HATI FEKI (2)

Zephiline F Ezekiel
HATI FEKI (2)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Hakuna taarifa za kukamatwa kwa wahusika japo polisi walikuwa wakiendelea na uchunguzi. Alitaka kumuuliza John kaka yake kama alikuwa akijua lolote linaloendelea kuhusiana na vifo hivyo. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Hakujua wazo alilokuwa nalo John kwani alihisi John lazma atakuwa na la kufanya na yeye angetoa ushirikiano. “Kaka, unampango gani baada ya haya yote,” Antony alimuuliza John siku mbili baada ya kumaliza mazishi. “Dah, bado…ila nawasubiri hao polisi wakamilishe uchunguzi wao. Wakati huo John alikuwa akifikiria namna ya kumpata Aminata. John na Antony walianza kufatilia mali za baba yao ili wazirithi. Walizunguka kote na kuongea na watu waliokuwa wameachiwa na kujua maendeleo ya biashara hizo. Walifanikiwa kwenye mali nyingi isipokuwa mgodi wa baba yao . Utata ukaanza kugubika kwenye suala la umiliki. Baada ya kifo cha baba …