
Mtunzi: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Akamalizia na tusi lake la kiitaliano. Lakini kwa mara ya kwanza akajikuta akilitoa tusi hilo kinyonge sana.
Inspekta Kobo akagundua kuwa alikuwa yu na uoga wa ajabu mno,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
uoga ambao hajawahi kuwa nao hapo kabla.
Ni hapa alipokiri kuwa yumkini damu nzito kuliko maji lakini penzi ni zito kuliko vyote, maji na damu ukivichanganya pamoja.
Inspekta akakiri kuwa katika mapambano ya zamani hakuwa muoga kwa sababu aliingia katika mapigano huku katikati ya uwanja wa mapambano pakiwa hakuna ndugu yake wala mtu anayempenda, hivyo hata akifa mtu kwake haikuwa tatizo.
Sasa anawatukana watu walioshika hatamu ya maisha ya mkewe kipenzi.
Inspekta akatubu kimyakimya.
Wakati anakiri kuwa anawaogopa watekaji, simu yake ikaita.
Nambari ilikuwa ngeni, akajua wazi kuwa huyo atakuwa ni mtekaji na sasa anataka kutoa masharti ili mkewe apatikane huku akiwa hai ama akaidi na kupokea kichwa cha mkewe kikiwa kimelowa damu mbichi na ujumbe wa kukera 'tengeneza supu unywe kama kweli ulikuwa unampenda'
Inspekta akaipokea simu ile kwa upole kabisa.
"Inspekta Kobo!" sauti kutoka upande wa pili ikamuita. Akaitikia 'rabeka'
"Samahani kwa usumbufu mkuu, lakini mimi ni daktari hapa Muhimbili. Sijui kama una taarifa zozote kuhusu mke wako. Daktari Anna Kobo."
Sijakuelewa taarifa kuhusu nini?" aliuliza kwa upole vilevile huku akiketi chini.
"Yupo hospitali hapa, naona amepatwa na hitilafu kidogo ila kila kitu kipo sawa. Itafaa ukifika huku." Taarifa iliishia pale.
Inspekta alitamani kuuliza maswali mengi lakini hakuna hata moja lililotoka hadi simu inakatika.
Jasho lilikuwa limeulowanisha mgongo, uso, kwapa na kifua.
Inspekta alikuwa ameoga jasho huku amekaa tu bila kukimbia.
Jasho lile likamfadhaisha mno, aakaanza kujipepea na gazeti lililokuwa mbele yake.
Bado halin hii ilimbughudhi, akajikaza kikakamavu na kusimama akaukaza mwili wake kisha akajikumbusha kanuni za kijasiri za jeshini.
Alipomaliza akabiga saluti, kisha akajiwekea kiapo kuwa hatatumia tena muda mwingi kutetemeka, kutokwa jasho na kunung'unika badala yake atautumia muda mwingi kutafuta majibu ya maswali yanayokielemea kichwa chake.
Akaipapasa bastola yake na kisha akasemanayo. Kana kwamba inamsikia.
"Unaonaje kama nikizitoa hizi risasi kwenye chemba kisha ziwe eneo husika tayari tayari kwa kupasua kichwa cha mtu atakayethubutu kunishambulia. Maana si unajua hawa wapinzani wangu wananijua nami siwajui..... sema nawe unazingua ungekuwa na macho tungesaidiana. MI naangalia kulia we kushoto...." Alizungumza huku akiziweka risasi katika njia yake. Watoto waliozoea kutazama picha za mapigano wanasema 'akaukoji mjegeja wake'.
Safari ya kuelekea hospitali kupokea taarifa mbaya kabisa kuwa mkewe alikuwa hai lakini alikuwa amezikosa fahamu zake. Kwa lugha ya kigeni 'alikuwa katika coma'.
Ni heri angekuwa amepoteza fahamu, dokta Kobo hakuwa kabisa na fahamu zake.
Na haikujulikana zitarejea lini.
Inspekta alichoka!
Alijikaza chozi lisimtoke, hakuweza.
Yalibubujika kama mtoto mdogo.
Akatoweka hospitali na kwenda kumalizia kilio chake katika kitanda alicholala Zubeda kule kwenye eneo la siri aliloamua kumuhifadhi.
Kwa wakati huo hakujali jambo jingine zaidi ya watu wake wa karibu wanaoingia matatani kwa sababu yake.
Hasira zake akazihamishia kwa Juma Kihwele.
Kumbukumbu za jina lile zikasababisha sharubu zake kusisimka. Akaendelea kuhisi kuwa huyu bwana ndiye aliyeandika zile habari, na kama aliziandika basi kuna mawili. Anasakwa na waliompa tenda hiyo chafu ili wammalize asije kutoa siri, ama la yupo mikononi mwa watu wabaya tayari kwa kuuwawa.
"Zuu, hivi bi mkubwa hakukueleza ni nani aliyempa maneno yale mazito?" Inspekta alimuuliza koplo Zubeda kwa upole kabisa.
"Hapana hakutaja jina lolote wala hakuelekea kufanya hivyo. Alikuwa anajua anachokifanya wakati anazungumza na mimi." Alijibu kwa kirefu huku akiwa ameketi.
Hali yake kiafya ilikuwa inaridhisha.
"Vipi kuna kitu kipya unahisi?" Zubeda akajazia swali.
Kimya kikatanda kabla inspekta hajaelezea hisia zake juu ya mwandishi wa habari aitwaye Juma Kihwele. Ili kuusadikisha ukweli akazimwaga hadharani sifa za kimbelembele alizonazo muhariri huyo.
Sifa zile zikamfanya Zubeda amuunge mkono inspekta katika hisia zake zile.
"Nilimsikia daktari akizungumzia juu ya risasi kushambulia nyumba ya Kihwele, usiku uliopita nadhani."
"Risasi? nani na nani walikuwa wanarusha?" Swali la kipuuzi likamponyoka. Akawa mnyonge alipogundua kuwa ameuliza kipuuzi.
Hakurekebisha!
Akatwaa simu yake na kupiga kwa rafiki yake wa kitengo cha mawasiliano.
Akamuuliza nini kimejiri.
Taarifa zikatoka kuwa inasadikika kuwa familia ya Juma Kihwele yaani mke na mtoto pamoja na ndugu mmoja ilikuwa imepotea.
Nguo zilizotapakaa damu zimeonekana na hazijulikani kama ni majeraha ama zinamaanisha vibaya kwa wahanga.
Hadi wakati huo hakuna anayehusishwa na tukio hilo moja kwa moja.
Taarifa ile iliyakaanga maini ya inspekta Kobo, uzuri sauti ilikuwa yasikika vyema hivyo hata Zubeda alisikia kila kitu.
"Zuu mpenzi wangu, huu mkasa utanizeesha upya. Nilijidanganya mkasa huu utanichangamsha na kuwa kijana..... ajabu nazeeka tena kwa kasi mno. Sijui kuwaza vizuri, sijui kujikaza, yaani nimekuwa kama fala hivi aliyevuta sigara bwege halafu hana uhakika wa chakula cha mchana wala usiku.
Badala ya kulia kiume nalia kama mwanamke.
Looh! mkasa huu unanibadili hadi jinsia mimi inspekta Kobo." Alilalama kwa uchungu mno huku akijitahidi chozi lisimdondoke.
Zubeda akafanya kosa kumbembeleza, Inspekta akaanza kulia kama mtoto.
"Wameanza na wewe wamekusababishia ajali, wamemzimisha mke wangu huko, na bado wanaendelea kuniumiza kichwa.....aah! Si wanikamate na waseme nini wanataka eeh! Kwani mimi ni mwanadamu wa kwanza kumsaliti mke wangu eeh! Mimi ni wa kwanza nauliza, mbona wameniandama hivi mimi lakini."
Kwa kilio hiki Zubeda alikiri kuwa inspekta alikuwa amekamatwa pabaya.
Wakati kilio hiki kikiendelea simu yake ya mkononi ikatoa mwanga.
"Angalia ni nani anapiga, kama ni namba mpya naomba usipokee. Sitaki kufia humu ndani, waniache nikafie ndani ya nyumba yangu." Alizungumza kwa hisia za malalamiko.
"Anapiga Komredi Kitengo." Zubeda akamtajia jina linaloonekana pale.
Inspekta akaipokea simu huku akiilazimisha sauti yake iwe ya kawaida tena.
"Halafu komredi, si uliniambia kuwa unapenda sana samaki aina ya Sato na Sangara wa Mwanza?" Mpigaji aliuliza lile swali.
Inspekta mdomo ukamfunguka asiamini aliyepiga simu ile alikusudia kumsumbua kwa swali la kizembe namna ile.
Zubeda yeye alijikuta anatabasamu.
"Mbona kimya komredi ama pweza wa jiji washakuvuruga hutaki tena sato." aliendelea.
"Komredi... najisikia usingizi mkuu. Niache nilale..." alijitahidi sana kulinda heshima iliyopo kati yao.
"Hivi Sato hata Shinyanga wapo au ni Mwanza tu?" Mpiga simu hakujali zile busara.
Inspekta akatamani kulitoa lile tusi lake la akiba lililo katika lugha ya kiitaliano lakini huyu mpiga simu licha ya kuwa na utani waliheshimiana sana.
Akabaki kujichekesha tu..
"Haya jiandae kwenda kula sato, hakikisha unaniletea walau mapande matatu yaliyokaushwa na mimi nijue utamu wa sato wa Mwanza."
"Una maana gani komredi?" Akauliza inspekta.
"Ndani ya siku mbili hadi tatu mtapelekwa Shinyanga nyie mnaojifanya mnajua sana kutumia bunduki na kulenga shabaha. Kuna kazi inawaita huko, nimekuibia siri tu ili usije ukasema sikukuagiza mapema sato." Alizungumza kwa utulivu kwa kuamini taarifa ile itakuwa njema kwa inspekta Kobo ambaye alikuwa mpenzi wa mapambano enzi zake.
"Komredi lakini mimi nimezeeka tayari na nimevunjika mguu mnajua... mbona.." Akataka kuendelea kulaumu akasita kwa kugundua kuwa analalamika sehemu isiyokuwa sahihi hata chembe.
"Sio wewe pekee kuna wenzako pia wamestaafu lakini umaridadi wao katika mapambano unawarudisha kazini."
Mazungumzo yalimalizika na kumwacha inspekta akiwa katika mtihani mwingine mzito.
Mkewe yu katika 'coma' hawara yake anajiuguza bado na sasa anatakiwa kwenda Shinyanga kwa oparesheni maalumu.
Oparesheni asiyoijua. Na alimtambua vyema mkuu wake akisema amesema. Ukimjibu kuwa una mgonjwa anakuomba vyeti vyako ulivyofuzu mafunzo ya udaktari hadi ubaki kumtibu mgonjwa, ukisema unaumwa anakuambatanishia daktari katika msafara wa kwenda katika tukio.
Kwa kifupi hapakuwa na sababu ya kukwepa majukumu akiyatoa.
Na kingine kibaya ni uhasama uliokuwepo baina yake na kiongozi wake wa juu.
IGP!
Uhasama usiokuwa na historia maalumu. Ila uliendelea kuwepo.
Njia pekee ya kukwepa majukumu kiutoka kwa IGP ilikuwa ni kujiua.
Alikuwa hakwepeki!
Inspekta Kobo alichoka sana. Ndani ya masaa machache akausikia waziwazi udhaifu uliouchota mwili wake.
Alipoupeleka mguu wake ofisini akakumbana na barua aliyoitarajia.
Wito!
GIZA lilikuwa ndani ya giza kwa mara nyingine, Konstebo Martin Nguzu alikuwa amempokea mama yake ambaye alikuwa mmoja kati ya wahanga wa ile kamatakamata iliyofanywa kwa masilahi ya watu wachache waliokuwa wamekerwa baada ya mwenzao mmoja kuuwawa kifedhuli.
Ghafla bin vuu mambo yakabadilika, kota zikatishiwa kuchomwa. Wakagwaya na kuwaachia huru wale waliokuwa wamekamatwa katika namna ya uonevu.
Ni giza hilihili sasa lipo ndani ya giza tena, ana kwa ana na mama yake mzazi.
Martin Nguzu alimpa pole mama yake huku akiwa na haraka sana ya kujua ni wapi hasa anapoweza kumpata Majenga waweze kuzungumza na kutambua ama kujitambua upya yeye ni nani na kwa nini haya yote yanatokea.
Hasira zake bado zilikuwa dhidi ya inspekta Kobo aliyeamini kuwa alimchomea ndani ya nyumba kisa mapenzi.
Alipona vipi na nini kinaendelea katika maisha yake haya nd'o makuu aliyojiuliza.
Kuhusu kutafutwa kwa Majenga na watu asiowajua kukapunguza ile hisi yake kuwa chanzo cha kiila kitu ni mapenzi.
Akabaini kuwa lipo la nyongeza.
Mama Martin ambaye hakuwa ameimarika sana kiafya safari hii alionyesha ushirikiano wa hali ya juu, usiku uleule alimpeleka Martin hadi nyumba aliyowahi kuishi mzee Majenga ambapo baadaye alipangisha na kuondoka zake kuelekea Shinyanga.
"Ila Shinyanga sijamuona kabisa..." Nguzu alizungumza wakati wanaelekea katika nyumba ile.
"Bado haujabadilika mwanangu, yaani Shinyanga kubwa vile wewe umtafute mtu usiyemjua na ukampata kabisa. Labda muujiza ama maigizo." Mama alimkata juu kwa juu Nguzu,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi