KONSTEBO NGUZU (10)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Kisha akatengeneza vamizi la kumrejesha Juma nyumbani bila maafa yoyote, ili aendelee kuwasoma watu wanaomfuatilia Juma. Akaivamia nyumba na kutoa kitisho kikali. Zoezi likafanikiwa Juma amerejea na wao wamerejea. Ni akina nani hawa? na wanataka nini kwa Juma? JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... haya yalikuwa maswali ambayo yalihitaji kupatiwa majibu upesi sana kabla naye hajajua ni kitu gani anaweza kufanya katika mchakato huu. Aliitoa taarifa hii ya mashaka yake juu ya watu anaowaona eneo hilo, taarifa ikapokelewa huku akisisitizwa kuwa makini zaidi. Masaa yalizidi kwenda bila kuona juhudi za watu wale kuingia ndani ya nyumba ya Juma, walibaki kurandaranda huku na kule bila kujua kuwa wanafuatiliwa. Kwa kuwatazama jinsi walivyokuwa wanatembea na kufanya mawasiliano alihisi yawezekana ni askari waliopo kazini, ama waliopoteza kazi za…