NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE (7)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
“Unanukia vizuri mpenzi wangu…” aliniambia, ghafla nikashtuka.

Maneno kama hayo niliambiwa na maiti ile ya kule makaburini kipindi alichotaka kufanya mapenzi na mimi.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI

SASA TUENDELEE...
Maneno yaleyale ndiyo aliyoyazungumza Mudi, karibu kabisa na masikio yangu.

“Nashukuru!” nilijibu huku nikiachia tabasamu pana lenye hofu.

“Umetafuta sana utajiri, hakika utakuwa zaidi ya hapa, ninachokitaka ni wewe kuwa mpenzi wangu milele,” alisema Mudi.

Kiukweli alinichanganya sana, hapohapo nikamuona akitoka katika sura ya Mudi na kurudi katika sura ya moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi mochwari, hakika ilinitisha sana. Nikataka nijitoe pale kitandani, akanikandamiza zaidi. Nikahisi kifua kikianza kubana na pumzi kuanza kukata.

Bado macho yangu yalikuwa yakiiona maiti juu yangu, ilikuwa imenikandamiza vilivyo pale nilipolala, sikumuona Mudi kabisa, nilijitahidi kujitoa kutoka hapo kitandani lakini nilishindwa kabisa.

Nilianza kuhema juujuu, kuna wakati nilihisi kama ningekufa kwani nilibanwa sana kiasi kwamba nguvu zikaanza kuniisha mwilini mwangu. Wakati sura ile ikiendelea kuwa ya hiyo maiti, ghafla ikabadilika na kuwa sura ya Mudi, nilishangaa, hata kule kubanwa kote kukatoka.

“Kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiniangalia usoni.

“Hakuna kitu,” nilijibu huku nikionekana kuwa na hofu kubwa usoni mwangu.

“Hapana! Kutakuwa na tatizo, kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiwa amenikazia macho.

Ni kweli kulikuwa na tatizo lakini sikutaka kumwambia, najua hakuwa akifahamu lolote lile, niliiona maiti lakini kama ningemwambia kuwa nimeiona maiti badala ya kumuona yeye, angeniikiriaje?

Nilijaribu kumwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo angeendelea kama kawaida yake. Tulifanya mapenzi siku hiyo, sikutaka kuondoka, nililala na Mudi hotelini hapo huku usiku mzima nikiota ndoto za ajabu sana, mara nakimbizwa makaburini na watu waliovalia mashuka meupe, mara nakuchukuliwa na kupelekwa mochwari kisha kuingizwa katika masanduku ya kuhifadhia maiti.

Mpaka tunaamka asubuhi, niliota ndoto mbili, zote zilikuwa za kutisha mo, sikujua kwa nini ilikuwa hivyo, nilitamani nipate majibu juu ya ndoto zile kwamba kwa nini kipindi cha nyuma sikuwa naota ndoto mbaya ila kipindi hicho zilikuwa zikija kwa sana?

Sikutaka kujali japokuwa moyo wangu ulikuwa na hofu kubwa. Asubuhi hiyo tukanywa chai na kumwambia Mudi kwamba ningeondoka kuelekea katika kijiji chetu cha Mbingu.

“Ni lazima niondoke mpenzi,” nilimwambia kwa sauti ndogo, ilikuwa kama saa nne asubuhi.

“Sawa! Ila ningependa niendelee kuwa nawe, ila haina jinsi, kwenda kuwaona wazazi ni jambo la msingi sana,” aliniambia kwa unyonge ambao ulinionyesha kwamba hata yeye hakupenda kabisa kuniona nikiondoka.

Hakukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima niondoke kuendelea na safari yangu. Tulipoagana na kwenda ndani ya gari langu, nikatulia, nikauegemea usukani na kuanza kufikiria kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.

“Tatizo nini tena?’ nilijiuliza lakini sikupata jibu.

Sikutaka kubaki mahali hapo, nikaondoka zangu na kuendelea na safari yangu. Njiani, sikuwa na furaha hata kidogo, wakati nikiwa nimebakiza kilometa kumi kabla ya kufika kijijini, nikashangaa kuona gari likipunguza mwendo na kisha kusimama pembezoni mwa barabara.

Nilishangaa, gari hilo halikuwa bovu, kulikuwa na mafuta ya kutosha, sasa kwa nini lilipunguza mwendo na kisha kujizima, nilibaki nikijiuliza sana lakini hata kabla sijapata jibu, niliisikia sauti ya mtu ikiniambia niangalie nyuma kwani kulikuwa na kitu.

Harakahara nikayapeleka macho yangu katika siti za nyuma, nilichokiona ni boksi kidogo likiwa limefungwa vizuri kabisa. Kwanza nikashtuka, sikujua ni nani aliliweka boksi hilo na ndani kulikuwa na nini.

Niliamini hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kufungua mlango wa gari langu na kisha kuingia ndani kwani ufunguo nilikuwa nao, sasa nani alidiriki kuufungua mlango na kuliweka boksi hilo? Nikakosa jibu.

Nikatoka hapo mbele na kuelekea nyuma, boksi lile liliandikwa jina langu kwa juu, nilikuwa na hofu kubwa lakini nilitakiwa kufungua, ilikuwa ni lazima nijue ndani kulikuwa na nini kwa nini lilikuwa ndani ya gari langu.

Wakati nimelichukua boksi hilo, cha kushangaza kabisa mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu mno, kijasho chembamba kikaanza kunitiririka, sikujua sababu ya kuwa kwenye hali hiyo, kumbuka hapo ilikuwa porini, nilizungukwa na miti kila kona, sikuogopa kuwa hapo, ila hilo boksi ndilo lililonitia hofu.

Nikafungua na kuangalia ndani. Kitu nilichokutana nacho, kilinishtua sana, kulikuwa na kisu kilichofungwa kitambaa chekundu katika mpini wake, nikajiuliza sababu ya kisu hicho kuwa humu garini ilikuwa nini?

“Umekiona hicho kisu?” niliisikia sauti ya mganga, niliangalia huku na kule, sikuona mtu, nikashangaa.

“Ndiyo mkuu!”

“Unatakiwa kutoa sadaka moja kila baada ya miezi miwili,” nilimsikia akiniambia.

“Sadaka?”

“Ndiyo! Bado tuna kazi kubwa na wewe, ni lazima ufanye tunachokuagiza ili utajirike zaidi,” aliniambia.

“Tuna?”

“Ndiyo! Sipo peke yangu, mimi na watu wa giza,” aliniambia.

“Watu wa giza?”

“Ndiyo!”

“Wakina nani?”

“Waliokupa utajiri,” alinijibu.

Hakika nilishangaa sana, maneno aliyoniambia kama sikuwa nikiyaelewa, ilikuwaje aseme kwamba yeye alishirikiana na watu wengine katika kunipa utajiri na wakati nilichokijua ni kwamba yeye peke yake ndiye aliyenipa utajiri huo?

Nilishangaa sana lakini bado sikuridhika, nilitaka kujua zaidi kuhusu hizo sadaka alizosema kwamba nilitakiwa kuzitoa, zilikuwa sadaka za nini? Fedha au?

“Ni lazima uue?” nilisikia sauti hiyo ikinipa majibu.

“Niue?”

“Ndiyo! Utajiri uliokuwa nao ni utajiri wa damu, huwezi kuwa nao milele mpaka utakapotoa damu, ni lazima uue kila baada ya miezi miwili, hakika utajiri utaongezeka na kuwa mwanamke tajiri kuliko wote nchini Tanzania,” aliniambia.

“Mimi niue?”

“Ndiyo! Hakika hautomfuata mtu na kumuua, angalia tena kwenye boksi,” iliniambia sauti hiyo, harakaharaka nikaangalia kwenye boksi, macho yangu yakakutana na kioo.

“Unakiona hicho kioo? Kichukue, kiangalie, unaona nini?” iliniuliza, nikakichukua na kuanza kukiangalia, sikuiona taswira yangu, taswira ambayo niliiona ilikuwa ni ya baba yangu.

“Ichome taswira hiyo kwa hicho kisu,” iliniambia.

“Unasemaje?” niliuliza huku jasho likinitiririka, hakika niliogopa kwani nilijua kwamba endapo ningeichoma taswira ile, basi baba yangu angekufa.

“Ichome…” sauti ya mganga iliniambia, nikabaki nikitetemeka.

Nilibaki nikitetemeka, sikujua ni kitu gani nilitakiwa nikifanye mahali hapo. Jinsi mganga yule alivyoniambia kwamba niichome taswira ya picha ya baba yangu katika kioo kile.

Kumuua baba yangu! Kilikuwa kitu kisichowezekana kabisa, nilikumbuka namna alivyokuwa akiyasumbukia maisha yangu kipindi cha nyuma, nilikumbuka jinsi alivyokuwa akijinyima kwa ajili yangu, yaani nipate maisha mazuri, hakujali kama alikuwa akila au la, alichokijali ni mimi kula na kulala sehemu nzuri.

Nilifanikiwa, nilitaka nimuonyeshee baba kwamba hatimaye ule umasikini uliokuwa umetutafuna kwa kipindi kirefu usingekuwepo tena, nilitaka niwaonyeshee wanakijiji kwamba kitendo changu cha kuondoka nyumbani kwetu na kwenda kijijini kilikuwa sahihi kwani kile nilichokitaka, tayari nilikipata.

Nilibaki nikiiangalia taswira ile, mawazo yote hayo yalinijia kichwani mwangu wakati ambao nilishika kisu kile. Mapigo ya moyo yalikuwa juu mpaka kuhisi kwamba kama angepita mtu yeyote mahali hapo basi angeyasikia kwa jinsi yalivyokuwa yakidunda.

“Zakia, ichome taswira hiyo,” niliisikia sauti ya mganga huyo.

“Siwezi…ninashinwa,” nilisema pasipo kuogopa kitu chochote kile.

“Kwa nini unashindwa?” aliniuliza.

“Nilitafuta utajiri kwa ajili ya wazazi wangu, sasa kwa nini nimuue na wakati kila kitu nilichokuwa nacho naye alitakiwa kukiona?” niliuliza swali nililoliona kuwa na hoja, ila kwa mganga huyo, halikuwa na hoja yoyote ile.

“Basi acha tuuchukue utajiri wetu, utarudi na kuwa masikini, tena masikini mkubwa zaidi ya ulivyokuwa,” aliniambia mganga yule.

Nilichanganyikiwa, sikutaka kuuachia utajiri ule kwani tayari nilishaonja utamu wake, nilitaka kuwa nao milele, yaani hata maisha baada ya kifo kama kungekuwa na matumizi ya fedha basi nitakapokufa niende nao kwani ulikuwa mtamu mno.

Kitendo cha kuniambia mamneno hayo, nikashindwa kuvumilia, sikuwa tayari kuona utajiri huo ukiondoka mikononi mwangu, ilikuwa ni lazima nimuue baba yangu.

Kwanza nikafikiria kwamba alikuwa mzee, hakuwa na nguvu za kutosha, kama ningemuacha basi mwaka huohuo hapo baadaye ilikuwa ni lazima afariki kwani umri ulikuwa umekwenda sana.

Kitendo cha kufikiria hayo, nikashangaa kupata majibu kwamba ilikuwa ni lazima nimuue, kama nisingemuua mimi basi angekufa miezi michache ijayo. Sikutaka kujiuliza tena, mawazo hayo yakanipa nguvu na hivyo kuchoma taswira ile. Nilipomaliza, mganga akaniambia niwashe gari, nikawasha na kuanza kuondoka mahali hapo.

Nilichukua saa mbili, nikafika katika Kijiji cha Mbingu. Kwanza wanakijiji walipoliona gari hilo, wakashangaa sana, hakukuwa na gari lolote la kifahari lililowahi kufika kijijini hapo, magari yote ambayo yaliwahi kufika yalikuwa yale ya mizigo ambayo yalifuata nafaka hapo kijijini, sasa watu wakawa wanajiuliza, je, huyo aliyeingia na gari la kifahari alikuwa nani?

Sikutaka kuteremka, unapofika kijijini kwetu, kwa jinsi ilivyokuwa ilikuwa vigumu sana kufika na gari mpaka karibu na nyumba yetu, ilikuwa ni lazima ufikie mbali, uteremke na kuanza kutembea kuelekea huko.

Watoto na watu wengine walishasogea mahali gari lilipokuwa na kuanza kuliangalia. Hawakujua ndani ya gari hilo kulikuwa na nani kwani vioo vya gari hilo vilikuwa ‘tinted’.

Najua walikuwa na maswali, nilichokifanya baada ya kukaa ndani ya gari kwa dakika kama tano, nikateremka, wengi waliponiona, hawakunifahamu, kwa jinsi nilivyovaa, miwani yangu na nguo za thamani, hakukuwa hata na mtu mmoja aliyehisi kwamba mwanamke huyo aliyekuwa akitembea nilikuwa mimi.

“Huyu ni Mzungu?” nilimsikia mtoto mmoja akiuliza, watoto wengine walikuwa wakinifuata kwa nyuma.

Nilitembea mpaka nilipofika karibu na nyumba yetu, kilichonishtua ambacho sikuwa nikikumbuka ni msiba uliokuwapo. Watu zaidi ya hamsini walikuwa mahali hapo, nilisikia vilio kutoka kwa watu kadhaa waliokusanyika nyumbani kwetu,

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni