BALAA (3)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... "Au unahamu…..?" Dokta Kilumba nae aliuliza swali lililoelea hewani, bila kutanabaisha Dokta Yusha alikuwa na hamu ya nini. "Mbona siwaelewi ndugu zangu" Dokta Yusha aliongea kwa sauti ndogo iliyokuwa ikiashiria kutoelewa kinachoendelea. "Naitwa Tamaa Karimu, unaitwa Yusuph Shaweji, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... sina undugu na wewe na wala sijawahi kuwa na undugu Na wewe, labda hawa wenzangu ndio ndugu zako" "Nani, mimi nitakuwa na ndugu kama huyo?" Dokta Sharifa alirukia kwa mtindo wa swali. "Lazima niwe makini, kuna kitu kinaendelea" Dokta Yusha alijionya mwenyewe kimoyomoyo. Wakati wanaongea na Dokta Yusha, lile kundi la wauaji walikuwa wamejipanga vizuri kule katika chumba cha kuhifadhia maiti . Tayari kwa kulinda usalama ili wale madaktari waje kufanya mchezo wao hatari. Mchezo wa kutoa mio…