
Mtunzi: Ally Mbetu
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Masalu utajiri wetu una siri nzito.”
“Siri! Siri gani hiyo?”
“Masalu utajiri wetu una siri nzito ambayo mimi ndiye niliyeibeba na sasa hivi nimeitua.”
“Una maana gani kusema hivyo?”
“Masalu kuna mambo huwezi kuyajua kutokana na umri wako,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
SASA TUENDELEE...
lakini kutokana na ukaribu na kuelewana kwetu sina budi kukufunulia yaliyojificha ili ujue nini kimetuzunguka. Mwanzo nisingeweza kukuambia kwa vile nimeelezwa kuwa maisha yangu hayatakuwa marefu hivyo leo nimefurahi sana kuja hapa. Haya nitakayokueleza leo si ya kutunga na kila ulilokuwa na swali nalo leo nitakupa jibu lake.
“Masalu mdogo wangu maisha yetu kabla hujazaliwa yalikuwa ya kawaida tu, baada ya baba kustaafu kazi pesa alizolipwa alinunua nyumba mnayoishi sasa hivi na pick up moja ambayo alifanyia kazi zake za kutuingizia kipato na kufungua duka ambalo lilikuwepo muda mrefu toka nikiwa darasa la nne.
“Maisha yaliendelea kama kawaida huku tukionekana familia yenye uwezo kwa sisi wote kusoma elimu nzuri. Walionitangulia wote walisoma elimu ya sekondari, lakini mimi nilipomaliza darasa la saba sikuweza kuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza.
“Lakini niliamini ningeendelea kusoma shule ya kulipia kama ndugu zangu walionitangulia. Wakati tukifanya taratibu za kunichukulia fomu ya kuanza kidato cha kwanza, siku moja nikiwa natoka chooni usiku kuna kitu kilinigonga mguuni. Nilipiga kelele kuomba msaada.
“Baba na mama walitoka na kuja nilipokuwa nimeshika mguu huku nikirukaruka, lakini ajabu hakukuonekana kitu chochote cha kuwashtua kutokana na nilivyokuwa. Nikiwa na wasiwasi labda nimegongwa na nyoka baba alinipa dawa ya maumivu na kunieleza patapoa tu.
“Usiku nililala vizuri, lakini asubuhi nilipoamka nilikuta mguu umevimba hata kutembea sikuweza. Sehemu ya juu kidogo ya mguu wa kulia kwa ndani kuliweka alama nyeusi, sikupelekwa hospitali zaidi ya kukandwa na dawa ya majani. Basi mdogo wangu mguu huo umenisumbua kwa muda mrefu bila kupelekwa hospitali.
“Hata muda wa kwenda shule ulipofika sikuweza kupelekwa shule kutokana na hali ya mguu wangu. Mpaka kipindi cha uandikishaji wanafunzi kinakwisha bado hali yangu ilikuwa tete hivyo sikuweza kujiunga na sekondari. Roho iliniuma rafiki zangu wengi walianza kidato cha kwanza. Nikawa mimi na ndani ndani na mimi, sehemu iliyokuwa na weusi ilikuwa ikiwasha na mwisho iliweka kidonda.
“Ajabu baada ya kutoka kidonda, mguu ulirudi katika hali yake ya kawaida, hata mti niliokuwa natembelea niliutupa. Niliona kama muujiza mguu wangu kurudi katika hali yake, niliamini mguu wangu ulikuwa wa kukatwa tu baada ya wazazi wangu kutoonesha juhudi zozote za kunipeleka hospitali.
“Hata nilipoweza kutembea sikuruhusiwa kutoka nje kama wenzangu, maisha yangu yalikuwa ya uani, kidonda changu kila siku kilikuwa kikivuja maji. Mdogo wangu wakati huo sikujua kama kidonda kile kilikuwa na sababu yake. Hali ya maisha nayo ilibadilika, kulitokea mabadiliko makubwa sana.
“Kwa muda mfupi tulinunua magari, kuongeza majumba kila kona ya Jiji la Mwanza na miradi mingi, ndugu zangu walifunguliwa maduka makubwa Mwanza mjini na mimi kukabidhiwa duka la pale nyumbani ambalo liliongezwa vitu vingi. Naimani mpaka unapata ufahamu ulinikuta dada yako nina kidonda mguuni.
“Siku zote nilihoji kwa nini wazazi wangu hawataki kunipeleka hospitali au kuniwekea dawa. Baba alinieleza kuwa kama wataniwekea dawa ya aina yoyote kidonda mguu utaoza, akaniambia kitapona chenyewe, nami nilikubali mwanzo bila kujua mwisho wake utakuwa nini.
“Pia nilipewa masharti ya kutotembea na mwanaume, nikaambiwa nikifanya hivyo nitakufa. Kwa vile umri wangu ulikuwa mdogo usiotakiwa kujiingiza katika mapenzi halikunisumbua sana. Siku zilizidi kukatika huku maisha yakibadilika kila siku, nami nilivunja ungo wa kuwa na hamu ya wanaume.
“Katika wateja wangu kuna kijana mmoja ambaye kwa kweli tulipendana naye sana na kunitamkia kuwa anataka kunioa si kunichezea baada ya kumueleza simjui mwanaume. Nilimueleza mama ambaye alinikemea sana kuwa nisirudie tena kusema kitu kama kile nitaweza kukorofishana na baba.
“Kutokana na kumuogopa baba niliamua kukaa kimya, siku zilikatika huku utajiri wa baba ukizidi kuwa wa kutisha na ndugu zangu wote wakinunua magari ya kifahari na kujenga maghorofa. Kila nilipotaka na mimi kuhama nyumbani na kuanzisha duka langu, kununua gari zuri na nyumba ya kifahari kama wenzangu nilizuiwa.
“Ajabu nilikaripiwa sana tena eti nisirudie tena kusema hivyo, majibu ya mama yalinishtua sana na kujiuliza iweje wote wawe na maisha mazuri kasoro mimi? Nilijiuliza labda mimi si mtoto wa mzee Makumiyane, lakini mama alinihakikishia ni mtoto halali wa mzee Makumiyane.
“Na hilo niliamua kuliacha kutokana na kumuogopa sana baba, muda ulivyokuwa ukienda ndugu zetu wote waliondoka na kuanzisha maisha yao na kubakia sisi wawili na wazazi wetu. Roho iliniuma sana siku ndugu zangu walipokuja kututembelea, kila mmoja alikuja na gari la kifahari. Hiyo ilikuwa tisa, kumi ilikuwa harusi za ndugu zangu ambazo ziliniumiza roho na baada ya muda walipata watoto.
“Nilijikuta nikijitoa mhanga na kumfuata baba kumuomba haki yangu kama wenzangu, baba alinigombeza kama ilivyokuwa kawaida yake. Lakini nilimueleza kuwa kama hataki basi kuna siku nitatoroka na kwenda kuanzisha maisha yangu kutokana na yeye kutoonesha kunijali au kunipa haki sawa na wenzangu.
“Alinitisha kama nitajaribu kutoka nyumbani nitamtambua, vitisho vyake havikunibabaisha baada ya kuona sina faida ya kuwepo pale eti kisingizio nina duka. Siku iliyofuata nilibeba kila kilicho changu na kuondoka, mama alinibembeleza nisiondoke lakini sikubadili uamuzi wangu. Ilibidi akimbiliwe baba alipokuja alishangaa uamuzi wangu.
“Nilimueleza nipo tayari kwa lolote atakalotaka kunifanyia, msimamo wangu ulimtisha sana baba na kuamua kuniweka chini na kunieleza siri iliyoniacha mdomo wazi.
“Nikabakia mimi siolewi, sina maisha mazuri, sina mtoto. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia. Nakumbuka siku moja kijana ambaye alitaka kunioa alikuja na kuniulizia ombi lake, siku ile baba na mama walikuwa wamekwenda kwenye sherehe ya mtoto wa dada aliyekuwa akipata ubatizo.
“Siku ile mdogo wangu lazima niseme ukweli kwa vile sina jinsi, nilitoka na kwenda kwa yule kijana na nilifanya naye mapenzi. Kwa kweli penzi nililopata lilinichanganya nikawa sisikii wala sioni. Ilifikia wakati wa kutoroka usiku kwa kuruka ukuta na kwenda kwa yule bwana.
“Mchezo ulinichanganya sana hata kutamani kuhama nyumbani.
“Kumbe kufanya kwangu mapenzi kulikuwa kunasababisha matatizo katika familia, kwa wiki moja kulitokea mambo ya kutisha. Moja nyumba ya Malimi iliungua moto na hakuna kilichosalimika, kabla hatujatulia gari la kaka lilipata ajali mbaya iliyosababisha lisirudi tena barabarani.
“Baba naye alivamiwa na majambazi akipeleka pesa benki za mauzo ya mwezi mzima. Hali ile ilimchanganya baba na kwenda kwa mganga wake kuulizia sababu ya majanga yale. Jibu aliambiwa mali imeingia uchafu kwa mimi kufanya mapenzi.
“Baba alikuja juu na kunitishia, nami sikumuogopa nilimueleza ukweli kama mimi ndiye chanzo cha utajiri kwa nini niwe na maisha duni wakati watu wasiojua adha niipatayo kutokana na mali wanazochezea kuishi maisha mazuri. Nilimueleza baba kuwa kama hatanipa mali tena iwe zaidi ya ndugu zangu wote lazima nitaondoka na kwenda kuishi maisha yangu.
“Baba alinitisha kwa kusema kama nitaondoka sitakaa muda mrefu lazima nitakufa, vitisho vile sikuviogopa na kumhakikishia kuwa nitaendelea na msimamo wangu na nipo tayari kufa lakini si kuwa kitega uchumi cha watu. Mama naye aliingia kwenye kazi ya kunibembeleza ili nibadili tabia zangu zilizoonekana chafu.
“Nilikubali kubaki nyumbani kwa masharti na mimi natakiwa niwe na gari na duka kubwa ambalo nitalimiliki mwenyewe. Tulikubaliana na mimi kufuta wazo la kuondoka nyumbani. Nilisubiri kutekelezewa niliyoyataka kwa hamu kubwa, nami nilikuwa na hamu ya kuendesha gari, nilikuwa na hamu ya kumiliki mali yangu mwenyewe.
“Siku zilikatika bila kuona dalili zozote za kununuliwa gari wala nyumba, wakati huo nilikuwa nimesimamisha mapenzi na shemeji yako. Mambo yalizidi kunyooka kwa Malimi aliyeunguliwa nyumba yake kujenga ghorofa analoishi sasa.
“Lakini mwenyewe sikuona kitu chochote, kila nilipouliza niliambiwa nisubiri mambo hayajakaa vizuri. Mambo hayajakaa vizuri wakati ndugu zangu kila kukicha walibadilika kimaisha? Niliona kama wananichezea, nikaanza kuweka pesa zangu taratibu bila kumshirikisha mtu.
“Shemeji yako nilimtuma anitafutie sehemu ya kufungulia duka akapata huku, nilimpa pesa za kulipia mwaka mzima na kumuagiza anunue vitu vyote muhimu kwa ajili ya duka naye alifanya kama nilivyomuagiza. Unajua Masalu katika maisha yangu huwezi kuamini toka nipatwe na tatizo la mguu lililozaa kidonda sikuruhusiwa kwenda kanisani.
“Ndugu zangu wote ndiyo waliokuwa wakienda kanisani, lakini mimi nilizuiwa kwa kuambiwa kama nitakwenda kanisani nitasababisha maafa makubwa kuliko yale ya kutembea na mwanaume. Nilijiuliza mimi ndiye sitakiwi kwenda kanisani lakini wadogo na dada zangu wote mlikuwa mnakwenda, kwa nini?
“Nilikatazwa hata kusoma Biblia, baba alisema mizimu haitaki kuchanganya mambo ya Mungu na mizimu. Basi nilibakia simjui Mungu wala kanisa. Baada ya kukamilisha vitu vyote muhimu vya dukani, shemeji yako alilisifia duka alivyolijaza. Nilijipanga kwa siri na siku moja nilitoroka usiku na nguo zangu bila wao kujua. Masalu siku mlipoamka na kunikosa ilikuwaje nyumbani?” Dada Monika aliniuliza huku akiwa ametuliza macho usoni kwangu.
“Mmh, kwa kweli walichanganyikiwa sana, walihaha kila kona, familia yote iliitwa asubuhi ile na kukutana. Hata mimi nilizuiwa kwenda shule, kilikuwa kikao kizito kilichokujadili. Niliwasikia wakisema bila kukuona kila kitu kitaharibika, siku ile hakuna kazi iliyofanyika, maduka yote yalifungwa na kuanza kukutafuta.”
“Basi mdogo wangu nilikuja huku kuanza maisha yangu ili kupata uhuru wa maisha wa kupanga mambo yangu bila kuingiliwa na mtu. Pesa niliyokusanya niliamini mpaka iishe nitakuwa nimepiga hatua kubwa katika biashara kwa vile nilikuwa naijua vizuri.
“Walianza upelelezi wa chinichini na kumjua mpenzi wangu ambaye walimbana kwa kumpeleka polisi ili awajulishe nilipo. Mwanzo aligoma kutokana na masharti niliyompa kama wazazi wangu watamuona asikubali. Mpango wetu ulikuwa kuishi pamoja nami nilitaka yeye asirudi tena kule.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi