SHEREHE KUZIMU (29)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA ILIPOISHIA... Nuru inayopenyeza katika dirishani la chumba alicholazwa, inaonekana kukera macho yake na kusababisha ageuzie shingo yake ukutani. Macho yake yanaonekana kuwa malegevu na yasiyokuwa na nguvu kabisa. Pamoja na hayo yote anaonekana kukunja ndita kutokana na maumivu anayohisi kwa mbali katika kichwa chake. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Masikio yake yanafanikiwa kunasa sauti ya mitambo ya oygen inayonguruma kwa mbali sana wodini mule. Baada ya kuushughulisha ubongo wake kwa muda wa kama dakika tano, aligundua kuwa yupo wodini amelala huku dripu ikiingiza dawa katika mwili wake dhoofu. “Sasa nimefikaje hospitalini?” alizidi kujiuliza maswali mwenyewe, kipindi ambacho fahamu zilikuwa zinazidi kumrejea. Swali hili ndilo lililompa tabu sana kuweza kupata jibu lake, kwavile alitafakari kwa muda mrefu hadi akapitiwa na u…