BALAA (7)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Dokta Yusha , aliikwepa ile ngumi, huku nae akipiga ngumi yake kwa nguvu iliyotua barabara katika mbavu za Tano ! Tano hakuamini kasi aliyoitumia Dokta Yusha kukwepa ngumi ile, pia hakuamini uzito wa ngumi wa Dokta Yusha, sasa tano akajua anapambana na mtu anayejua anachokifanya. Hakujiuliza tena, sasa aliamua kupiga mapigo ya kifo, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... mapigo ambayo yakimgusa mpigwaji yanaondoka na roho yake….Balaa! Tano alianza na teke lilikwenda kwa kasi kama umeme, teke liliombatana na uzito wa kilo kadhaa. Dokta Yusha aliliona teke lile, teke liliolekezwa shingoni kwa lengo ya kuondoka na shingo yake, aliinama kidogo, teke likapita, ila upepo wa teke lile ulimyumbisha Dokta Yusha na kumdondosha chini, akiwa amelala pale chali, tano aliruka juu na kushuka chini huku akiwa amekitanguliza kifuti cha mguu wake wa kushoto, kifuto kil…