
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Jumba ambalo hakuwa anajua linalindwa na walinzi wangapi, jumba ambalo hakujua ni aina gani ya ulinzi wanaoutimia. Ni mbwa ama binadamu? 'Bora nife kwa bastola, bora nife kishujaa, kuliko kufa kwa njaa!" Dokta Yusha aliiokota ile bunduki iliyokuwa inatumiwa na Sita, SMG ambayo dokta Yusha alikuwa anajua kuitumia. Alifunzwa Kiwira Mbeya, katika Chuo cha Magereza,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
na alishawahi kuitumia mara kadhaa huko Mtwara, alikoajiriwa. Dokta Yusha alipiga hatua za taratibu kuelekea nje ya chumba kile. Chumba alichoambiwa ndio kaburi lake. Kwa maana hiyo Dokta Yusha sasa alikuwa anatoka katika kaburi lake! Nje kulikuwa na giza, ingawa si kubwa sana kama la mle ndani. Nje angalau kulikuwa na mbalamwezi, mbalamwezi ambayo ilimuwezesha kuona Dokta Yusha. Kwa mwendo wa kunyata Dokta Yusha alikuwa anatambaa na ukuta wa kile chumba
kuelekea upande wa mashariki, upande ambao lilikuwepo geti kubwa jeusi la nyumba ile. Aliishika imara ile bunduki iliyomdondoka Sita, tayari kupiga endapo atasikia ukelele wowote ule utakaotokea mbele yake. Dokta Yusha alikuwa tayari kwa lolote. Tayari kuuwa! Tayari kuuwawa! Aliambaa na ule ukuta wa bluu hadi akaumaliza, sasa ilimbidi apite sehemu ya wazi ili kulifikia geti. Sehemu hatari zaidi, sehemu ambayo ni rahisi sana kudunguliwa na risasi! Maana hakukuwa na kizuizi chochote. Alikwenda kwa haraka, kwa kusaidiwa na giza, au tunaweza sema kwa kudra za Mwenyezi Mungu, alilifikia geti.
Dokta Yusha aliangalia pembeni ya geti, alimwona mlinzi, mlinzi ambaye alikuwa amelala huku akitoa sauti mbaya ya kukoroma. Mlinzi mzembe sana akiyelinda nyumba hatari sana! Dokta Yusha alimsogelea yule mlinzi taratibu akijua kwa vyovyote funguo ya geti atakuwa nayo yeye. Alimfikia. Kwa kutumia mkono wake wa kulia alimpiga karate moja ya nguvu katika chembe, mlinzi hakuweza kustahamili uzito wa karate ile, alikufa usingizini. Alimpekua haraka haraka yule mlinzi, alikipata alichokitaka...funguo. Dokta Yusha sasa alikuwa anafungua geti la kutoka nje ya nyumba ile hatari, nyumba ambayo hakuna mateka aliyewahi kutoka hai baada ya kuingia mle.
Dokta yusha alifungua geti na kutokomea msituni akiwa na bunduki yake. Wakati Dokta Yusha, akitoroka kule kambini msituni. Kundi la Six killers walikuwa njiani wakirejea kambini kwao. Walikuwa wanatoka Kilwa Masoko mjini, walikoenda kufanya starehe zao. Wote walikuwa wamelewa ndani ya gari huku wanaimba nyimbo zisizoeleweka. Walikuwa na furaha sana baada ya kuona mipango yao inaenda kama ilivyopangwa, pia waliweza kumkamata mtu ambaye alikuwa anawasumbua sana, Dokta Yusha. 'Laiti wangejua'
*****
Katika hospitali ya wilaya Kilwa Kivinje hali ya wagonjwa ilikuwa mbaya sana. Kulikuwa hakuna huduma kabisa kwa wagonjwa wa hospitali hiyo. Madaktari waliokuwa wanaaminiwa sana kwa kutoa huduma nzuri sasa walikuwa wamebadirika. Walidharau sana wagonjwa, hawakuwajari kabisa. Malalamiko mengi yalipelekwa katika uongozi wa wilaya, lakini malalamiko hayo hayakubadirisha kitu. Madaktari hawa sasa walikuwa na pesa nyingi sana, pesa za kumuhonga mtu yeyote yule atakayeonesha kutaka kuwaingilia au kukwamisha mipango yao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa alikuwa kimya, mkuu wa wilaya ya Kilwa alikuwa kimya, na mbunge pia alikuwa kimya, ingawa walipelekewa malalamiko mara kwa mara huku hali za wagonjwa waliolazwa hospitali zikiendelea kuwa mbaya! Upande wa hali za Nasra, Hasina nazo zilikuwa taabani. Nasra alikuwa anapumulia mashine katika hospitali ile iliyokuwa na huduma dhaifu sana kwa sasa, Nasra alikuwa amehamishwa wodi na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, ICU, hali yake ilikuwa mbaya sana. Huku Hasina na Mzee Mpaukha wakiwa bado wanapigania maisha katika wodi ileile aliowaacha Dokta Yusha. Mwili wa marehemu dereva Musa ulikuwa ushatolewa katika ile wodi na kupelekwa machinjioni. Katika chumba cha kuhifadhia maiti ambako ndipo kundi la Six killers walikuwa wanafanyia shughuli zao.
Kutoonekana kwa Dokta Yusha siku nzima, ilizua hofu kwa ndugu zake. Dokta Yusha alitafutwa ule usiku lakini hakupatikana, na kwa bahati mbaya zaidi alikuwa hapatikani kwa simu yake pia. Hali ilikuwa ngumu sana kwa familia zote mbili. Familia ya Mzee Mpaukha na familia ya Mzee Yusuph, baba yake na Dokta Yusha. Dokta Yusha alikuwa anahitajika sana wakati ule, pengine kuliko wakati wowote ule, alikuwa mtu muhimu sana, licha ya kutaka kujua usalama wake mwenyewe, lakini pia alihitajika sana kuwahudumia wagonjwa wa pale hospitali, hasa kumuhudumia mkewe Nasra na rafiki wa mkewe Hasina, ambao walikuwa na hali mbaya kupita kiasi. Ndugu walitafuta sana. Lakini hawakumuona!
*****
Usiku huo Kundi la Six Killers nd'o walikuwa wanarudi kambini kwao, huko porini Ngome. Walishuka katika gari yao huku wakiwa na furaha kubwa sana. Furaha iliyotokana na pombe, furaha iliyotokana na mipango yao kwenda sawa. Taa za gari yao zilipomulika geti wote walipigwa na butwaa! Geti lao lilikuwa wazi, waliingia ndani moja kwa moja bila kusemeshana, walienda katika chumba cha mateka wao. Walimsahau hata kumwangalia mlinzi pale mlangoni. Mateka wao hakuwepo! Wakajaribu kumpigia simu Sita. Cha kushangaza hata Sita waliyemuacha kwa ajili ya kumlinda Dokta Yusha nae hakuwa anapatikana.
Walirudi tena getini, ndipo walimkuta mlinzi akiwa amelala, walipomgusa ili kumuamsha, mlinzi alidondoka chini moja kwa moja. Macho yaliwatoka vibaya sana! Hakika Dokta Yusha alikuwa kawaweza sana, ilikuwa haijawahi tokea hata siku moja kutoka mtu salama katika nyumba ile. Ilikuwa ni mwiko, ilikuwa ni dhambi kubwa sana kwao kutoka mtu katika nyumba ile akiwa hai! Ile nyumba ilikuwa ni zaidi ya kaburi, kile kiti kilikuwa ni mithili ya Israel mtoa roho. Nyumba ile ilikuwa imeondoka na roho za watu wengi sana. Roho za watu mbalimbali wasio na hatia, roho za askari wengi, roho za wapelelezi wengi, roho za viongozi wengi na roho za watu wa kawaida zisizo na hesabu. Kile kiti kilikuwa kimewageuza rangi watu wengi sana. Kutoka rangi yao ya asili,
kuwapeleka rangi nyekundu kisha nyeusi tii, kisha kutoa harufu kali sana. Kile kiti hakikuwahi kukosea katu. "Natoa nusu saa, Dokta Yusha awe mbele yangu hapa, hapana siyo Dokta Yusha, natoa nusu saa maiti ya Dokta Yusha iwe mbele yangu hapa. Maana akija mzima hapa nitamfanya kitu kibaya sana, naona bora mniletee maiti tu inatosha" Don Genge aliunguruma kwa hasira. Dokta Yusha sasa aligeuka mwiba. mwiba mkali sana! Vijana wa Six Killers, ambao sasa walibaki wanne tu. Maana Tano alikuwa anauguza goti lake, na Sita alikuwa hajulikani alipo mpaka sasa waliingia kazini.
Moyo wa Don Genge ulikuwa unafukuta moto, alikuwa na hasira isiyomithilika katika moyo wake. Ni kweli, Dokta Yusha angepelekwa hai pale, ingekuwa balaa! Walipotoka nje kundi la Six killers walijigawa. Wakati Moja na Nne wakielekea upande wa mashariki wa pori lile, Moja na Tatu walielekea upande wa magharibi. Kumsaka Dokta Yusha. Ilikuwa ni msake mpaka umpate! Wakati kundi la Six killers likijigawa namna hiyo kumsaka Dokta Yusha kwa kwenda upande wa mashariki na magharibi. Dokta Yusha alikuwa mbali kidogo na ile kambi ya wale makatili. Ilikuwa ni porini sana, Dokta Yusha alikuwa anasonga mbele akiwa hajui anaelekea wapi. Hadi sasa alikuwa hajui msitu ule upo sehemu gani nchini Tanzania.
Alikuwa anaenda mbele tu ili kukiepuka kifo. Na bunduki yake mikononi. Saa kumi na mbili asubuhi ilimkuta Dokta Yusha akiwa katika ufukwe mwanana wa bahari ya hindi. Ulikuwa ufukwe mpya ambao hakuwahi kufika wala kuuona hapo kabla. Moja na Nne, waliokuwa wanaenda upande wa mashariki, upande sahihi alioelekea Dokta Yusha. Huu upande kulikuwa na ufukwe wa bahari ya hindi ambao watu wengi ndani ya Kilwa walikuwa hawaufahamu. Moja na Nne nao walifika katika ule ufukwe. Ingawa ilikuwa mbali na pale alipotokea Dokta Yusha. Jamaa wakaanza kutembea ufukweni kumsaka Dokta Yusha. Dokta Yusha alikuwa amechoka sana, alikuwa anatembea taratibu ufukweni huku akiangalia nyuma mara kwa mara. Ufukwe ulikuwa mrefu sana, kiasi kwamba ni ngumu kumuona mtu aliye mbele yake.
*****
Kundi la Six killers walipewa nusu saa kupeleka maiti ya Dokta Yusha. Na sasa ni masaa mawili hawakuwa na maiti ya Dokta Yusha wala harufu ya Dokta Yusha. Mara kwa mara Don Genge alikuwa anawapigia simu vijana wake, lakini jibu lilikuwa lilelile, hawakuwa wamemuona Dokta Yusha. Mwishowe Don Genge aliwaambia vijana warudi kambini, ili waende kujipanga upya. Hiyo ndio ilikuwa nusra ya Dokta Yusha kukamatwa kule ufukweni mwa bahari. Dokta Yusha aliendelea kuufata ule ufukwe. Bila kujua ufukwe ule utamfikisha wapi? Lakini aliufata. Kambini kundi la Six killers walikutana. Kilikuwa ni kikao tofauti na vikao vyote walivyowahi kufanya. Kikao hiki kilitawaliwa na hasira, hofu na chuki!
Wote walikuwa na hasira kali kwenda kwa Dokta Yusha. Wote walikuwa na hofu ya kukamatwa na Polisi, maana yake walikuwa wanaamini Dokta Yusha alishaijua mahali ilipokuwa kambi yao, wote walikuwa na chuki, walikuwa wanamchukia sana Dokta Yusha. Ni yeye ndiye aliyeingilia kati mipango yao ambayo ingewawezesha kupata hela nyingi sana. Hela ambazo zingewawezesha kuwa matajiri milele. "Mambo yamebadilika haraka sana, sisi tulipanga hivi lakini mambo yanaenda vile. Sasa tumefikia katika hali mbaya sana, mipango yetu inaenda mrama, ndio...mipango yetu inaenda songombingo. Kidudu kidogo sana kinawasumbua. Kumbukeni nyinyi ni nusu makomando, mnashindwaje kumkamata mtu ambaye hajapita kozi yoyote. Tano na Sita nimewapoteza ilhali yule nyang'au hana hata jeraha letu.
Yaani Tano anapambana na kale jamaa na kukishindwa, hizo ni dharau, dharau kubwa sana, dharau zisizo na mfano. Natoa oda mpya sasa, ukimuona Dokta Yusha popote pale muue kwanza kisha nd'o umhoji. Hatutakiwi kufanya mchezo kabisa! Kumtafuta Dokta Yusha kwende sambamba na kutoa mioyo kule hospitali. Leo usiku tumepanga na Dokta Sharifa tuwatoe mioyo wale majamaa zake, ili imuumize, tukimuuwa mkewe na kumtoa moyo lazima atajitokeza, hapo ndipo tutamuuwa kirahisi" Don Genge alitoa hotuba ndefu huku kila mtu akikubali kwa kutingisha kichwa.
Kwa hakika, Kundi hatari la Six killers walikuwa wanataka kupiga pigo la mwisho! Baada ya maelezo hayo kila mmoja aliingia ndani kupumzika. Six killers walikuwa wamechoka sana. Wote pombe zilikuwa zimewaisha vichwani mwao. Ama hakika Six killers walikuwa wamepatikana, na kupata pigo kubwa sana, baada ya wapiganaji wao wawili kukutana na mkono wa Dokta Yusha! Wakati vijana wanne wa Six killers wakiwa wameenda kupumzika,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi