SHEREHE KUZIMU (22)

Zephiline F Ezekiel
SHEREHE KUZIMU (22)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI ILIPOISHIA... Sifa njema waliyoijenga ya kuzungumza na watu vizuri ndiyo iliyopelekea duka la nguo la Vivian alilolifungua katikati ya jiji hilo kupata mafuriko ya wateja. Kama ilivyokuwa jijini arusha duka la Vivian bado liliendelea kuendeshwa katika namna ya kuwaunganisha watu na kuzimu pasipo wao kufahamu kilichokuwa kikiendelea. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Bidhaa zenye mvuto wa hali ya juu zilizokuwa dukani kwa Vivian zilikuwa zinatokea kuzimu. Majini yaliendela kufanya kazi ya kuwavuta wateja ili waweze kwenda kwa wingi katika duka hilo. Ndani ya kipindi kifupi Vivian alifanikiwa kuwateka wateja wa wafanya biashara wenzake. Nelson alifurahi sana alipokuwa anaona duka la nguo alilokuwa amemfungulia mke wake linafanya vizuri katika mauzo. Hakujua kwamba kuna namna ambayo ilikuwa inatumika kuwavuta wateja katika duka l…