alichotaka tu ni kuhakikisha kuwa mtu anabaki salama.
Maskini Sam wawatu walikuwa hajui chochote, alikuwa anakoroma pale chini huku damu zikiwa zinamtoka puani na mdomoni.
……………..
Sam alikuwa kwenye gari ya POLISI mkoa wa Mbeya anakimbizwa Hospitali.
Japo alikuwa ameshapata huduma ya kwanza kwenye Hospitali ya polisi pale makao makuu lakini ilibidi akapate huduma zaidi kwani hali yake ilikuwa hairidhishi.
Gari ilikuwa inakimbia kwa kazi huku dripu zikiwa zimening’inia kwenye mikono ya SAM.
Huku nyuma ofisini alikuwa ameketi RPC na msaidizi wake ambaye ni Afande Mbaruku wanajadiliana.
“Nikweli kakukosea lakini njia unayotumia kumuadhiibu sio sahihi”
“Sio sahihi kivipi eeenh…au kwasababu sio wewe?”
“Ndio inawezekana ni kwasababu sio mimi ndio maana nafikiria kwa busara kuliko wewe…hivi unadhani ukimuua hapa, tena kwenye eneo la kazi utakuwa salama wewe? Hicho cheo chako unataka utuachie eeenh?”
“Hivi kweli mtoto nimlete kwangu ili nimsaidie alafu anitom…ee mke wangu na watoto wangu?”
“Unasemaje? Kafanyaje?”
“Kaio..ba familia yangu yote”
“Mhhhh….”
Baada ya Afande Mbaruku kusikia vile aliguna kwani hakuweza kuamini kile ambacho alikisikia mdomoni kwa RPC.
“una uhakika na unachokisema Afande?”
“Sasa unadhani nimechanganyikiwa au… hii…hii” RPC alikuwa analia.
“una uthibitisho afande?” Afande Mbaruku aliuliza kwa sauti ya upole kwani hata yeye alishaona uzito wa swala lililokuwepo mbele yake.
RPC alichukua laptop yake na kuwasha video iliyokuwa inaonyesha kila kitu kilichofanywa pale kwake na Sam.
Afande Mbaruku aliangalia kila kitu huku nayeye matamanio yakimshika kwa Jinsi wale mabinti walivyokuwa wazuri na wanaovutia.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)