BABA KIUMBE WA AJABU (13)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KUMI NA TATU TULIPOISHIA... Wazo lile nilitaka nishauriane na mwenzangu kabla ya kutoa uamuzi, nilipanga akija nitamgusia suala lile ambalo kwa upande wangu lilichukua sura mpya ya kutishia maisha yangu. Wakati nikiwa kwenye dimbwi la mawazo mpenzi wangu aliingia kwa hali aliyonikuta nayo ya kujilaza mikono kichwani ilimshtua sana. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... “Vipi?” “Masalu?” “Mambo mazito.” “Kivipi?” Nilimueleza niliyokutana nayo nyumbani, alibakia mdomo wazi asiamini nilichomueleza. “Sasa bila kugongwa na gari ingekuwaje?” “Hata sijui.” “Sasa kwa nini mganga hakukuambia?” “Aniambie nini wakati aliniambia nitakayoyaota ndotoni ndiyo nitakutana nayo?” “Sawa, lakini alitakiwa akupe tahadhari.” “Mganga hawezi kukuambia kitu kijacho kabla ya kutokea ili usije sema uongo.” “Pole sana mpenzi wangu sasa tutafanya nini?” Mara simu yangu iliita nilipoang…