Machapisho

BALAA (22)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (22)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI ILIPOISHIA... Hali ilikuwa tete mle ndani kwa upande wa Dokta Kilumba. Vijana wale wawili makini walikuwa wamembana Dokta Kilumba kisawasawa. Mwanasheria mlevi nae alitoka pale mlangoni na kusogea pale walipokuwa Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Siku hiyo Mwanasheria alikuwa hajatia hata tone moja la pombe, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... lakini mwendo wake ulikuwa wa kilevi. Sauti yake ilikuwa ya kilevi. Ama hakika Mwanasheria mlevi alikuwa ameathiriwa sana na pombe, pombe ilikuwa imeweka kambi ya kudumu katika mishipa yake ya damu. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga …