
Mtunzi: George Iron Mosenya
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Mtindo wa matukio aliokuwa akiutumia Ngengekuzenza ambaye alisadikika kuwa mkuu wa oparesheni hiyo isiyokuwa na jina ulikuwa mtindo wa akili nyingi kuliko nguvu. Wakilinda huku analipua kule,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
wakiachia hapa anaingia mzima mzima.
Lakini hakuna aliyewahi kumtia machoni.
Mnamo mwaka 1988, Ngengekuzenza anakutwa amepoteza maisha mtaroni bila kuwa na jeraha wala ujumbe wowote.
Maswali mengi yakabaki bila majibu. Wengine wakisema hili hawa wanalipinga bila kuwa na hoja za msingi.
Muhariri akamaliza kupitia alichotaka kupitia kisha akapitia majina yote ya askari waliokuwa wamehamishiwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Konstebo Martin Nguzu!
Jina hili likamkuna sana Juma, akawa anatamani sana kuonana na askari huyu amuulize mawili matatu iwapo ana uhusiano wowote na mzee yule wa miaka ya themanini aliyetikisa nchi na kisha kukutwa amepoteza maisha bila jeraha lolote.
"Nitamtafuta taratibu tu.." alijisemea wakati akiyaweka sawa magazeti yale mengi ili aweze kuaga na kuondoka.
"Kama ni yeye nitaandika makala ambayo itanipa Tunzo ya mwandishi bora. Kupata Tunzo na ujana huu mbona ni fahari sana. Nitawakomesha ofisini watanitungia jina jipya kwa soni itakayowakumba" Alijisemea huku akiwa wima na tabasamu pana usoni.
"Babu kuna gazeti moja ninatoka nalo."
"Ukumbuke tu kurudisha na kulitunza vyema mjukuu wangu Juma." Babu akamsihi.
Juma akaaga na kutoweka. Hakuelekea nyumbani badala yake alifuata uelekea tofauti ili ausogelee mwanga kuhusiana na martin Nguzu.
Alisahau kuwa mwanga haumwepushi mtu kupotea njia, mamia kwa mamia hupotea njia mchana kweupe na jua likuwa linaimulika dunia.
"Siku mbili za msingi katika maisha yako ni SIKU YAKO YA KUZALIWA na ile siku utakayogundua NI KWANINI UMEZALIWA...."
KUPENDWA RAHA, tena raha hii huja pale unapoyaona waziwazi mazingira ya penzi lenu kudumu sana.
Mapenzi mengi yanayohusisha watu wengi wasiokuwa na uwezo mzuri kifedha huvunjika mapema kwa sababu ya kutowajibika.
Sasa penzi la Konstebo Nguzu lingevunjikaje?
Zuu haombi kuongezewa salio kwenye simu, halalamiki kununuliwa simu mpya, ukiona anaomba kulipiwa kodi basi huo ujumbe ameutuma bahati mbaya huenda alikuwa anamaanisha ni yeye anataka kumlipia Nguzu kodi ya pango, haombi kununuliwa nguo badala yake analalamika kuwa kabati limejaa mno hana pa kuweka nguo nyingine.
Sasa penzi linavunjikaje hapo, labda wachokane tu!
Nguzu hakuwa na mpango wa kuchoka penzi hili.
Penzi lililomfanya anawiri na kujisahau kabisa kuwa yeye ni Konstebo, kuna kipindi aliwahi kujiona kuwa yungali Mkuu wa majeshi yote ya ardhi na anga nchini Tanzania.
Mapenzi bwana!
Ikiwa imepita miezi takribani minne tangu gundi ya huba iwaunganishe wawili hawa huku lile pepo la wizi wakilihalalisha na kuwa halali.
Konstebo Nguzu alikuwa eneo lake la kazi majira ya asubuhi.
Ilikuwa yapata saa mbili na dakika chache asubuhi katika kituo cha polisi Magomeni usalama, mgahawa ulikuwa umesheheni tayari wateja ambao asilimia kubwa walikuwa ni askari wa kituo kile. Nguzu akiwa mmoja kati yao
Si kwamba raia wema hawakuruhusiwa kutumia mgahawa ule lakini kama ilivyo ada ya Tanzania, raia wanawaogopa askari wao na askari wanapenda kuogopwa.
Watachangamanaje?
Mama muuza alikuwa amejikita katika kuwahudumiwa supu na chai askari waliokuwa wakiwania, kila mmoja akitaka kuhudumiwa wa kwanza ili aingie katika majukumu yanayomuhusu.
Vyeo hadi kwenye chakula cha kulipia? Nguzu alinung'unika katika nafsi yake baada ya kuambiwa ampishe askari mwenzake ahudumiwe kwanza kwa sababu tu alikuwa amemzidi cheo.
Akatii!
Kanuni muhimu kabisa katika jeshi, akawa ameifuata.
Kitendo cha kukatishwa zamu yake kikamfanya anune, kisha akaghairi kunywa supu akaagiza soda baridi akaketi na kuanza kunywa.
Hata kabla soda haijafika robo, akatakiwa kumpisha kiti mkubwa wake mwingine aketi.
Sasa ladha ya soda ikabadilika ghafla na kuwa chungu mithiri ya pombe inavyokuwa kwa mnywaji wa siku ya kwanza.
Akiwa ameegemea ukuta alijitazama begani hakuwa na nyota hata moja mwenzake alikuwa ameanza kuchafuka begani.
"Konstebo!" Sauti ikamtoa katika lindi la mawazo.
Akageuka huku na kule kutazama ikiwa ni yeye anaitwa ama kuna konstebo mwingine jirani na yeye.
Hakuwepo!
"Konstebo!" akaitwa tena kwa cheo chake, cheo cha chini kabisa katika jeshi la polisi. Akaitikia wito, akamwona yule bwana mwenye cheo cha Inspekta akimwonyeshea ishara kuwa kiti kipo wazi aketi.
Akaruka upesi akatua katika kiti.
Kitendo cha kupewa kiti na Inspekta kikarejesha ladha ya soda ile na ubaridi ukapenya vyema kooni.
Akiwa katika utulivu wa hali ya juu bila kuingilia mazungumzo aliyoyakuta alibaki kuinywa soda yake kwa hatua ndogo ndogo.
Lakini alikuwa anatetemeka, na hapa akagundua kuwa kuketi na watu wanaomzidi vyeo lilikuwa jambo lililomuathiri kupindukia.
Masiko yake yalikuwa wazi kusikiliza mazungumzo ya wawili aliowakuta pale.
Ilikuwa ni kuhusu kesi fulani iliyoonekana kuwasumbua vichwa, alitamani kuchangia hoja kidogo lakini akakumbuka kuwa wenzake walisahau ni lini mara ya mwisho kuwa katika cheo chake cha chini.
Akaufunga mdomo.
Lakini kichwani alikuwa anazungumza akijaribu kuwashauri wawili hawa ni kitu gani wanapaswa kufanya kuhusiana na kesi iliyokuwa mikononi mwao.
"Hawa watu nyota zao zote ni bure kabisa, sasa wao wanaona suluhisho ni kumkamata mke wa mshtakiwa. Je kama huyu bwana alimwoa huyu mwanamke ili kumfurahisha mama yake tu.. atajali nini? Mi binafsi sioni kama ni suluhuhisho...." akatokwa na tabasamu jepesi. Inspekta akaliona.
"Vipi Konstebo mbona unatabasamu, ni utamu wa haya mazungumzo ama..."
"Hapana afande, ni utamu wa hii soda, sijatumia siku nyingi sana..." Akajibu kwa utulivu wa hali ya juu.
"Unaitwa nani Konstebo..."
"Konstebo Nguzu, Martin Nguzu afande!"
"Unaitwa nani.." akauliza tena, Konstebo Nguzu akajitambulisha tena kwa ukakamavu.
"Sawa Konstebo Nguzu. Unaweza kutupisha kidogo sasa!" Inspekta alimwamuru, Konstebo Nguzu akajiondokea huku kichwani akiona ni jambo la fahari sana kujihusisha kimapenzi na Koplo Zubeda. Kwani kwa kufanya hivyo anayapooza maumivu yake yote ya kuamrishwa hovyo kila mara.
Amri alizoamini kuwa ni dharau!
Akiwa yu katika fukuto la ghadhabu, simu yake ya mkononi ikaitwa. Akalitazama jina na kupokea upesi.
Walau alikuwa amepigiwa na Koplo Zubeda, mwanamke aliyekuwa anamfariji na kumpa raha, hali iliyomfanya kuzisahau shida zake.
Wakazungumza kwa dakika kadhaa kujuliana hali kisha wakaagana huku wakipeana ahadai kedekede.
Kisha wakaingia kazinui, kila mmoja katika kituo chake.
Nguzu Magomeni na Koplo Zuu Chang'ombe polisi Temeke.
_______
SIMU YA JUMA (Kimbelembele) ilimweka, bado alikuwa kitandani maana hiyo ilikuwa ni siku yake ya mapumziko.
Koplo Mtani, jina lilisomeka. Akapokea upesi.
"Amakweli ukiwa unakitafuta kitu kwa dhati sana unaweza usikipate ila huwa kinajileta wakati umekata tamaa tayari." Alianzisha maongezi bila kusalimia.
"KUnani tena afande."
"Leo nimekutana na Nguzu wako. Tena tumeketi meza moja asubuhi kweupe pee! Kumbe ni ka konstebo, kapole halafu kakijana tu. " Alijibu kwa bashasha Koplo Mtani.
Juma akaketi kitako, na kuuliza maswali mfululizo. Koplo akayajibu yote kiufasaha na kumweleza kuwa siku inayofuata afike kituoni amwonyeshe mtu wake.
Damu ya muhariri wa gazeri la Siri Kali ikachemka, ubinafsi alioanza nao ukaendelea kumtawala hakumwambia mtu ni mpango gani anao dhidi ya Konstebo Martin Nguzu.
Kwanini amshirikishe mtu angali aliamini kuwa anenda kuandika makala pekee??
Amakweli maarifa mengi, mbele kiza!
Maarifa ya muhariri Juma Kihwele (Kimbelembele) hayakumfanya ang'amue kuwa si kila mtembezi hujua uelekeo.
Akatamani siku iliyotajwa ifike upesi.
Masaa akayaona hayasogei, hayawi hayawi mwezi ukaondoka zake baada ya kumaliza utawala wake wa muda, jua likatoka katika usingizi wake na kuisalimia dunia.
Akaianza siku na kauli dogoshi ya Koplo Mtani, 'Ni ka konstebo , kapole halafu kakijana tu'.
"Ukihisi unaweza kufanya jambo fulani, sawa UPO SAHIHI.
Ukihisi hauwezi kufanya jambo fulani, sawa UPO SAHIHI pia.
Maamuzi ya KUWEZA ama KUTOWEZA yapo katika himaya yako......"
KIMBELEMBELE kilimfanya Juma Kihwele akose usingizi kabisa, alijigeuza huku mara ageuke kule. Alijisemesha kwa sauti ya chini na kucheka mwenyewe.
Mzigo wa kimbelembele kile ulikuwa mzito sana na dhahiri ulionekana kumwelemea. Akaamini kabisa bila kukigawa kidogo kile kimbelembele basi huenda pasingekucha.
Akamuita mkewe chumbani.
"Dear, nimeshindwa kulala mwenzako"
"Ushaanza! hapo unataka kuniambia matukio yenu ya kisiasa huko. Mi siyawezi." Alijibu mkewe huku akiketi.
"Bora ingekuwa habari za siasa, ya leo kubwa kuliko. Jamani mapenzi haya.." akasita akajikohoza kisha akaendelea.
"Unamfahamu Koplo Zubeda Msangi."
"Eeh! namfahamu si huyu mama wa hapo mtaa wa pili. Uliyeniambia wakati ule kuwa ni nyumba ndogo ya Inspekta nani vile."
"Eewala! Inspekta Kobo." Akahitimisha kwa madoido muhariri Juma Kihwele wa gazeti la SIRI KALI.
"Kafanya nini tena maana we nawe na kazi yako. Kuna habari kaandikwa ama..." Akahoji kwa utulivu akionekana kuwa bado hajavutiwa na simulizi hiyo ya mumewe.
"Bora angekuwa ameandikwa... Sikia ipo hivi, nilikuwa namfuatilia kijana mmoja hivi ni askari. Kuna vitu kadhaa nahitaji kujua kuhusu yeye. Huwezi amini katika kumfuatilia nikamwona anakuja hadi nyumbani kwa Koplo. Kama kawaida yangu nikitaka kujua jambo sichoki, nikaendelea kusubiri hadi walipotoka. Kwa kifupi Koplo Zubeda Msangi anajihusisha kimapenzi na hako kakijana kapole Konstebo Martin Nguzu ambaye nahitaji kufahamu mambo kadhaa kuhusu yeye." Akamaliza na kumtazama mkewe.
Bado hakuonekana kuvutika!
"Ubaya ni kwamba huyo sijui Konstebo sijui Inspekta wote siwajui vizuri. Nd'o nashindwa kuelewa unashindwa kulala kwa nini haswa. Kisa Zubeda anajihusisha na mtu mwingine amakiasa nini. Nifafanulie basi...."
"Mke wangu, katika kazi yetu ya uandishi kuna mambo mengi. Kuna baadhi ya fursa huja zenyewe machoni, hapa unabaki kupima mzani nani anakupa pesa nyingi. Je? ni bosi wako ofisini ama ni huyo muhusika wa hii habari..."
"Kwa hiyo unataka kuigeuza biashara hiyo habari? Na wewe ulipolala na yule dada wa mapokezi nani aligeuza biashara lile tukio lako ama wewe tu nd'o wayaona mabaya ya wenzako..... nilijua umeniitia mambo ya maana kweli mume wangu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi