HATI FEKI (1)

Zephiline F Ezekiel
HATI FEKI (1)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA KWANZA JOHN AMIGOLAS YUKO MAHABUSU BAADA YA KUKUTWA AKIWA NA MWILI WA MFANYABIASHARA MAARUFU, GULAM , MARA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI AMBAO WALIMVAMIA NA KUCHUKUA PESA ZAKE ZOTE NA KUKIMBIA NAZO HUKU WAKIMPIGA RISASI NA KUMUUA. JOHN ANASHIKILIWA NA POLISI. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... ASUBUHI ya siku hiyo John alikuwa amesimama peke yake.nywele zikiwa timtim huku amepauka baada ya muda mrefu wa kutokuoga na mgomo wa kutokujishughulisha na chochote hadi atakapopata hatma ya jambo lililomleta hapo. Mawazo yalikuwa yakimwandama baada ya usingizi wa mang’amung’amu ambao alikuwa hajauzoea. Hakuna aliyejali. Labda kwa kuwa hawakupewa taarifa juu. Juu ya hali aliyonayo. Hakuna aliyejua ni nini kilichomkumba. Alipiga ndoo teke. Ndoo iliyokuwepo karibu na sehemu aliyokuwa amelala. Sababu za yeye kuwepo hapo pamoja na ndoo havikumwingia akilini. Alivu…