KONSTEBO NGUZU (14)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... "Ila Shinyanga sijamuona kabisa..." Nguzu alizungumza wakati wanaelekea katika nyumba ile. "Bado haujabadilika mwanangu, yaani Shinyanga kubwa vile wewe umtafute mtu usiyemjua na ukampata kabisa. Labda muujiza ama maigizo." Mama alimkata juu kwa juu Nguzu, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... haikuwa mara ya kwanza hali ile. Tangu utoto wake. Mtoto hakui kwa mama! Walipewa ushirikiano mkubwa sana walipowasili eneo lile, uzuri mtoto wa mzee Majenga alikuwa anaishi katika chumba kimojawapo, na alikuwa pale kama msimamizi wa nyumba ile. "Kumpata kwa leo itakuwa ngumu sana, maana leo watu wametoa kodi. Na yule akipata kodi anamalizia katika ulevi wake.” Mtu aliyekuwa anawapa maelekezo alisema kwa masikitiko. “Unaweza kujua baa ambazo hupenda kuzitembelea?” Nguzu aliuliza kwa udadisi. “Bora angekuwa anaenda b…