BABA KIUMBE WA AJABU (16)

Zephiline F Ezekiel
BABA KIUMBE WA AJABU (16)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KUMI NA SITA TULIPOISHIA... “Japo unakuhusu lakini mazingira yake hayakuwa mazuri.”  “Yawe mazuri vipi ikiwa aliyekufa ni mzazi wangu?” “Sawa mzazi wako lakini unajua kifo chake kilitokana na nini, Na dada yako  baada ya kifo cha baba yenu maneno aliyokuambia, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... sasa nini kigeni kwako?” “Nimekuelewa, lakini watanitambua.” “ Masalu jambo hili linahitaji utulivu, nakuomba tuondoke hapa twende sehemu yoyote ili upate utulivu wa moyo.” “Nashukuru kwa kunipa moyo na kuwa mtu wangu muhimu.” “Najua upo katika kipindi kigumu hivyo nahitaji kuwa karibu yako na kuhakikisha hupati mawazo mabaya. Nina imani utavuka kipindi hiki kigumu.” “Nashukuru sana, sasa tutakwenda wapi?” “Twende Musoma au Shinyanga.” “Mi nafikiri Musoma panafaa.” “Vipi kuhusu duka linaendelea?” “Hata najua.” Kwa kweli nilijibu nikiwa sijui nini kinaendelea, muda …