BALAA (17)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI NA SABA ILIPOISHIA... Labda Tano alishikwa na ganzi katika mguu ulipewa jeraha na Dokta Yusha , maana hakusikia kabisa maumivu ya ule mguu wake mbovu. Akiwa amelala pale chini Daniel Mwaseba aliuona vizuri sana mguu ule. Ulivyokuwa unashushwa, kwa kasi ya haraka alinyoosha mikono yake yote miwili na kuudaka mguu ule mbovu, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Daniel Mwaseba aliuzungusha kwa nguvu zake zote. Mguu mbovu wa Tano uliteguka aisee! Tano alianguka chini akigalagala na kulia mithili ya mtoto mdogo. Alikuwa anasikia maumivu yasiyo na mfano. Daniel Mwaseba akiwa na ghadhabu aliruka juu na kushuka chini, aliukanyaga tena mguu mbovu wa Tano palepale kwenye kifuti. Tano alilia kilugha cha kwao.... " Six killers nd'o nini?" Tano alimwangalia Daniel Mwaseba kwa hasira sana. Alijitahidi kukusanya mate ya kutosha mdomoni, ingawa kwa shida lakini a…