BALAA (6)

Zephiline F Ezekiel
Jina: BALAA
Mtunzi: Halfani Sudy

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Alirudia mara nne.Mwanasheria akakata roho akiwa amelewa.

Tano alitoka nje huku akiwa na furaha tele. Bila kujua kama alimuua mtu asiye sahihi. Yeye alimuua Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Ndugu Juma Ngozi. Wakati Mwanasheria aliyeongea na Dokta Yusha, Mwanasheria mlevi alikuwa kilabuni wakati ule, akinywa pombe na kupigizana kelele na kina mama Kindumba

Usiku uleule Tano alirudi Kilwa Kivinje. Kuendelea na kazi yake ya ulinzi pamoja kumuwinda Dr Yusha. Maana usiku wa siku hiyo pia, ilikuwa lazima waipata mioyo kumi na tano katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alifika Kivinje mishale ya saa tano usiku. Na kuikuta kazi ya kutoa mioyo imeshaanza.

Asubuhi mji wa Kilwa Masoko uliamka na taarifa mbaya tena. Taarifa ya kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa, Ndugu Alex Mwasola. Mwasola alikutwa ameuwawa nyumbani kwake. Muuza maziwa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kushuhudia maiti ya Mwasola. Alikuwa na ratiba ya kumpelekea maziwa kila siku. Siku hiyo aligonga sana mlango nje, aliposukuma mlango ulifunguka na alipoingia ndani, alilakiwa na maiti ya bosi wake. Mwili wa Mwanasheria Mwasola, umelala juu ya sofa huku ukiwa umetapakaa damu kifuani. Alirudi nyuma na kuondoka bila kuaga. Hakumsimulia mtu kuhusu tukio lile, muuza maziwa aligeuka bubu.

Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, katika ofisi ya Mwanasheria watu walikuwa wamejaa. Ilikuwa siku ya kazi kwahiyo watu walijaa kufata huduma katika ofisi hiyo, watu wengi walikuwa wamekaa nje ya ofisi hiyo kwa kadri ya saa tano, bila Mwanasheria kutokea. Walijaribu kumpigia simu lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Bahati mbaya Mwasola alikuwa hajaoa na wala hakai na mtu yeyote nyumbani kwake. Ilibidi atumwe mlinzi kwenda kwa Mwanasheria kumwangalia. Ilipo ofisi ya mwanasheria na mtaa wa National hakukuwa mbali sana. Yule mlinzi aliyetumwa kwa Mwanasheria alikutana na balaa.
Picha mbaya kama aliyokutana nayo Muuza maziwa. Mwili wa Mwanasheria ukiwa umelala sofani huku kisu kikiwa kinaning'inia kifuani mwake, na damu zilizoanza kukauka kifuani. Yule mlinzi alishindwa kuvumilia, alipiga makelele, makelele yaliyowajaza kwa kasi majirani.

Walimkuta Mwanasheria ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri. Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Muda mfupi tu habari za kifo cha Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia Mwanasheria mlevi.

Taarifa za kuuwawa kwa Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika ulevi, mama Kindumba.

"Mwanaaa" Mama kindumba aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
"Nambie mama kindumba" Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
"Umesikia wajina wako kauwawa!"
"Nani tena?"
"Mwanasheria"
"Mama kindumba unaumwa nini, Mwanasheria si mimi hapa" "Mwanasheria wa ukweli bana"
"Unaamaanisha Bwana Mwasola?"
"Ndiyo huyo huyo"
"Haaaa!"
"Ndo hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake"
"Aisee, lakini poa bora nibaki Mwanasheria peke yangu"

Mwanasheria mlevi alitia mzaha uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani yake..
"Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake sana"

Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta Yusha ilizua kizaazaa kipya..

Walimkuta Mwanasheria ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri. Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Muda mfupi tu habari za kifo cha Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia Mwanasheria mlevi.

Taarifa za kuuwawa kwa Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika ulevi, mama Kindumba.

"Mwanaaa" Mama kindumba aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
"Nambie mama kindumba" Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
"Umesikia wajina wako kauwawa!"
"Nani tena?"
"Mwanasheria"
"Mama kindumba unaumwa nini, Mwanasheria si mimi hapa" "Mwanasheria wa ukweli bana"
"Unaamaanisha Bwana Mwasola?"
"Ndiyo huyo huyo"
"Haaaa!"
"Ndo hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake"
"Aisee, lakini poa bora nibaki Mwanasheria peke yangu"

Mwanasheria mlevi alitia mzaha uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani yake..
"Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake sana"

Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta Yusha ilizua kizaazaa kipya.

"Hallo Dokta Yusha "
"Nambie Mwanasheria"
"Una taarifa za msiba Dokta"
"Nani tena amefariki Mwanasheria?"
"Mwanasheria Mwasola ameuwawa!
" Acha utani Mwanasheria, Mwasola ameuwawa! "
"Kachomwa kisu Dokta"
"Etiiiii"
"Ndiyo hivyo Dokta"
"Nakuja Masoko sasa hivi, ahsante sana kwa taarifa Mwanasheria"
Simu ikakatwa.

Dokta Yusha aliipokea simu ile akiwa katika benchi la wagonjwa. Lakini mtu wa pembeni yake hakuwa mgonjwa, alikuwa ni Tano wa Six killers, katika harakati zake za kumuwinda Dokta Yusha. Alisikia kila kitu alichoongea Dokta Yusha, huku akishangazwa na taarifa kwamba Mwanasheria kauwawa ilhali Dokta alikuwa anaongea na Mwanasheria.

Dokta Yusha alinyanyuka pale kwenye benchi, akiwa na Lengo la kwenda Kilwa Masoko kwenye msiba. Alipanda gari yake na kuondoka bila ya kujua kama kuna mtu alikuwa anamfata nyuma kwa kutumia pikipiki. Sasa Tano aliamua kuumaliza mchezo, kumuua Dokta Yusha kisha kwenda Kilwa Masoko kumuua huyo Mwanasheria mpya!
Hii inaitwa LIWALO NA LIWE! Tano aliona mchezo unaelekea kubaya, aliamua kuumaliza leo!

Walipofika karibu na kijiji cha Mpara gari la Dokta Yusha lilipata tatizo la kiufundi, lilizima ghafla na kusimama. Ilikuwa bahati mbaya kwa Dokta Yusha..na bahati nzuri sana kwa Tano wa Six killers

Dokta Yusha alisimamisha gari. Na kuanza kulikagua, Tano nae alisimama pale na pikipiki yake.
Hatari ilikuwa inamkaribia Dokta Yusha!

"Vipi tena kaka" Tano aliuliza huku alimsogelea Dokta Yusha.
"Gari linanisumbua kidogo" Dokta alijibu huku akilichungulia gari lake kwa chini, uvunguni.
"Ngoja nikusaidie kidogo"
"Sawa"

Dokta Yusha alifanya kosa, kukaribiana na Tano, tena wakiwa wawili porini lilikuwa ni kosa kubwa sana. Tano hakuelekea kwenye gari, Tano alimfata Dokta Yusha pale chini. Dokta Yusha alimtazama yule jamaa na kuingiwa na woga kidogo, alishangaa jinsi ya yule dereva pikipiki alivyokuwa anamfata kwa kasi, tena kishari!
Dokta Yusha nae alisimama, alijipanga kwa shari yoyote.

Tano alitoa kitu kwenye mfuko wa ndani wa koti, ilikuwa bastola!
Sasa Dokta Yusha hakuwa na mshangao tena, alikuwa makini. Kitu ambacha Tano alikuwa hajui, Dokta Yusha alikuwa amepitia mafunzo ya uaskari kabla ya kuwa dokta, mafunzo ya uaskari magereza huko Kiwira, Mbeya. Na kufanya kazi kama askari magereza mkoani Mtwara. Dokta Yusha hakuwa mgeni kuitumia bunduki, hakuwa mgeni wa kutazamana na bastola. Ndio maana bastola aliyooneshwa na Tano haikumtisha kabisa, zaidi ilimuongezea umakini.

Tano yeye alimchukulia Dokta Yusha kama raia wa kawaida, raia ambaye atatetemeka baada ya kuoneshwa bastola, au labda atajikojolea baada ya kuona bastola ikimuelekea usoni mwake.
Lakini haikuwa hivyo kwa Dokta Yusha!

Tano na Dokta Yusha walikaribiana sana, Tano alifanya kosa la kiufundi, alimkaribia sana Dokta Yusha na ukaribu ule ulizua jambo!

Dokta Yusha alirudisha nyuma mguu wake wa kulia, na kuuleta mbele kwa kasi na nguvu kubwa sana!
Mtindo wa kuupeleka mguu namna ile huitwa teke!
Teke lile la Dokta Yusha lilifika ulipokuwa mkono wa Tano ambao ulikuwa umeshika bastola, bastola ilisukumwa kwa kasi na kujisweka pembeni ya barabara. Sasa Dokta Yusha na Tano walibaki mikono mitupu, wakitazamana kama majogoo.

Tano alitabasamu, alifurahi sana na ujanja aliouonesha Dokta Yusha, alimuona kama amejipalia mkaa wa moto, Tano alijiweka vizuri kimapambano!

Dokta Yusha naye hakutetereka, hakutetemeka, alimwangalia jinsi Tano alivyosimama na kupanga ngumi, yeye alikuwa amesimama tu kawaida.
Tano alimfata Dokta Yusha kwa kasi kwa teke lilikuwa linaelekea tumboni kwa Dokta Yusha, kwa kasi ya ajabu Dokta Yusha alijisogeza pembeni kidogo, kukwepa lile teke. Tano akapita kwa kasi na lile teke lake hadi pembeni mwa barabara kwenye nyasi fupi. Tano alisimama tena huku akiwa amefura kwa hasira, kukwepa vile na Dokta Yusha ilikuwa ni dharau kubwa sana kwake, akajipanga tena upya, kwa bahati mbaya alikuwa anaongozwa na hasira. Ni kosa kubwa sana katika mapambano kuongozwa na hasira.

Dokta Yusha alicheka kwa sauti kubwa kwa dharau, alicheka kwa lengo la kuzidi kumtoa Tano wa Six killers mchezoni, na kweli kicheko kile kilipokelewa tofauti kabisa na Tano muuaji, kicheko kiliibadirisha ile hasira ya Tano na kuigeuza kuwa jazba!
Dokta Yusha alifanya vile makusudi, kwa jinsi alivyomuona amesimama Tano na jinsi alivyopanga ngumi, alijua Tano siyo wa kiwango chake. Tano alikuwa mahiri zaidi yake. Sasa alikuwa anatumia mbinu ya kumpandisha hasira Tano ili apoteze umakini, huku yeye akifikiria namna ya kujiokoa na alifanikiwa tena kwa hilo!

Tano alifura kwa hasira na jazba ya hali ya juu. Moyoni mwake kulikuwa kunafukuta!

Alirusha ngumi kwa mkono wake wa kulia, ngumi ya nguvu iliyorushwa na mtu mwenye nguvu, Dokta Yusha alijaribu kuikwepa, lakini hakufanikiwa kuikwepa yote, mkwaruzo wa ngumi ile ulimpata kidogo katika sehemu ndogo ya mbavu ya kushoto, alisikia maumivu kidogo, lakini hakutaka kuonesha kama alisikia maumivu, Tano hakusubiri, ngumi ya kushoto sasa ilikuwa inaelekea katika mwamba wa pua wa Dokta Yusha, kwa kasi na umakini Dokta Yusha alifanya mambo mawili ya kustaajabisha sana…

Dokta Yusha, aliikwepa ile ngumi, huku nae akipiga ngumi yake kwa nguvu iliyotua barabara katika mbavu za Tano!
Tano hakuamini kasi aliyoitumia Dokta Yusha kukwepa ngumi ile, pia hakuamini uzito wa ngumi wa Dokta Yusha, sasa tano akajua anapambana na mtu anayejua anachokifanya. Hakujiuliza tena, sasa aliamua kupiga mapigo ya kifo,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni