MAUAJI YA KASISI (3)

Zephiline F Ezekiel
MAUAJI YA KASISI (3)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Black Cheetah alishtushwa na wito huo kutoka katika lindi la mawazo, akawatazama wanakikundi wenzake ambao yeye aliona wangefaa kwa kazi hiyo lakini sasa walimfanya hata yeye kushikwa na wasiwasi. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Ok, tunafanya kazi au hatufanyi tuchague moja” aliwapa mtego. Baada ya kutafakari mara mbili mara tatu wote waliamua kuingia kazini kuisaka hiyo monstrance. Miaka kumi nyuma… Al-hamis kuu 1996 Kanisa la Holy Family lilishehani watu mapaka nje wakifuatilia misa takatifu ya alhamis kuu ambapo yalifanyika maadhimisho ya karamu ya mwisho. Hakukuwa hata na njia ya kupita kuelekea popote kila mtu alipo basi ni hapohapo. Katika madhabahu makasisi wapatao sita pamoja na baba Askofu walikuwa wakiendesha misa hiyo kubwa ambayo mwisho wake huwa inakuwa na maandamano ya kuhamisha mwili wa Bwana kuupeleka mahali pengi…