RANIA (4)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (4)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Jao,ukweli kuhusu maisha yangu hi huu..alisema Fasha kisha akamsogelea jao na kumnong'oneza kitu fulani. Jao hakuamini maskio yake kwa alichokisikia.. SASA ENDELEA.. Mwanamfalme!!!... Aliita jao kwa mshtuko. Ni kweli jao...mimi sio mtoto halali wa Mfalme,Mfalme hana uwezo wa kupata mtoto..nilimsikia mama yangu malikia akiongea na mganga... Alisema Fasha kwa unyonge sana. Jao alibaki mdomo wazi... Hakuamini alichokisikia. Kwahyo, wazazi wako wako wapi?.. Aliuliza jao. Sijui walipo... Siwafahamu...alisema Fasha. Kwa mujibu wa malikia na mganga, mimi sio mtoto halali na wa Mfalme na hata malikia sio mama yangu mzazi.. Siku nilipojua huo ukweli sikulala usiku mzima..si unakumbuaka?..aliuliza Fasha. Nakumbuka mwanamfalme.. Alisema jao. Basi nilikua nikisumbuliwa na ukweli huu unaouma..alisema Fasha. Sasa, utafanya nini siku ikijulikana?..aliuliza jao kwa wasiwasi. Nitaondoka kama wakitaka..na ndio maana nakua mbabe na katili maana najua mw…