MWAJUMA UTAMU (2)

Zephiline F Ezekiel
MWAJUMA UTAMU (2)
Jina: MWAJUMA UTAMU Mtunzi: Juma Hiza SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... "Amefanyaje?" aliniuliza Daniel kisha nikaanza kumsimulia kila kitu. Nilipomaliza kumsimulia nikamuona akivuta pumzi ndefu na kuziachia kwa pupa, kama ilivyokuwa kwa Baba yake na yeye pia hakutaka kuamini, kitendo cha kuwachanganya kimapenzi na Baba yake kilimuumiza mno. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Nilishangazwa na maamuzi aliyoyachukua Daniel, hakutaka kuendelea kuushuhudia uchafu kama huo ukiendelea mbele yake, alichoamua kukifanya ni kuniambia kuwa siku hiyo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa mapenzi yetu, hakutaka kusikia nikimuita mpenzi tena. Niliumia sana baada ya Daniel kuchukua maamuzi hayo, mtu ambaye niliamini ndiye angeweza kuwa msaada wangu kwa wakati huo hakutaka kunisikia hata mara moja. Maisha yalibadilika ndani ya nyumba, kila siku nilikuwa ni mtu wa kumuomba Mungu aninusuru na mabaya ambayo yangeweza kunito…