KONSTEBO NGUZU (18)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... "Lakini baba, huyu ana pesa na cheo atakusumbua sana. Yaani nina uhakika hautafikia hata nusu ya azma yako." "Kwanini unasema una uhakika." nilimuuliza salama. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... "Si kila kitu kipo wazi, ana pesa na vyeo na zaidi ana kundi kubwa la watu linalomzunguka." “Nd’o maana unasema ni hakika?” “Ndio baba” "Sikiliza mwanangu Salama na uliweke hili milele katika maisha yako, hapa duniani kuna kitu kimoja tu nd'o cha uhakika vingine vyote si vya uhakika. KIFO pekee ndo jambo la uhakika, kila mtu atakufa hii haina mjadala. Ujiue, unyweshwe sumu, ugongwe na gari ama hata ukilala usiamke. Vyote vina maana moja tu ya uhakika.... asije akakudanganya mtu kuwa jambo hili ni uhakika... anakulaghai na wewe unayemsikiliza na kumkubalia unakuwa upande wa mjinga. Sipendi uwe m…