Machapisho

BALAA (15)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (15)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... Watu wote mle ndani walikuwa na nakala ya gazeti la Shupavu mkononi, wakisoma habari ile mbaya sana iliyoandikwa na Mwandishi wetu. Wote walikuwa wamejiinamia chini, wamekuwa wadogo mithili ya piriton. Gazeti la Shupavu lilianika kila kitu kuhusu wao na mipango yao. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... "Kuna msaliti kati yetu" Moja wa six killers aliropoka kwa sauti kubwa. Wengine wote walikaa kimya, kama hawakuisikia ile kauli toka kwa Moja. Kilipita kimya cha dakika kama tano, Tano ambaye sasa alikuwa amepata nafuu kile kidonda cha goti alivunja ukimya. "Hakuna msaliti..." "Ilaaa...." Moja alidakia kabla Tano hajamalizia alichotaka kusema. "Mimi nina wasiwasi Sita ametekwa, na ni yeye ndiye aliyetoa siri zetu hizi" Tano aliongea kwa upole. Don Genge alimwangalia Tano kwa jicho Kali huku akiteteme…