KONSTEBO NGUZU (24)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (24)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... "Mpigie tajiri..." Sauti iliyokuwa ya kwanza kumtetemesha Nguzu ilizungumza. Baada ya sekunde chache, mazungumzo yalisikika upande uliosikika zaidi ulikuwa upande wa kwanza huku aliyepigiwa simu akisikika kwa mbali sana. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Simu haikukatwa iliachwa hewani na hapo Nguzu akarushiwa swali. "Unaitwa nani? na upo hapa kwa shughuli gani?" Nguzu akafikiria kuhusu kuongopa kuhusu jina lake, lakini akachagua kucheza karata nyingine. "Naitwa Martin, nipo hapa kwa ...." "Martin nani?" Swali lilitupwa, hadi sasa alikuwa hajaziona nyuso za maadui zake. "Martin Nguzu!" Akamalizia. "Acha upuuzi, hatuna muda wa kupoteza," alijibu kwa hasira kisha akarejea katika simu yake, "Tajiri... huyu mjinga anasema anaitwa Martin Nguzu. Hana faida kwetu...…