NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE (1)
Jina: NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA KWANZA KWA jina ninaitwa Zakia Ramadhani , ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto kumi, mama yangu aliyeitwa Zubeda Hassani na baba yetu aliyeitwa Saidi Ramadhani ambaye hapo tulipokuwa tukiishi alijulikana zaidi kwa jina la Mzee Mkude. Familia yetu ilikuwa miongoni mwa familia masikini zilizokuwa zikiishi katika Kijiji cha Mbingu kilichokuwa katika Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro. Hatukuwa na fedha, baba alikuwa mkulima mzuri wa mpunga , mara kwa mara aliamka asubuhi sana na kuelekea shambani kulima huku mama akibaki nyumbani akiandaa uji, unapoiva, ninaondoka naye na kuelekea huko shambani. Maisha yalikuwa magumu, yalituumiza lakini hatukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kupambana usiku na mchana ili tupate angalau fedha za kufanya mambo yetu mengine. Maisha hayo ya kimasikini, niliyachukia sana, nilitamani kuwa na fedha na kuyabadilisha maisha hayo, baba yangu atembelee gari, awe na nyumba nzuri …