MWAJUMA UTAMU (1)

Zephiline F Ezekiel
Mtunzi: Juma Hiza

SEHEMU YA KWANZA
Nakumbuka ulikuwa ni mwaka 2010, nilipata bahati ya kufanya kazi za ndani katika nyumba moja iliyokuwepo maeneo ya Kijitonyama. Ilikuwa ni familia ya Mzee Gidion pamoja na mke wake ambapo katika maisha yao walifanikiwa kupata watoto wawili, mtoto wa kwanza alikuwa ni wa kiume aliyejulikana kwa jina la Daniel na mwingine wa mwisho alikuwa ni wa kike aliyejulikana kwa jina la Naomi.

Mzee Gidion alikuwa akimiliki kampuni moja hapa mjini iliyomuingizia kiasi kikubwa cha pesa, aliishi maisha mazuri yeye pamoja na familia yake.

Baada ya kupita miezi mitatu tangu nilipoanza kufanya kazi za ndani katika nyumba hiyo Mzee Gidion alianza kunitamani, alichokuwa akikihitaji ni penzi langu tu, aliahidi kunifanyia mambo mengi sana katika maisha yangu endapo kama ningekubali ombi lake la kulala naye kitanda kimoja.

Kiukweli lilikuwa ni jambo gumu mno hasa ukizingatia mke wake ndiye aliyenileta katika nyumba hiyo kwa lengo la kufanya kazi, sikuwa tayari kumkubalia ombi lake lakini kutokana na tamaa za pesa zilizoniingia nikajikuta nikimkubalia na kuanzisha mahusiano naye ya kimapenzi.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kushiriki mapenzi tangu nizaliwe, Mzee Gidion ndiye alikuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu, alionekana kufurahishwa sana na kitendo hicho, kwanza hakutegemea kama angeweza kunikuta na usichana wangu mpaka kufikia umri wa miaka ishirini niliyokuwa nayo, hilo lilizidi kumfurahisha mno.

Niliendelea kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Mzee huyo ambaye aliniambia nilitakiwa kufanya siri, hakutaka mke wake afahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alinitahadharisha niwe makini kwani kama mke wake angeweza kufahamu mahusiano yetu ningejiingiza katika matatizo makubwa.

Hilo halikuwa tatizo, niliendelea kuwa katika mahusiano na Mzee Gidion huku penzi lake likizidi kuniteka. Ukumbuke kuwa Mzee Gidion ndiye alikuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu, alikuwa amenifungulia dunia mpya ya mapenzi, hapo kabla nilikuwa ni mtu wa kuyasikia mapenzi jinsi ambavyo watu walivyokuwa wakiyasifia pamoja na utamu wake, sikuwa nikifahamu lolote kuhusu mhemko na raha ambazo mtu alikuwa akizipata wakati akifanya mapenzi.

Tangu nilipofanikiwa kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza na Mzee Gidion nilijihisi kuwa kiumbe kipya, nilijiona kukamilika kuwa msichana.

Kipindi hicho Mzee Gidion alianza kunijali, alikuwa akinipa kiasi cha pesa chochote nilichokuwa nikikihitaji.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
"Msichana mrembo kama wewe unatakiwa uwe na simu kali, upendeze yaani ubadilike, uishi kimjinimjini, nitahakikisha nayabadilisha maisha yako Mwajuma," aliniambia Mzee Gidion.

"Nitashukuru Baba," nilimwambia.

"Usiniite Baba, sifananii kuwa Baba yako mzazi hata wa kuchorwa, niite mpenzi au Gidion tu inatosha," aliniambia.

Kwa kumtazama Mzee Gidion alionekana kuwa Baba yangu kabisa, alikuwa ni Mzee wa makamo ambaye alifanikiwa kuwa na watoto wawili. Kipindi hicho Daniel ambaye ndiye mtoto wake wa kwanza alikuwa akisoma chuo kikuu cha Daresalaam, alikuwa akisomea sheria, ulikuwa ni mwaka wake wa pili.

Kwa upande wa Naomi alikuwa kidato cha tatu, alikuwa akisoma Morogoro katika shule moja ya bweni, maisha yake yote yalihamia huko mpaka wakati wa likizo ulipofika ndipo ambapo aliweza kurudi nyumbani.

Unaweza ukaona jinsi ambavyo maisha yalivyokuwa katika nyumba hiyo, kila mtu alionekana kuwa bize na mambo yake, kuanzia Mama, Baba na watoto, muda mwingi nilibaki peke yangu nyumbani.

Mzee Gidion aliitumia nafasi hiyo kuwa fursa ya kuwa karibu na mimi. Aliamua kuninunulia simu kwa lengo la mawasiliano, alihitaji kuwasiliana na mimi zaidi na zaidi.

Siku ziliendelea kukatika huku penzi kati yangu na Mzee Gidion likizidi kupamba moto. Alipanga kuninunulia nyumba pamoja na gari la kifahari kwa dhumuni la kunihamisha nyumbani hapo, hakutaka kuona mapenzi yetu yakiendelea kuwa siri, alinogewa na utamu wa penzi langu.

Nilijisikia furaha sana kusikia hivyo, niliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kusahau umasikini niliyotoka nao nyumbani kwetu Mtwara.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kiliniweka katika wakati wa furaha sana, nilizidi kumpenda Mzee Gidion, nilisahau kama alikuwa ni mume wa mwanamke aliyenitoa kijijini na kunileta mjini kwa lengo la kufanya kazi, ahadi nilizowaahidi wazazi wangu pamoja na kiapo nilichokiapa mbele yao kwa wakati huo nilikuwa nipo kinyume kabisa.

Katika kipindi hicho ambapo nilikuwa katika mapenzi na Mzee Gidion, Daniel mtoto wa Mzee huyo na yeye alianza kunitamani, sijui nilimvutia na nini ila nilishangaa akinitongoza, alionekana kunihitaji kupita maelezo.

"Daniel embu acha kunitania bhana," nilimwambia huku nikionekana kutomuamini kabisa.

"Sikutanii Mwajuma kweli nakupenda, nahitaji kuwa na wewe," aliniambia Daniel.

"Umenipendea nini sasa?" nilimuuliza.

"Vingi tu vingine siwezi kukuambia," alinijibu.

Unajua kwanini sikuweza kumuamini Daniel? Kwanza alikuwa ni mtoto aliyetokea katika familia ya kitajiri, alikuwa ni msomi ukiachana na mimi ambaye nilifeli kidato cha nne, pili alikuwa ni handsome, alivutia mno, kwa kumtazama ilikuwa ni vigumu kuamini mvulana kama yeye kukosa msichana.

Alinisumbua sana, kila siku ombi lake lilikuwa ni moja, kuna kipindi nilimuonea huruma alipoingia chumbani kwangu kisha akawa ananibembeleza nimkubalie. Haikuwa rahisi kumkubalia kwani tayari nilikuwa katika mapenzi mazito na Baba yake na tulikuwa kwenye mipango mingi, nilikuwa nikisubiria itimie.

"Hapana Daniel siwezi kukubali hilo litokee wewe ni kama kaka yangu," nilimwambia Daniel.

"Mwajuma nakupenda, macho yangu yamekutazama wewe, una kila sababu za kuwa na mimi, umeuteka moyo wangu wa mapenzi tafadhali naomba usiuumize nitakufa," aliniambia Daniel huku machozi yakimlengalenga.

Nilishindwa kuvumilia kumuona Daniel akiendelea kuteseka kwa ajili yangu, nilimuonea huruma sana, mwisho wa siku nikajikuta nikishawishika na kumkubalia tukawa wapenzi.

Daniel alifurahi sana, hakuamini kama alifanikiwa kunipata huku nyuma ya pazia hakujua nini kilichokuwa kikiendelea kati yangu na Baba yake.

Kitendo cha kumchanganya Baba na mtoto kimapenzi hakika kilikuwa ni hatarishi sana, sikutaka kumwambia lolote Daniel, nilihofia mambo mengi mabaya ambayo yangeweza kunitokea.

Nilizidi kufaidi utamu wa penzi la Baba na mtoto huku kila mmoja kwa nafasi yake akikiri kunipenda kupita kawaida.

Siku ziliendelea kukatika, Mzee Gidion alianza kuingiwa na wasiwasi juu yangu, alihisi kuna mchezo mchafu ambao nilikuwa nikimchezea, hakutaka kuamini jambo hilo hata mara moja, alianza kufanya uchunguzi wake na mwisho wa siku akafanikiwa kugundua kuwa nilikuwa nikitembea na mtoto wake. Hilo lilimuumiza sana, alinilaumu mno. Naweza kusema siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kumuona mwanaume mtu mzima kama Mzee Gidion akilia mbele yangu huku sababu ikiwa ni mapenzi, hakutaka kuamini kama yeye pamoja na mtoto wake walishiriki mapenzi na mimi.

Mzee Gidion alipagawa, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, moyo wake ulimuuma mno, aliponitazama alionekana kuwa mwenye hasira, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.

Nilishindwa kuamua la kufanya kwani mpaka kufikia muda huo nilikuwa tayari nimeshafanya makosa. Kwanza nilikuwa nikitembea na mume wa mtu kwa kujua, pili niliwachanganya kimapenzi baba na mtoto. Haya yalikuwa ni makosa ambayo kiukweli sikuwahi kukaa na kuwaza kwamba kuna siku yangeweza kunigharimu maisha yangu.

Nilishindwa kuvumilia kumuona Mzee Gidion akiendelea kulia mbele yangu kama mtoto mdogo, ilibidi nimsimulie kila kitu kilichotokea kwa Daniel mpaka nikajikuta nikimkubalia na kuwa wapenzi, sikuacha kumuomba msamaha kwa kosa nililokuwa nimelifanya, nilikiri kukosea na kumuahidi kutorudia tena makosa.

Baada ya kumueleza hayo pamoja na kumuomba samahani Mzee Gidion hakutaka kunielewa kabisa, alinichukia, alinifananisha na kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima.

Hilo lilizidi kuniumiza mno, kitendo cha kuniita kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima hakika kiliniumiza sana, moyo wangu ulikuwa kwenye maumivu makali mno.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuishi maisha ya visasi kila siku, Mzee Gidion alikuwa ni mtu wa kunitishia maisha, alinikosesha amani ya moyo niliyoishi nayo kwa muda mrefu, sikuwa huru tena, muda wote nilikuwa nikimfikiria pamoja na vitisho alivyokuwa akinipa.

Kuna kipindi nilitamani kumueleza mke wake ukweli wote wa kile kilichokuwa kikiendelea kati yangu na mume wake lakini unafikiri ningeanzia wapi? Ningeupatia wapi ujasiri huo wa kumueleza kila kitu na wakati hapohapo tayari nilishamkosea kwa kitendo cha kutembea na mume wake.

Hiyo iliendelea kubaki siri ya moyo wangu, siri iliyokuwa ikinitesa mno. Mzee Gidion hakuacha kushiriki kufanya mapenzi na mimi, aliendelea kunitumia kimwili lakini safari hii haikuwa kama hapo awali, alibadilika na alikuwa akifanya mapenzi na mimi kama sehemu moja wapo ya starehe, yaani alinifanya kuwa kama kahaba ambaye alinitumia wakati alipohitaji kufanya mapenzi tu. Hilo liliniumiza sana, siwezi kusema ni maumivu kiasi gani niliyokuwa nayo katika moyo wangu lakini naweza kusema tamaa zangu za pesa ndizo zilizonipelekea nipitie katika wakati huu mgumu.

Daniel alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuigundua tofauti yangu japo Mama yake alianza kuniuliza kuhusu mabadiliko yangu lakini nilimficha, sikutaka kumueleza ukweli.

"Niambie nini kinachokusumbua mpenzi, malaika, mke, malkia wa maisha yangu," aliniuliza Daniel.

"Hakuna kitu," nilimjibu.

"Usiniambie hakuna kitu wakati nikikuangalia nakuona kabisa kuna kitu unanificha," aliniambia.

"Kweli hakuna kitu."

"Usinifiche tafadhali."

"Naogopa kukuambia Daniel."

"Unaogopa nini wewe niambie au mimba imengia?"

"Hapana bora ingekuwa mimba ningejua baba yake yupo."

"Ni nini sasa?"

"Ni kuhusu baba yako."

"Amefanyaje?" aliniuliza Daniel kisha nikaanza kumsimulia kila kitu. Nilipomaliza kumsimulia nikamuona akivuta pumzi ndefu na kuziachia kwa pupa, kama ilivyokuwa kwa Baba yake na yeye pia hakutaka kuamini, kitendo cha kuwachanganya kimapenzi na Baba yake kilimuumiza mno.

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni