SHEREHE KUZIMU (34)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA THELATHINI NA NNE ILIPOISHIA... Alijua kuwa mpenzi wake atakuwa ameteketea ndani ya moto ule. Hakuona sababu ya kuendelea kuishi bila kuwa na Benedict maishani. Alichukua uwamuzi wa kukimbilia ndani ya nyumba ili na yeye aweze kuteketea na mpenzi wake. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Malengo yake hayakufanikiwa kwasababu alikamatwa na askari wa zima moto. Adela alizidi kulia kwa uchungu hadi mashuhuda wa tukio lile wakamuonea huruma. Baada ya kulia kwa muda mrefu alipoteza fahamu hadi saa mbili asubuhi alipojikuta yupo hospitali. Mshumaa uliokuwa unaangaza nuru maishani mwake tayari ulikuwa umeshazimika. Aliyachukia maisha kiujumla. Alihisi moyo wake umepata jeraha ambalo hakujua litapona mwaka gani. Hakuona sababu ya kuendelea kukaa jijini Mwanza , ili hali kilichokuwa kimempeleka kilikuwa kimefikia tamati japo kwa maumivu makubwa. Aliondoka ho…