KONSTEBO NGUZU (8)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Alihofia kulala kitanda kimoja na mume wake ambaye amemsaliti, aliogopa sana shetani mpenda kifo asije kumwingia kichwani na kumsababisha amdunge mume wake sindano ya sumu.

Aliijua hasira yake hasahasa ambapo mumewe angejaribu kumwongopea zaidi.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Licha ya kujifaragua wakati yupo hospitali kwa Zubeda kuwa hana mapenzi ya dhati sana kwa mumewe, aliongopa na moyo wake ulilijua fika hilo.

Daktari huyu hakuwa na mahali pengine pa kuzilaza hisia zake zaidi ya kifuani kwa Inspekta Kobo.

Sasa angali anapambana mumewe asijafuliwe jina lake, tayari mambo yamekuwa kinyume.

Akanyanyua simu yake na kumpigia yule muhariri Juma aliyemfuata na kumshirikisha juu ya habari ile na kumtaka wafanye biashara.

Simu haikupokelewa.

Akatuma ujumbe mfupi ulioambatana na kitisho kikubwa.

Mmoja asiyekuwa na moja wala mbili alikuwa ni Inspekta Kobo.

Habari hii ilimfanya akayatafuta magazeti yale mara moja, akaziendea kurasa zilizoelezea kwa kina juu ya habari ile.

Akashusha pumzi kidogo baada ya kukuta jina lake halijawekwa wazi lakini mwandishi wa makala ile alionyesha kujua kila kitu ni vile hakuamua kutajha katika makala hii ili aje kuuza magazeti mengine wakati mwingine atakapoamua kulianika jina la muhusika waziwazi.

Inspekta akakumbuka kile kiwiliwili chini ya mti. Akaamini kuwa ni kiwiliwili kile kilimuona wakati anaingia na kutoka.

Yule mwandishi alijuaje nitaenda kwa Nguzu eeh! alijiuliza Inspekta huku ikimjia pia ile sauti aliyoisikia usiku ule.

Sauti ambayo si ngeni lakini alikuwa ameisahau tayari.

"Lakini sijamuua Nguzu mimi. Mungu wewe ni shahidi. Niliitafuta amani tu..... nilipanga kumuua lakini nilighairi wanishushudia mwenyezi Mungu." Alizungumza peke yake Inspekta huku moyo wake ukiona haya kwa sababu ni mwaka mzima na miezi ilipita bila kuingia katika nyumba za ibada.

Akarejea katika magazeti yale na kusoma majina ya waandishi wa habari zile.

Akabaini kuwa zile habari zilifichwa jina la mwandishi wakaishia kufanya mazoea yao ya kuandika kuwa imeandikwa na MWANDISHI WETU.

"Attaccati a sto cazzo" Akabwatuka lile tusi pekee la kiitaliano analolifahamu huku akiyatupa yale magazeti mezani.

"Who the hell is mwandishi wetu?! eeh! kwani sisi hatujui aliyeandika habari hiyo ni mwandishi wenu you bastard!" Alilalama peke yake huku sasa akiwa wima.

Akajaribu kuwafikiria wafanyakazi wa magazetini ambao ni wasumbufu. Ambao siku hazipiti hawajapiga simu jeshi la polisi kuuliza maswali kadha wa kadha.

Akainyanyua simu yake na kupiga katika kitengo cha mawasiliano jeshi la polisi.

"Komredi, umekuwepo kwenye shifti tangu jana?" akaulizia.

"Nimekaa siku ya tano leo, mwenzangu anaumwa. Vipi afande..."

"Naulizia kama kuna simu yoyote kutoka gazeti la SIRIKALI..."

"Lile gazeti la Juma Kihwele.." akauliza kimasihara. wakacheka kidogo kwa sababu walimjua vyema.

"Yule bwabna sijui atakuwa anaumwa. Leo siku ya sita au saba hakuna simu kutoka kwake."

Inspekta akashukuru na kukata simu.

"Huyu mjinga kuna kitu anajua, hawezi kukaa kimya siku zote hizi." alijisemea huku akichukua kalamu yake na karatasi kisha akaainisha mambo kadhaa.

MOJA, Juma Kihwele anaijua hii habari lakini ameogopa kuiandika kwa jina lake.....

PILI, haijui hii habari lakini alivyo na kimbelembele anaifuatilia kwa kina akiandika awalipue wahusika.

Yote mawili yalimaanisha kuwa Juma ni mtu muhimu sana katika hili jambo.

Inspekta akaingia chumbani kwake, akaitoa bastola yake mafichoni na kuitazama kwa muda kisha akasema nayo.

"Let's go to work boy! (Twend'zetu kazini)"

Simu yake ya mkononi ikaita wakati akiipachika bastola yake pahali alipozoea kuipachika.

Ilikuwa ni simu kutoka kwa mkewe.....

Mapigo ya moyo yakaenda mbio sana.

Inspekta akashukuru na kukata simu.

"Huyu mjinga kuna kitu anajua, hawezi kukaa kimya siku zote hizi." alijisemea huku akichukua kalamu yake na karatasi kisha akaainisha mambo kadhaa.

MOJA, Juma Kihwele anaijua hii habari lakini ameogopa kuiandika kwa jina lake.....

PILI, haijui hii habari lakini alivyo na kimbelembele anaifuatilia kwa kina akiandika awalipue wahusika.

Yote mawili yalimaanisha kuwa Juma ni mtu muhimu sana katika hili jambo.

Inspekta akaingia chumbani kwake, akaitoa bastola yake mafichoni na kuitazama kwa muda kisha akasema nayo.

"Let's go to work boy! (Twend'zetu kazini)"

Simu yake ya mkononi ikaita wakati akiipachika bastola yake pahali alipozoea kuipachika.

Ilikuwa ni simu kutoka kwa mkewe.....

Mapigo ya moyo yakaenda mbio sana.

Akaipokea ile simu huku akiwa anatetemeka mikono yake katika namna iliyomtishia amani.

Alipoiweka simu sikioni kimya kikatanda kutoka upande wa pili.

"Mama! Mama! Mke wangu... ongea basi mama." alizungumza kwa upole wa hali ya juu.

Badala ya kujibiwa akaanza kusikia pumzi zikipishana kwa kasi sana na hapo akaanza kukisikia kilio.

Dokta Kobo alikuwa analia.

Suala la mkewe kuangua kilio ikawa kama msumari wenye ncha kali unasukumwa katika paja lake angali ana fahamu zote.

Maumivu!

"Mama Melinda! una nini mke wangu nieleze... au niambie basi upo wapi nije sasa hivi." Alisihi Inspekta Kobo lakini simu ikakatwa bila kusikia neno lolote.

Akapagawa.

______

SHAMALIWA, Mwanza.

Umati wa watu haukuwa mkubwa sana. Walikuwa ni wanafamilia walioridhia ile taarifa ya kifo cha ndugu yao.

Mama mzazi wa Nguzu hakuisha kulia na kulalamika kuwa alimkanya mwanaye asijiunge na jeshi lakini hapohapo akikiri kuwa ugumu wa maisha ulikuwa chanzo cha yote hayo.

Waliojaribu kumbembeleza walikuwa wamefikia kikomo na sasa walimwacha alie kuzimia na kisha kuzinduka peke yake.

Kuzika majivu! Mama yake alikataa kata kata, alidai kuwa hakuyaaga majivu katika kituo cha basi bali alimuaga mwanaye tena kwa kumkumbatia, leo hii akubali kuyazika majivu asiyoyajua?

Hapana... akasimama kidete na wanafamilia wakamuunga mkono, hawakufanya maziko hayo.

Ambaye aliamini Martin Nguzu amefariki sawa, ambaye hakuamini sawa.

Mama Martin hakuwa katika upande wa walioamini.

Na kila alipojaribu kuamini, lilikuja wazo jingine kuwa yawezekana mwanaye amefanyiwa ubaya tu. Sio kifo cha kawaida.

Ndivyo walivyo akinamama.

Ule uchungu wa mwana unasababisha haya.

Siku ya tano ikiwa inayoyoma na jambo hililikiwa limepunguza makali mioyoni mwa wengine kasoro mama mtu.

Majira ya usiku ule uliingia ugeni ambao hakuna aliyeutilia maanani, maana kwa kipindi hicho watu walikuwa wanakaa nje, ndugu na jamaa wanacheza mchezo wa karata mpaka usiku wa manane na wengine kulala nje kabisa.

Huyu bwana alikuwa mkimya kabisa na koti lake kubwa la kuzuia baridi, alijitikisa kwa sababu za msingi tu na hakugeuka huku wala kule, alikuwa amejiinamia.

Kadri muda ulivyozidi kwenda na watu walizidi kupungua, wengi walienda kulala.

Huu nd'o muda ambao yule bwana alijitikisa tena kwa kiasi kikubwa.

Alisimama!

Akapiga hatua kadhaa bila mtu yeyote kumtilia mashaka, akasogea pembezoni akaichomoa pakti ya sigara na kutoa moja, akaiwasha na kuuvuta moshi wake ndani ya kifua chake na kwa umaridadi kabisa akaupuliza angani kisha akautazama unavyotokomea angani.

Akafanya vile takribani mara tatu, kisha akaizima. Akapiga hatua nyingine tena akaufikia mti kisha akaanza kuyatazama mazingira ya pale kwa uchache akahisi ni wakati muafaka wa kufanya kusudio lake na hakuona jambo lolote la kumzuia.

Akapiga hatua huku mkono wake ukiwa katika mifuko yake, akajipitisha jirani kabisa na kundi la akina mama wawili waliokuwa wamejilaza.

Akamwona muhusika wake.

"Ndiye!" akajisemea.

Kisha kwa kitendo cha upesi sana akainama, akamziba mdomo na kisha akaichomoa silaha yake na kwa lugha ya vitendo akazungumza naye.

"Ukileta vurugu nitakuchinja."

Huku akiwa amemdhibiti vyema kabisa akamnyanyua wakaondoka kutoka katika eneo lile.

Alipomfikisha pembeni kiasi akampiga teke kali miguuni, kisha akatua naye chini.

"Mzee Majenga anaishi wapi?" lilikuwa swali kavu kabisa kutoka katika sura ngumu.

Mama akabaki kuhangaika asijue ni nini hiki kinatokea angali ana kovu la msiba wa mwanaye wanatokea watu kumuuliza juu ya mzee Majenga.

"Alihamia Shinyanga." alijibu kwa ufupi.

"Nitakuua sina masihara. Alihamia lini na awali alikuwa ana anishi wapi? nani ndugu zake?" Alijaza maswali mazito.

"Kama mwanangu mmemchoma moto, ukinichinja hautakuwa umefanya dhambi mpya. Nipeleke kwa mwanangu, sina jibu jingine...." Alijibu kikaidi. Huku nafsi yake ikiwa radhi kabisa yule bwana amuue ili aondokane na huu uchungu wa kuishi bila mwanaye.

Mkono wenye nguvu ukashusha ngumi katika bega la yule mama kisha kiganja kikawahi kuziba mdomo.

Maumivu yakanyimwa kilio.

Yule mama akabaki kuhema juu juu huku akiwa ameyakodoa macho yake.

"Sasa utanijibu vizuri kabisa sivyo. Mzee Ma..." hakuweza kumalizia akahisi kuna mguso fulani kwa mbali katika bega lake.

Akageuka bila hofu yoyote, akakutana na giza likiwa ndani ya giza.

Lakini hili halikuwa giza ambalo linaweza kutembea.

Ngumi kali ikatokea katika lile giza la maajabu, ngumi moja ikatua katika koo la yule bwana.

Akajaribu kukohoa akawa ameikohoa roho yake. Umauti ukamfika.

"Mama!" giza lile likaita.

Mama aliyekuwa anahema juu juu huku akiwa anafanya dua maalumu kwa ajili ya kuiaga dunia akarejea katika fahamu zake.

Haikujalisha giza lile lilikuwa totoro kiasi gani, mama alitambua ubini wake ipasavyo.

"Martin!" akaita.

"Nipo hai mama." akajibiwa.

Mama akaamka akaketi kitako asiamini kuwa alikuwa anapokea miujiza katika uzee wake.

Ubaya wa wanawake siku zote ni pale akili zao zikitulia.

Mwanzo alikuwa ametulia tuli akizungumza na lile giza, lakini baada ya akili kukaa sawa akaanza kupiga mayowe.

Mkono ukawahi kumziba mdomo.

"Mama, huyu alikuwa anataka nini kwako."

"Simjui."

"Mama, sijauliza kama unamjua. Alikuwa anataka nini?"

"Muulize labda wewe atakueleza vizuri."

"Hakuna mzoga uliowahi kuzungumza katika dunai hii mama. Nieleze.."

"Amemuulizia mzee Majenga.... yule mzee alikuwa rafiki sana na babu yako. Wewe humjui..." alitoa maelezo yale.

Majenga!

Jina lile likapiga katika kichwa chake kwa kujirudiarudia, ni jina hili lilimjia punde tu baada ya kurejewa na fahamu asijue nani aliliingiza katika kichwa chake.

"Uliponaje mwanangu, nyumba iliteketea yote ile. Tuliona kwenye Televisheni.." mama alimuuliza.

"Mama usimwambie mtu yeyote kama umeonana na mimi, mimi nipo hai na ninaamini nina kazi kubwa ya kufanya kabla sijasimama hadharani na kuutangazia uma kuwa ninaishi."

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni