BABA KIUMBE WA AJABU (15)

Zephiline F Ezekiel
BABA KIUMBE WA AJABU (15)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KUMI NA TANO TULIPOISHIA... “Nashukuru mzee wangu.” “Basi ondoa hofu hakuna chochote kitakachokukuta, kila atakayekugusa kitamrudia.” Niliagana na mganga kisha nilimpitia mpenzi wangu na kurudi hotelini kujiandaa na kwenda msibani. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... Tukiwa njiani simu ya dada iliita, nilitaka kuacha kuipokea lakini niliipokea ili nijue ana shida gani. “Haloo,” nilipokea. “Asante Masalu, asante sana.. njoo umle nyama baba,” dada alisema kwa sauti iliyoonesha analia. “Tena wewe ndiye ninayekutafuta mchawi mkubwa , nakuapia sitakusamehe wewe na wote hata marehemu baba  mpaka nakufa. Vitendo vyote mlivyonitendea hamkuridhika mpaka mnaitaka roho yangu kwa nguvu? Hivi nikifa mtafaidika nini?” “Nani anataka kukuua?” “Kitendo mlichofanya wiki moja iliyopita sitawasamehe mpaka nakufa, mnanilaumu nahusika na kifo cha baba. Hebu niambieni mimi …