KONSTEBO NGUZU (22)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (22)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI ILIPOISHIA... Balaa! Akajaribu kumshirikisha Nguzu aliyekuwa bado hoi. Nguzu hakuwa na la kuchangia. Askari yule imara ndani kwa ndani na legelege kwa umbo la nje alitoweka mpaka chooni. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Huku aliweza kuona kila kitu kilivyokuwa kinaendelea nje. Alimtua Nguzu na kumsihi anywe maji yanayotoka katika bomba ili aweze walau kupata nguvu kiasi. Wakati huo akiendelea kuilazimisha akili yake ifanye kazi kwa kasi zaidi kuhusu tukio linalokuja mbele yao, alifahamu fika kuwa hakuna namna ya kuwa salama angali mle ndani kuna maiti mbili. Kwa namna yoyote yeye na Nguzu watayamalizia maisha yao gerezani. Maji yalikuwa msaada mkubwa sana kwa Martin Nguzu . Hayakumfanya kuwa imara sana lakini walau macho yake yaliweza kuona na aliweza kupumua vyema kwa sababu aliweza kuyaondoa mabonge ya damu yaliyounda uzio mbele y…