KONSTEBO NGUZU (9)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... "Uliponaje mwanangu, nyumba iliteketea yote ile. Tuliona kwenye Televisheni.." mama alimuuliza. "Mama usimwambie mtu yeyote kama umeonana na mimi, mimi nipo hai na ninaamini nina kazi kubwa ya kufanya kabla sijasimama hadharani na kuutangazia uma kuwa ninaishi." JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alisihi Nguzu. Kisha akamkumbatia mama yake na kumbusu shavuni. Upesi mama akaipapasa shingo ya nguzu katika giza lilelile. Na hapo akatokwa na tabasamu pana lililosindikizwa na machozi ya furaha. Aliyekuwa mbvele yake alikuwa yuleyule mtoto aliyetoka katika tumbo lake. Martin Nguzu! Ameponaje? hilo halikuwa swali lililomuhangaisha...... Bora uzima. Walizungumza kwa dakika kadhaa kuhusu Majenga kisha wakaagana. Akiwa anafanana na giza kwa jinsi alivyovaa alitembea kwa tahadhari kubwa huku akiamini wapo wengine wanaweza kuvaa…