BALAA (27)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (27)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... Daniel Mwaseba alikuwa aneshatambua tayari nia ya Tatu wa Six Killers, labda pengine kabla ya yeye kufikiria kufanya hivyo. Kumbuka siku zote Daniel Mwaseba alikuwa anaendeshwa na hisia, na mara zote hisia zake zilikuwa sahihi, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... hisia za Daniel Mwaseba hazikuwa kuwa hisia za uwongo. Ujio wa Tatu kwa kutumia kichwa Daniel Mwaseba aliutambua. Hakutaka kukwepa kile kichwa, Daniel alikomaza tumbo lake, kichwa cha Tatu wa Six Killers kilienda kukutana na tumbo imara la Daniel Mwaseba. Tumbo lililokuwa tayari kwa mkutano huo. Kama kichwa cha Tatu wa Six killers kilidhani kuwa kimekomaa basi kilikuwa kinajiongopea chenyewe, tumbo la Daniel Mwaseba lilikuwa zaidi yake. Tumbo lilikuwa limekomaa hasa! Au tunaweza sema limekomazwa na mmiliki wa tumbo lile, ambaye ni Daniel Mwaseba. Baada ya zuio la kichwa kile…