HATI FEKI (6)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... John na Aminata waliamua kuendelea kuwafatilia wale watu wa Mosses. “John, tuwawahi kabla hawajatuwahi, kwa sasa hawajui tulipo. Tumeanza na hao watatu. Tuhakikishe tunawamaliza wote,” Aminata alisema baada ya kuona mambo yamekwisha tulia. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Itabidi tusilale kwenye hii nyumba Aminata wala kwako tusiende, huenda wameshajua niko na wewe,” John alimsihi Aminata wasiendelee kuishi hapo badala yake wahamie hata hotelini ili wafanikishe kwanza mipango yao kisha watarudi. Walifunga nyumba na kisha kuondoka jioni na kwenda hotelini kuishi huko, waliamua wawe wanabadili hoteli mara kwa mara ili wasijulikane wako hoteli gani. Huko walikua wakifika usiku tu. Mchana kutwa walishinda barabarani wakiangalia baadhi ya watu wa Mosses ili kuwamaliza. Waliangalia pia njia ambayo wataitumia kuvamia ngome yao iliyokuwa kambi …