Machapisho

BALAA (25)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (25)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO ILIPOISHIA... Alimshika Mbili shingoni na kumrudisha Mbili ndani kwa nguvu. Sasa mkao ulibadirika....Daniel Mwaseba akakaa ule upande ulikokuwa mlango huku Mbili akiwa kwa ndani. Wote wakiwa wamejipanga tayari kwa mapambano. Mbili alikuwa na silaha ya kisu tu ambayo ilikuwa imetulia kiunoni, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... kisu alichotumia kukata suruali ya Daniel Mwaseba. Daniel alikiona kile kisu pale kiunoni. Lakini hakujari. Sasa Daniel alikuwa anautambua vizuri sana uwezo wa watu wale kimapambano. Sasa aliamua kupiga mapigo ya nguvu! Mapigo hatari wanayofunzwa watu maalum ili kuwapiga watu maalum. Mbili nae alisimama imara....tayari kwa lolote. Daniel nd'o alianza kushambulia, alirusha kareti ya nguvu iliyokuwa inaelekea moja kwa moja katika shingo ya Mbili, lakini mbili aliiona. Kwa kasi ya haraka aliinama kidogo huku akiachia ngumi…