KONSTEBO NGUZU (21)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (21)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Wakaufikia mlango, Nguzu hakuendelea kuwa kondoo. Katika mlango ule wa kioo, aliweza kumsoma yule mlinzi, kuna shambulizi alijiandaa kumkumba nalo kabla hawajaingia ndani ama kuishia palepale. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Nguzu akawa sekunde moja mbele, akatokwa na teke maarufu kwa jina la 'Shukrani ya punda'. Lilikuwa teke la nyuma! Mlinzi ambaye hakutarajia pigo lile akapepesuka mpaka chini, alimanusura bunduki yake imuue yeye mwenyewe kwa kumchoma kooni. Macho yakamtoka pima! Nguzu akawahi kukitoa kisu chake na kujitoa mpaka pale chini kisha akadidimiza katika mkono wa mlinzi. Akatokwa na yowe kubwa kwa muda mfupi, Nguzu akachomoa ile ngumi yake ya kupunguza sauti. Ikamwingia yule bwana na palepale akaiondoa miwani yake. "Naitwa Martin, Konstebo Martin Nguzu . Sikijui kifo bado, ukifanya mfano wa kunida…