
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Aminata alitaka kujaribu bahati yake kwa kumuuliza mengi kuhusiana na kundi lao. Kwa kipindi kifupi cha kujuana na Dula aliweza kuonana na wengi katika kikundi hicho akiwemo Mosses ambaye baada ya Dula kumtambulisha alionekana kumtamani sana Aminata.
“Unakaribisha sana shemeji. Wakati wowote.”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Alisema Mosses kisha kutoka baada ya kumsalimia Aminata.
Aminata alimwangalia sana. Mosses alikuwa ni mrefu mweupe. Sura yake ilikuwa ikifanana na chotara wa Kiarabu. Ni Mnyamwezi wa Tabora lakini maisha yake alikulia Arusha. Alifanikiwa kusoma hadi kidato cha sita. Ni biashara za magendo ndizo zilizomfanya Mosses asiendelee na chuo kwa ni alifaulu vizuri lakini pesa ilimfanya asitamani tena kusoma. Na huo ndio ukawa mwisho wa kurejea yaliyo vitabuni.
Alianzisha kampuni ya magendo ambayo haikusajiliwa ya kununua magari na kuyauza. Baada ya miaka sita iligundulika lakini hawakuweza kumkamata kwani alikimbilia nchini Kenya na kuishi kwa miaka miwili. Baadaye Mosses alirudi na kuanza ujambazi. Ngome yake aliiweka katika msitu mmoja wa Kambi ya Fisi. Huko hakuweza kuonwa na yeyote kwani alijiimarisha kwa kuweka uzio na walinzi wa kutosha. Alianza kufanya ujambazi na utekaji wa magari akishirikiana na watu wake.
*****
Aminata alifanikiwa kujua juu ya Mosses. Sasa roho yake ilitulia. Hakujali kuhusiana na kifo cha Dula ambaye baada ya kubainika ametoa siri za kundi.. Mosses alimpiga risasi na kufa. Aminata baada ya kusikia habari hizo aliamua kujificha kwa muda.
Alikimbilia jijini Dar es Salaam ambako aliamua kusomea masuala ya Upelelezi na jeshi. Alijua Dula hakumdanganya baada ya kumweluezea ukweli ya siku walivyoteka gari la mzee Peter na familia yake na kuwaua kisha kuchukua mali.
Aminata alitumia mbinu kubwa sana kumshawishi Dula ili amwelezee. Ni pale alipoamua kumvulia nguo akimaanisha kwamba ni wapenzi. Hapo sasa Dula alidiriki kuunyanyua mdomo wake na kumwambia Aminata kila kitu.
Usiku huo Dula alijua ungekuwa mrahisi sana. Baada ya kumwambia Aminata juu ya siri za kundi lake. Aminata alimtamkia Dula kuwa anampenda sana na kumwahidi kuwa wake. Dula alifurahi sana. Alimkumbatia Aminata kwa nguvu na kumbusu. Hapo ilikuwa ni kazi rahisi. Dula alijiandikia ushindi kwa mtoto mzuri Aminata.
“Mbona sikuelewi tena Aminata,” Dula alihoji baada ya kumwona Aminata akitoka kitandani na kukaa kitako katika moja ya masofa yaliyokuwa katika chumba cha hoteli waliyofikia.
“Hapana Dula, usijali. Siko tayari leo. Nimeumwa sana leo.”
“Kwa hiyo tutalala tu hivi hivi?”
“Siyo hivyo. Ni kwa leo tu. Wewe ni mpenzi wangu. Siku yoyote utanitumia uwezavyo.”
Dula alikubali kwa shingo upande na kulala.
*****
Aminata alifanikiwa kumaliza mafunzo yake ya upelelezi. Alirudi Arusha na kujiunga moja kwa moja na Jeshi la Polisi. Ni ujanja wake na uchapaji kazi wake ndio ulipelekea kutunikiwa cheo cha Ofisa Upelelezi. Ilikuwa ni furaha kwake.
Kati ya mambo ambayo aliyafanya ni uchunguzi na kugundua biashara ya dawa za kulevya iliyomhusisha kigogo mmoja mkubwa serikalini.
Ni katika mpaka wa Tanzania na Kenya. Eneo liitwalo Namanga ndipo tukio hilo lilipotokea. Akiwa kati ya maafisa wapelelezi wadogo na walioibukia katika kazi hiyo. Aminata aliiamrisha kushushkwa moja ya mabegi ambalo ndani lilikuwa limesheheni nguo.
Aliliangalia lile begi na hasa baada ya ofisa mmoja mkaguzi kuliwekea alama kumaanisha kwamba lilikuwa safi na kwamba hakukuwa na chochote kibaya. Ofisa huyo alizima alamu ya mashine ya kukagulia na kuipitisha juu ya begi hilo. Baada ya kumaliza aliiwasha. Aminata alikuwa ameona tukio hilo.
“Nasema shusha tena hilo begi. Sijaridhika na ukaguzi wake.” ofisa yule aliogopa kidogo na kumjia juu Aminata.
“Nimelikagua, halina shida. Haya mzigo mwingine.” yule ofisa aliamrisha baada ya lile begi kupakiwa kwenye gari.
“Nimesema, fungua begi,” Aminata alitoa tena amri ambayo safari hii yule ofisa aliitii na kufungua begi. Aminata alitumia kifaa maalumu na kugundua ndani ya lile begi kulikuwa na dawa za kulevya.
Haraka alichukua simu yake ya upepo na kuwasiliana na polisi ambao walifika maramoja na kuwachukua wale wahusika ambao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali.
Walipelekwa Kituo cha Polisi cha Kati cha mjini Arusha kwa ajili ya mahojiano huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na biashara hiyo. Watuhumiwa baada ya uchunguzi walifikishwa mahakamani akiwemo kigogo wa serikalini ambaye ndiye aliyewatumia watuhumiwa wenzake kuziingiza dawa hizo zilizotokea nje ya nchi.
Wakati wa sherehe moja kubwa ambayo iliwahusu maofisa wapelelezi. Aminata alipata bahati ya kupandishwa cheo na kuwa Ofisa mkuu. Baadaye alihamishiwa jijini Dar es Salaam. Alishindwa kupinga kwani mkuu wa polisi alitaka iwe hivyo. Aminata alihamia Dar es Salaam.
Huko Dar es Salaam, palikuwa hapakaliki. Mara nyingi alirudi Arusha kwa ajili ya kazi yake moja tu. Kazi ya kuuangamiza mtandao wa Mosses Ndula. Ulikuwa ni mtafutano baina yake na Mosses Ndula ambaye alidhamiria kumweka Aminata mikononi mwake.
*****
John alikuwa hana raha. Alimfikiria sana wakati huo. Alikumbuka kwamba hakumwachia namba za simu Aminata bali alimwambia tu amtafute baada ya mazishi ya ndugu zake.
Alifikiria sana atampataje na mwisho aliamua arudi kituo cha polisi kwani mara ya kwanza kufika kituoni hapo alikuwa amefungwa pingu huku Aminata akiwa ni moja ya watu waliompeleka kituoni hapo kutokana na kesi yake kuwa kubwa japo iligundulika kuwa si yeye aliyemuua mfanyabiashara anayedaiwa kuuliwa. Aliingia na kumkuta Afande Nicco na kumsalimia.
“Habari yako afande.”
“Ahh! We mwalifu, umerudi tena, umejileta eeh?” Afande Nicco aliongea kwa mzaha uliosababisha John acheke.
“Karibu tena, leo umekuja kumshtaki mtu au kunisalimia tu?” Aliendelea na utani afande Nicco.
"Hapana nimekuja kukusalimia na kuulizia jambo moja. Kuna dada mmoja alikuwa pamoja na Afande Mushi waliponileta siku ya kwanza. Anaitwa Aminata.”
"Aminata, we unataka kutembea na ofisa upelelezi?” Alisema Afande Nicco kwa mshangao na kauli zake za utani. John alicheka kidogo.
"Hapana, kuna jambo anataka nizungumze naye, aliniambia nimtafute."
“Kwani huna namba zake za simu?”
“Hapana, hakunipa siku hiyo. Kama unayo naomba unisaidie.”
"Sawa mi n’takupa namba zake za simu na kwa nini hakukuachia namba zake?" Alihoji Afande Nicco.
"Sielewi, ila alisema tu nimtafute." Afande Nicco alimpa John namba za simu kisha waliagana. John aliwasha gari lake na kuelekea nyumbani. Alichukua zile namba na kumpigia Aminata.
"Haloo!"
"Habari yako, sijui nani mwenzangu?" Sauti ya upande wa pili ilikuwa ni ya Aminata ambaye alitaka kujua ni nani aliyempigia simu.
"John, mtoto wa Amigolas, marehemu sasa, tulikutana Hospitali ya Mount Meru na kunitaka n’kutafute baada ya mazishi ya ndugu zangu."
"Ooh! John, pole sana. Ila umechelewa sana kunitafuta. Mimi nipo hapa McDonald's Pub kama utaweza kufika hapa muda huu itakuwa vizuri zaidi." Aminata aliongea kwa furaha baada ya kujua aliyempigia simu ni John.
"Nakuja hapo sasa hivi Aminata."
"Sawa nakusubiri John.”
Aminata alikumbuka dhamira yake. alijua akiwa na John mpango wake utafanikiwa kwa asilimia mia moja. Alijua pigo alilolipata yeye ni sawa na alilolipata John na hivyo ingekuwa rahisi sana kufanya kazi pamoja.
Alikuwa tayari ameshaijua vyema familia yote ya mzee Amigolas. Aliijua baada ya kutaka kuwa katika upelelezi wa wauaji wa familia hiyo.
Japokuwa alishafahamu mtandao mzima lakini Aminata hakudiriki kuwaeleza polisi juu ya mtandao huo kwani lengo lake lilikuwa ni moja tu. Kulisambaratisha.
******
John aliwasha gari lake . Askari wa mlangoni aliwahi kufungua geti na John kuondoa gari kwa kasi ili amuwahi Aminata. Ilimchukua dakika 10 mpaka kufika McDonald's Pub. Alikuta magari mengi nje. Alilipaki gari lake karibu na mlango wa kuingilia ndani. Aliteremka na kutoa simu yake na kumpigia Aminata.
"Haloo Aminata."
"John, njoo moja kwa moja hadi counter, nipo peke yangu hapa."
"Sawa Aminata, nakuja hapo sasa hivi," John alielekea hadi counter na kumkuta Aminata akiwa ameshikilia glasi ya wine. Mhudumu alipomwona John alimkaribisha.
“Karibu kaka, n’kusaidie nini?”
"Hapana sitatumia chochote.”
“John, you should take something... mhudumu, mletee wine kama yangu,” Aminata alimwagizia John wine. Walikaa na kuanza kuongea baada ya wine kuletwa.
“John,” aliita Aminata.
“Yes Aminata, nakusikiliza.”
“Pole sana na msiba wa wazazi wako na ndugu zako. Nauhakika polisi bado wanaendelea na uchunguzi. Mimi ni ofisa upelelezi ndiyo maana uliniona siku ambayo ulikamatwa niliongozana pamoja na Inspekta Morris na Afande Mushi.
Wote kwa sasa wanafanya uchunguzi wa nani anahusika na vifo vya wazazi wako na ndugu zako.”
“Natamani sana kuwajua watu hao,” alisema John huku kainamisha kichwa chini na kusababisha huruma kwa Aminata.
“Utawajua John, kabla hawajakamatwa, mimi na wewe tutawakamata."
“Tutawakamata vipi lakini?” Alihoji John kwa mshangao kwani hakuwa na uzoefu wa kukamata wahalifu. Iweje apewe jukumu hilo.
“Mi siyo polisi, n’tawezaje Aminata.”
“Namaanisha, nataka ulipe kisasi na si kuwakamata. Kama walivyoua ndugu zako, yapasa na wao waangamizwe. We ni mwanamume. Amka. Wale wakikamatwa na polisi baadaye watatoka. Inatakiwa wamalizwe kabisa.”
“Kumbe unawajua Aminata?” Alihoji John.
“Ndiyo John, ni mtandao mkubwa sana wa kihalifu, unaoogopeka sana. Kiongozi wao anaitwa Mosses Ndula, huwa hakai hapa nchini, anakuja bila yeyote kujua nakuondoka. Na huyo ndiye jabali lao. Ndiye aliyewatuma watu wake wawaue wazazi na ndugu zako. Inawezekana pia wakawa wanawatafuta na nyie wawili.”
“Sisi wawili, mi na nani?”
“Unamfahamu pacha wangu, unamfahamu Antony?”
"Ndiyo John, kwenu nawafahamu japo nyie hamnifahamu. N’mefanya kazi nyingi sana kumsaidia baba yako. Na hiyo ilinifanya niwajue..... Nadhani ni muda wa kwenda. Nitakuelezea mengi tukifika kwangu."
"Naomba tuongozane, twende pamoja nyumbani kwetu ukapafahamu," John alimwambia Aminata ili waongozane kwenda kwao.
"Sawa John," Aminata alikubali na kuongozana na John. Hakutumia usafiri wake. Aliliacha na kuondoka pamoja na John aliyekuwa na usafiri wake.
*****
Walitumia dakika ishirini tu kufika Njiro nyumbani kwa kina John. Walikuta watu watatu wakiwa wamesimama nje ya geti. Mlinzi aliwafungulia na kuingia. John alikuwa bado hajawatambua hadi alipofikia geti kabisa. Mlinzi alifungua geti kubwa na kuliruhusu gari la John kuingia.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi