SHEREHE KUZIMU (35)

Zephiline F Ezekiel
SHEREHE KUZIMU (35)
Jina: SHEREHE KUZIMU Mtunzi: Frank Silaa SEHEMU YA THELATHINI NA TANO ILIPOISHIA... Mume wake na mwanae walikuwa tayari wameshatangulia mkutanoni. Baada ya kupingana kwa muda mrefu na nguvu ile iliyokuwa inamsukuma hatimaye alijikuta njiani, akitembea kwa mwendo mkali kuelekea kule kwenye mkutano. KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA NAYO... Kwa vile hapakuwa mbali sana muda mfupi baadae alifika eneo la tukio. Ghafla mapepo yaliyokuwa ndani yake yalianza kufurukuta kwa vile lile eneo halikuwa la kawaida. Wahudumu walijaribu kumshika lakini hakushikika kwa vile alikuwa na nguvu zisizo za kawaida. Alianza kukimbia kuelekea madhabauni ambapo kulikuwa na watumishi mbalimbali wa Mungu. Watu wote waliacha kusikiliza mahubiri na kumtazama Vivian ambaye alionekana kuwa na mapepo hatari. Alikuwa akilia kama paka, wakati mwingine alijongea mithili ya nyoka mwenye sumu kali. Watumishi wa Mungu, walianza kufanya maom…