SHEREHE KUZIMU (30)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA THELATHINI ILIPOISHIA... “MGONJWA ALIYECHOMWA KISU AENDELEA KUDUNDA.” Gazeti la Kiu . Licha ya magazeti mbalimbali kupambwa na habari hiyo lakini pia redio, televisheni, na mitandao ya kijamii iliripoti maendeleo ya Benedict hospitali. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Waungwana walilaani vikali tukio la kutaka kuuwawa kwa mgonjwa huyo. Hata hivyo mashirika binafsi na taasisi mbalimbali zilitoa rai kwa serikali kuhimarisha ulinzi dhidi ya kijana huyo. Majuma kadhaa mbeleni, daktari mkuu kitengo cha mifupa , alimtembelea Benedict wodini na kukuta hali yake inazidi kuwa njema. Alipendekeza kwa vile fahamu zimemjia basi utaratibu wa kuwasiliana na ndugu zake ufanyike muda wowote kwanzia saa ile. Daktari wa zamu alipewa jukumu hilo la kusimamia zoezi la Benedict kutoa utaratibu wa kuwasiliana na nyumbani kwao. “ Daktari Fransisco , ambaye ndiye aliyepewa…