Mtunzi: Nyemo Chilongani
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mara mguso wa mtu huyo ukahama kutoka begani mwangu na kuanza kuelekea chini, nilizidi kutetemeka mno, mikono yake ikahamia katika mgongo wangu na kuanza kuushikashika, baadaye akahamia katika kiuno changu,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
SASA TUENDELEE...
nikabaki nikianza kulegea mwili wangu.
“Ni kipindi kirefu kimepita, miaka kumi pasipo kumgusa mwanamke yeyote yule, upo tayari mpenzi wangu?” aliniuliza.
Sikumjibu, nilibaki kimya, wakati nikiwa nimesimama vilevile, ghafla nikaanza kuona mazingira ya mahali pale yakianza kuondoka na mazingira mengine kuingia.
Mbele yangu kukaonekana kuwa na kitanda kikubwa, ndani ya chumba kikubwa, alichonifanya ni kunisukumia kitandani, niliona kweli nimeangukia kitandani, ila ukweli ni kwamba niliangukia ndani ya kaburi lake, kitanda, lilikuwa jeneza lake, alichokifanya, naye akaja kwa juu yangu mgongoni, nikajigeuza ili nimuone, sikumuona, ila miguso yake, ilionyesha kabisa kwamba alikuwa hapo pamoja nami kwani yeye ndiye alianza kunivua nguo, yaani nalivuliwa nguo na mtu nisiyemuona.
Nilitakiwa kutulia vilevile, kumbuka kwamba nilifanya mapenzi na maiti kumi na tisa na hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho, hivyo niliona kuwa na sababu zote za kutulia kwani baada ya hapo, nilikuwa na uhakika wa kupata utajiri kama alivyoniambia mganga yule.
Ndani ya kaburi lile ndipo tulipoanza kufanya mapenzi, maiti ile ilikuwa ikinuka sana, sikuwa nikiiona ila niliihisi miguso yake kila kona katika mwili wangu.
Nilifanya naye mapenzi kwa saa moja ndipo akamaliza, nikahisi akiondoka mahali hapo na kuisikia sauti ya mganga ikinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya, sasa ningekuwa tajiri mkubwa.
“Umefanikiwa, sasa utakuwa tajiri mkubwa tu,” nilisikia sauti ya mganga.
Nilichokifanya ni kutoka nje ya kaburi na kuvaa nguo zangu. Kilichonishangaza, ghafla nikaanza kuona moshi mzito ukifuka kutoka ndani ya kaburi lile, sikujua nini kiliendelea, moshi ule mzito ukalifunika kaburi lote hata lisionekane, wakati nashangaashangaa tu, ghafla moshi ule ukakatika na kaburi lile kujifukia kama lilivyokuwa mwanzo.
Sikutaka kubaki mahali hapo, nikatoka na kuelekea nje ya eneo la kaburi lile huku tayari ikiwa ni saa nane usiku. Nilimkuta mganga akiwa amekaa pembeni akinisubiri, aliponiona, kwanza akatoa tabasamu pana, nikamsogelea.
“Hongera sana, hakika umenifanya nijisikie fahari sana,” aliniambia mganga yule.
“Kwa hiyo lini nitapata utajiri?”
“Utaanza kesho, ila nataka ufanye kitu.”
“Kitu gani?”
“Biashara yoyote ile…”
“Mmh!”
“Ndiyo hivyo! Utakapoanza, amini kwamba ndipo utajiri utakapoanzia..” aliniambia huku akinikazia macho.
Nilichokiamini ni kwamba mara baada ya kufanikiwa kufanya mapenzi na maiti zile basi ningepata utajiri kwa kukuta begi la fedha liwakiwa sehemu kumbe sivyo.
Akaniambia kwamba natakiwa kufanya biashara ambayo ndiyo ingekuwa chanzo cha utajiri wangu, sikuwa na jinsi, japo kwa kishingo upande, nikakubaliana naye. Na hivyo kuondoka mahali hapo.
Siku iliyofuata, nikamwambia Dickson pale Ubungo kwamba nilitaka kufanya biashara na biashara yenyewe ambayo niliichagua ilikuwa ni kuuza magazeti, akanikubalia hivyo kutafuta meza na kuanza kufanya harakati zote za kuhakikisha magazeti yanauzwa mara moja.
Siku mbili zilizofuata, tayari nilikuwa na meza yangu, niliweka juu magazeti mengi, nikatafuta vitabu vya hadithi na kutulia. Kitu cha ajabu ambacho sikuwahi kukiona ni pale watu walipoanza kumiminika katika meza yangu na kuanza kununua magazeti.
Nilishangaa, huwa ni vigumu kwa magazeti kumalizika kwa saa moja, lakini huwezi kuamini, magazeti mia moja niliyopewa, yote yaliishia ndani ya saa moja tu. Si mimi nileyeshangaa, hata watu wengine wa pale walishangaa pia.
Haikuwa kawaida kabisa na sidhani kama iliwahi kutokea. Magazeti yakaisha lakini nikashangaa watu wengine wakija mezani kwangu, waliiona meza ikiwa tupu ila wakawa wananiuliza kuhusu magazeti, yapo au yamekwisha, nilishangaa, meza ilikuwa tupu, sehemu zingine zilikuwa na magazeti, kwa nini hawakwenda huko?
Huo ulikuwa mwanzo, niliendelea kufanya biashara ya kuuza magazeti, ikaanza kuyabadilisha maisha yangu, nikawa naongezewa magazeti mengi, nikaanza kuyaona maisha yakianza kubadilika, fedha ziliingia, baadaye nikaanzisha biashara nyingine ya kuuza juisi na maji, hiyo ndiyo iliyoniingizia fedha zaidi na hivyo kupanga chumba Manzese Midizini.
Naweza kusema huo ulikuwa mwanzo tu, ndani ya miezi mitatu tangu nianze kufanya biashara hizo, nikashangaa nikiwa na akiba ya milioni tatu chumbani kwangu. Sikujua nilizipataje, ila nilichokijua ni kwamba kulikuwa na nguvu fulani nyuma yangu, nikafanikiwa zaidi.
Ulipoingia mwezi wa tano tangu nifanye biashara hizo, nikajikuta nikiwa na milioni tano. Nikashtuka, utajiri ukaanza kuninyemelea pasipo kukumbuka kwamba unapokuwa na utajiri wa kishetani huwa huna furaha, huna amani, ni utajiri unaotesa na kuumiza mno. Huo ndiyo ukaanza kuninyemelea. Mara ya kwanza, sikujali, ila baadaye, nilikuja kujuta kwa nini nilitaka utajiri.
Kusema ukweli hakukuwa na kipindi nilichokuwa na furaha kama kipindi hicho, sikuamini kilichokuwa kikiendelea, masikini mimi, ambaye niliishi katika maisha ya umasikini mkubwa mkoani Morogoro, eti leo hii na mimi nilikuwa na mamilioni ndani ya chumba changu.
Maisha yalibadilika kabisa, nilifanya biashara kwa kujituma kiasi kwamba hakukuwa na mtu aliyehisi kwamba fedha zangu zilikuwa za kishirikina, nilitaka niwe tajiri mkubwa, mwenye biashara nyingi, niingize hata milioni mia moja kwa mwezi.
Nilijitahidi kufungua biashara mbalimbali tena zilizoniingizia fedha. Fedha zilimiminika, hakukuwa na aliyejua kilichokuwa kikiendelea zaidi ya Dickson tu ambaye alikuwa rafiki yangu wa karibu na ndiye aliyenipokea mara baada ya kufika Dar es Salaam.
Nilifanikiwa sana, nikaanza mipango ya kujenga nyumba yangu kubwa maeneo ya Goba huku nikinunua gari yangu nzuri kwa ajili ya kutembelea. Ndiyo hivyo, maisha yalibadilika na nilikuwa na kila sababu ya kutumbua pesa nilivyotaka.
Nakwambia kuhusu maisha yangu, nakwambia kwamba inawezekana kupata utajiri wa kishirikina lakini kamwe utajiri huo mwisho wake huwa mbaya mno. Niliwahi kuzungumza na watu wengi, najua nchi yetu imejaa masikini lakini kamwe usithubutu kupata utajiri kwa njia za kishirikina kwani huwa na gharama yake, shetani hatoi kitu pasipo kukuumiza, hatoi kitu pasipo kukupa masharti ambayo anajua kwamba utashindwa tu.
Wengi waliniona kama mwanamke anayejua kufanya biashara sana pasipo kujua kwamba nyuma ya maisha yale kulikuwa na nguvu kubwa ya kishetani. Kumbuka kwamba familia yangu ilikuwa masikini sana, wazazi wangu walihangaika kwenda shambani kila siku asubuhi, hivyo nilikuwa na kila sababu ya kuwasaidia.
Nilichokifanya baada ya siku kadhaa ni kurudi kijijini kwetu, sikupanda basi, nilitumia gari yangu binafsi, Harrier nyeusi, mpya kabisa. Sikutaka kwenda kijijini moja kwa moja, nilitaka kupitia Ifakara kuonana na Mudi, yule mwanaume, utingo aliyenisaidia kiasi cha fedha kilichonifikisha Dar es Salaam, unamkumbuka?
Nilipofika Ifakara, nikaelekea mpaka katika kituo cha daladala. Wanaume wote wakabaki wakiniangalia kwa matamanio, nilikuwa mrembo mno, niliyenukia fedha kila nilipopita, walinitamani lakini kwa kuniangalia tu, hawakuona kama nilistahili kuwa nao.
“Unamuulizia Mudi anayeishi Mazobezobe?” aliniuliza mwanaume mmoja.
“Ndiyo! Yupo wapi?”
“Ametoka, ila msubiri, atarudi muda si mrefu, amekwenda Zilimpompa,” aliniambia kijana huyo, Zilimpompa ulikuwa mmoja wa mitaa hapo Ifakara.
Sikuwa na jinsi, sikutaka kuondoka mahali hapo, nakumbuka niliwahi kumwambia Mudi kwamba nilikuwa nikielekea Dar kutafuta utajiri na kuna siku ningekuwa tajiri, hakuwa akiamini, alinisaidia lakini najua aliona kwamba nakwenda Dar kupoteza muda, kujiuza na kufanya mambo mengine.
Leo hii nilirudi tena kwake, sikuwa Zakia yule masikini, nilikuwa Zakia mwenye pesa, niliyeendesha gari, niliyejipulizia manukato ya The Princess ambayo yalikuwa ni zaidi ya shilingi laki tano, nilikuwa na gari la kifahari, yaani kila nilichokuwa nacho, kilionyesha kwamba nilikuwa na pesa.
Baada ya saa moja, huku nikiwa garini nimesinzia, mara nikasikia kioo cha gari langu kikigongwa, nilipoyafumbua macho yangu na kumwangalia mgongaji, alikuwa Mudi. Uso wake ulikuwa kwenye mshangao mkubwa, kwanza hakunijua mimi nilikuwa nani, nikakishusha kioo.
“Mudi, mambo vipi?” nilimsalimia huku nikimuonyeshea tabasamu pana.
“Poa,” alinijibu huku uso wake ukiwa kwenye maswali mengi.
“Unanikumbuka?”
“Hapana! Wewe unanijua?” alinijibu na kunitupia swali.
“Jamani mpenzi! Kweli hunikumbuki?” nilimuuliza huku nikimfungulia mlango na kumtaka aingie.
Akaingia, alionekana kujishtukia sana, alikuwa mchafu, mavazi yake yalichakaa sana. Humo, bado alikuwa na maswali mengi, mimi nilikuwa nani na kwa nini nilimuita ndani ya gari? Hapo ndipo nikamuweka wazi kwamba mimi nilikuwa Zakia, mwanamke yule wa miezi kadhaa iliyopita ambaye nilikuwa na safari ya kwenda Dar.
“Zakia! Ni wewe?” aliniuliza huku akinishangaa.
“Ndiyo! Nimeona nije kukusalimia,” nilimwambia.
“Imekuwaje tena?”
“Nini jamani?”
“Kuwa hivyo!”
“Hahaha! Nilikwambia nakwenda Dar kutafuta utajiri, si unaona nimeupata,” nilimwambia huku nikitoa tabasamu.
Alibaki akinishangaa, sikutaka kujali sana, nilimwambia kwamba siku hiyo nilikuwa mgeni wake, nilitaka kulala naye, kumbuka alinisaidia nauli, elfu hamsini, nilitaka nimlipe, siyo fedha bali kumpa mapenzi motomoto ambayo asingeweza kuyasahau maisha yake yote.
Tukaondoka na kuelekea katika hoteli moja iliyokuwepo hapo Ifakara, nikachukua chumba na kuingia chumbani, tulipofika, akakaa kitandani, akavua nguo, akaenda bafuni, ila aliporudi, nikashangaa sana, hakuwa yule Mudi ninayemfahamu, alibadilika na kuwa moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi, maiti iliyojaa damu ambayo nguo zake tu zilionyesha kwamba alipata ajali. Nikashtuka sana!
“Kuna nini mpenzi?” aliniuliza swali hilo, hapohapo nikamuona akibadilika na kuwa Mudi.
Kiukweli nilichanganyikiwa sana, nilitetemeka mwili mzima na kuuhisi mwili wangu kama umepigwa shoto fulani ya umeme. Mudi akanisogelea, akanitupa kitandani na kutulia juu yangu. Nilibaki nikimwangalia kwa macho yenye kurembua, tayari nilianza kuingia katika ulimwengu mwingine wa mahaba.
“Unanukia vizuri mpenzi wangu…” aliniambia, ghafla nikashtuka.
Maneno kama hayo niliambiwa na maiti ile ya kule makaburini kipindi alichotaka kufanya mapenzi na mimi.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi
