KONSTEBO NGUZU (11)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Hata tukio la kukuta pesa katika nguo aliyoianua katika kamba usiku ule baada ya kujinasua katika kifusi katika nyumba iliyokuwa imeanguka bado kilimtatanisha. "Nani wa kusahau pesa katika nguo ndani ya jiji la Dar es salaam !!" JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... alijisemea na kujikuta akitokwa na tabasamu kubwa sana kulikumbuka jiji lile na vituko vyake. "Mzee Majenga kuna kitu anapaswa kunieleza, sidhani kama nipo kawaida." aliweka hitimisho lile. Wakati anarejea katika chumba chake akaanza kumuwaza tena mama yake mzazi. Nini kinatokea? alijiuliza huku hofu ikianza kumwingia. Hakutaka kupuuzia hii hisia iliyomjia ghafla, akajiahidi kuwa siku inayofuata atalazimika kurejea jijini Mwanza . Akarejea katika kile chumba chenye kunguni wapenda sifa. Akajilaza na kusinzia. Alfajiri ilimkuta barabarani, akadandia g…