
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Na siku atakayoyokea tu huyo jamaa amkonyeze, kwa bahati nzuri siku ileile Tano alienda TigaTisa, na Daniel Mwaseba ndipo alipokonyezwa na yule Mhudumu. Daniel Mwaseba pale alipokaa alimuona vizuri sana Tano.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Bila wasiwasi wowote Tano alichagua meza moja iliyokuwa tupu na kukaa. Yule Mhudumu alienda Kumsikiliza Tano. Kisha alirudi tena kaunta kuchukua alichoagizwa. Daniel Mwaseba alimshuhudia Mhudumu akipeleka bia mbili katika meza ya yule jamaa, kisha akaondoka. Daniel Mwaseba alinyanyuka pale alipokaa na kuifuata ile meza aliyokaa Tano. Ghafla, Tano aliushuhudia ugeni asioujua katika ile meza yake. Tano alimwangalia kwa umakini mkubwa sana yule kijana mgeni aliyeivamia meza yake bila kukaribishwa. Yule kijana nae ( ambaye sisi tunamtambua kama Daniel Mwaseba) alitulia tuli, kama hakuwa amefanya jambo lolote lile ajabu.
Baada kama ya dakika moja ya ukimya, Daniel alimuita Mhudumu wa Baa ile kwa kutumia ishara ya mkono. Mhudumu alienda kwa mwendo wa taratibu akiwa anatetemeka, alijua anaitwa ili akayaeleze pale yote aliyomwambia Daniel Mwaseba kabla. Lakini haikuwa hivyo, alipofika pale Daniel alimuagiza maji makubwa ya baridi aina ya Kilimanjaro. Wakati Mhudumu akienda kuchukua maji. Ndipo Daniel alijitambulisha kwa yule jamaa mwenye mwili wa kibabe. "Naitwa Daniel Mwaseba.." Alivyolitaja tu hilo jina, kwa kutumia macho yake makini ya kipelelezi, Daniel Mwaseba aliona mstuko alioupata yule jamaa, ulikuwa mstuko mkubwa ulioiacha sura yake ikiwa katika hali ya kutahayari.
Bila shaka Tano hakutegemea kabisa kukutana na mtu mwenye jina kama lile. Kabla Daniel hajaongeza kitu chochote, Mhudumu aliyaleta maji ya Kilimanjaro makubwa aliyoyaagiza Daniel Mwaseba. Akayaweka juu ya meza pamoja na glasi ya wastani. Mhudumu aliondoka huku uwoga ukitapakaa hadi katika mwendo wake. Daniel Mwaseba alifungua ile chupa kubwa ya Kilimanjaro, akamimina maji nusu katika glasi, akanywa funda moja dogo. Alitulia akiyaruhusu maji yale ya baridi kupenya katika koo lake.
Aliyefanya hayo yote kwa umakini mkubwa sana. Kuhakikisha yule jamaa hafanyi ujanja wowote ule. Kwa upande Tano hakuwa tayari kabisa kulisikia jina la Daniel wakati ule. Mara nyingi sana alishazisikia sifa na umahiri wa Daniel Mwaseba katika mapambano. Kwa bahati mbaya zaidi alikuwa amekutana na Daniel Mwaseba akiwa mgonjwa, mgonjwa wa goti aliloumizwa na Dokta Yusha. Tano alijutia kitendo cha kuachana na wenzie kimoyomoyo, wangekuwa wote labda wangeweza kumkabili Daniel Mwaseba na kumzidi mbinu. Tano alitafakari kwa kina afanye nini ili anusurike katika kisanga kile, lakini hakupata, akili ilikuwa inagoma kabisa kuwaza.
Kila akiwaza akili ilikuwa inamrudisha palepale mezani na mbele yake alikuwa anatazama na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba. "Unaitwa nani mwenzangu?" Daniel aliuliza kwa sauti yake ya upole yenye kuonesha urafiki. Jamaa hakujibu, alikaa kimya kama hajaulizwa kitu. "Usinilazimishe nitumie nguvu kijana, nina nguvu za kukufanya chochote!" Sasa Daniel alisema kwa ukali kidogo. Tano alimwangalia tu Daniel Mwaseba, huku akitafuta namna sahihi ya kutoa bastola yake iliyokuwa kiunoni kwake. "Huwezi kuniwahi kwa bastola yako iliyopo kiunoni" Daniel alikijibia kitu ambacho Tano alikuwa anakiwaza tu kichwani kwake. Tano alistuka sana! Licha ya kusomea saikolojia ya wahalifu Daniel Mwaseba alikuwa na kipawa cha kutambua vitu vinavyopita katika kichwa cha Mhalifu. Daniel hakuujari mstuko wa Tano wa Six Killers. Yeye aliuliza swali lengine kabisa.
"Kwanini ulimuua Mwanasheria?" Tano hakujibu kitu, aliendelea kuwa bubu. "Naona umeshindwa kunijibu hapa tukiwa kama rafiki, sasa utanijibu mahala pengine tukiwa kama maadui" Daniel Mwaseba alichomoa bastola na kumuonesha Tano kwa siri sana. Hakuna mtu mwengine wa pembeni aliyeweza kuiona ile bastola kwa jinsi alivyooneshwa zaidi ya Tano mwenyewe. "Hii bastola nzuri sana, halafu ina kiwambo cha kuzuia sauti. Naweza nikakufumua kichwa chako kimyakimya bila mtu yoyote kutambua sababu ya kichwa chako kutawanyika! Naomba ufuate nitakachokuelekeza" Uso wa Tano ulistuka sana kutokana na kauli ya kitisho toka kwa Daniel Mwaseba.
"Nyanyuka taratibu na utoke nje ya baa hii, nakuomba twende kirafiki, ujanja wowote ule utakaoufanya inamaanisha unakitafuta kifo chako kwa nguvu!" Tano aliishiwa ujanja, hakuwa na chochote cha kufanya, alikutana na mjanja wa wajanja, alitoka nje taratibu huku akifuatwa kwa nyuma na Daniel Mwaseba kwa umakini mkubwa sana. Safari yao iliishia katika nyumba ya kulala wageni aliyofikia Daniel Mwaseba, pembezoni mwa bahari ya hindi, Kimbilio lodge. Huku njiani wakitembea kama marafiki wa kweli. Watu waliopishana nao njiani bila kuhisi hatari yoyote kati ya watu hawa wawili, laiti wangejua vitu vilivyokuwa vinazunguka katika vichwa vya watu hao wawili. Walipoingia tu ndani ya chumba chake, Daniel Mwaseba alimkaribisha Tano kutoka kundi la Six Killers. "Karibu sana rafiki yangu, haya sasa kwa hiyari yako naomba unambie unaitwa nani?" "Kunileta hapa haimaanishi kwamba mimi ni mateka yako, eti kwamba nitakwambia chochote unachojisikia kuniuliza" kwa mara ya kwanza Tano alijibu huku mdomo wake akiubetua kijeuri kwenda juu.
"Hahaha kumbe nawe jeuri" Daniel Mwaseba alikuwa anacheka huku akimtazama kwa umakini Tano. Ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa, Daniel Mwaseba alirusha teke la haraka lililotua katika goti la Tano, goti lilelile lililojeruhiwa na daktari makini kabisa, Dokta Yusha. Tano alipiga ukelele mkali sana kutokana na maumivu aliyoyapata katika goti, kutokana na pigo lile la teke toka kwa Daniel Mwaseba. "Sipendi kukutesa kijana, naomba unambie kila nitakachokuuliza" Daniel Mwaseba aliongea maneno hayo yakienda sambamba na ngumi mbili nzito zilizompata barabara Tano katika shavu lake la kulia. Ngumi hizo zilileta athari kwa Tano, Damu zilikuwa zinamchuruzika mdomoni. "Utasema husemi?" "Nitasema" Tano alijibu huku akitema rundo la damu. "Safi sana kijana" "Unaitwa nani?" "Tano" "Tano nani?" "Tano wa Six killers" "Sijakuelewa" "Naitwa Tano wa Six killers" "Six killers ndio nini?" Tano alikaa kimya.
Daniel Mwaseba alipatwa na hasira juu ya ukimya wa Tano, alirusha ngumi ya nguvu iliyotua katikati ya mdomo wa Tano, ngumi iliyorudisha jibu, meno mawili ya Tano yalidondoka sakafuni. "Six killers ndio nini?" Daniel aliuliza kwa ukali! Tano aliona hana ujanja, ilimpasa afanye kitu ili aweze kujiokoa katika mdomo wa kifo! Kwa nguvu zake zote Tano alisimama. Ingawa alisikia maumivu makali kwenye goti lakini alisimama. Alirusha teke la nguvu lililomkosa Daniel Mwaseba kidogo sana. Bila wepesi wa Daniel Mwaseba kulikwepa teke lile angepata madhara makubwa sana. Tano aliyebadirika na kuwa kama mzimu alirusha ngumi ya nguvu iliyompata Daniel Mwaseba katika bega la kushoto. Tano alikuwa amechachamaa, alikuwa anataka kufa na mtu.
Daniel nae akajipanga vyema sasa. Tano wa Six Killers alikwenda mzima mzima kumvaa Daniel Mwaseba. Daniel Mwaseba alimuona vizuri sana, alikuwa ameshajipanga vizuri kimapambano, Daniel alisogea pembeni kidogo, Tano alipita moja kwa moja kwa kasi kubwa sana na kwenda kuuvaa ukuta. Ebwana wee! Alijigonga vibaya sana usoni. Dakika hiyohiyo uso wa Tano ulivimba na kutoa kitu kiitwacho nundu katikati ya paji lake la uso! Tano alipata maumivu yasiyo na kifani, alitumia nguvu nyingi sana kwenda kumvaa Daniel Mwaseba. Tano wa six killers hakuweza kustahamili maumivu aliyokuwa anayapata, alianguka chini mzimamzima. Daniel Mwaseba hakumuonea huruma kabisa. Sasa angalau kidogo alishayajua madhara ya Tano. Hakutaka kumpa mwanya wa kufanya chochote. Alimfata kwa teke la nguvu palepale chini alikokuwa amelala.
Teke la kiume lililotua barabara katika kifua cha Tano, Tano alitoa mguno hafifu wa maumivu na kuanza kutoa madonge mazito ya damu mdomoni. "Nakufaa" Tano alisema kwa sauti dhaifu, ama hakika alikuwa amepatikana hasa. Daniel Mwaseba alimjibu, alimjibu kwa teke kali sana la uso. Daniel alikuwa na huruma sana kwa raia wema. Lakini kwa bahati mbaya hakuwa na huruma kabisa kwa wahalifu kama Tano. Uso mzima wa Tano ulitapakaa damu. Tano alijikusanya pale chini, akijitahidi kuvuta pumzi zake za mwisho. Daniel Mwaseba aliinama pale chini alipokuwa amejipweteka Tano, alimshika koromea kwa mkono wake wa kulia.
Tano macho yalimtoka pima!, Daniel Mwaseba alimkaba kiasi kwamba alishindwa hata kumeza mate, ama kumeza damu ambazo ndizo zilikuwepo mdomoni mwake. "Six killers ni nini?" Daniel Mwaseba aliuliza kwa nguvu akiwa anaangaliana na Tano. "Hata nisi-po-kwambia uta-ni-fanya n-ini, mi-mi ni mfu ta-ya-ri, nifa-nye utakacho si-kwa-mbii ki-tu" Daniel Mwaseba akajua yule jamaa amegoma kusema. Alimwacha pale, akasogea kwenye kabati lililokuwa ukutani, akafungua na kutoa mkoba wake. Alitoa kamba za katani, kamba alizotumia kumfunga vizuri sana Tano miguuni na mikononi, hakutaka kumuua, alitaka kujua vitu kwanza toka kwa yule jamaa. Alimwacha kamfunga vizuri Tano na kutoka nje ya kile chumba. Hakwenda mbali sana Daniel, alijibana sehemu akiangalia kitatokea nini pale mlangoni.
Alimwacha kamfunga vizuri Tano na kutoka nje ya kile chumba. Hakwenda mbali sana Daniel, alijibana sehemu akiangalia kitatokea nini pale mlangoni. Kwa jinsi Tano alivyofungwa kamba zile na kwa hali aliyokuwa nayo, mimi na wewe tusingeweza kufungua zile kamba. Lakini Tano wa Six killers hakuwa mimi na wewe. Tano alikuwa nunda kweli. Tano alikuwa mjuaji, Tano alikuwa jambazi mahiri, Tano alikuwa mbabe, Tano alikuwa mtemi. Tano alikuwa sugu! Daniel Mwaseba akiwa amejibanza katika mpenyo katika korido ya nyumba ile ya kulala wageni alishangaa kuuona mlango wa chumba chake ukifunguliwa na mtu kutokea ndani. Tano alikuwa anaenda taratibu kumfata Daniel Mwaseba pale chini alipokuwa amelala.
Ngoma sasa ilikuwa imemgeukia Daniel, tena imemgeukia kwa kasi sana! Tano alikuwa anatisha kama mzimu! Tano alinyanyua guu lake baya la kulia juu, saizi ya kimo cha mbuzi akawa analirudisha kwa kasi kuelekea katika kifua cha mwanaume, Daniel Mwaseba, Tano alikuwa anautumia mguu uleule alioumia vibaya sana gotini. Labda Tano alishikwa na ganzi katika mguu ulipewa jeraha na Dokta Yusha, maana hakusikia kabisa maumivu ya ule mguu wake mbovu. Akiwa amelala pale chini Daniel Mwaseba aliuona vizuri sana mguu ule. Ulivyokuwa unashushwa, kwa kasi ya haraka alinyoosha mikono yake yote miwili na kuudaka mguu ule mbovu,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi