MKONO WA JASUSI (20)

Zephiline F Ezekiel
MKONO WA JASUSI (20)
Jina: MKONO WA JASUSI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI ILIPOISHIA... Wakakokotana mpaka mtaa huo, Amata akaonana na yule kijana, kweli, akamkaribisha na kumpa kompyuta yake ya mezani aitumie. Akaibomoa mfuniko wake na kuipachika ile Hard Disk ili kupata vilivyomo. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Wkati akiendelea na kazi hiyo Yule mwanadada akapitiwa na usingizi, alkadhalika Yule kijana. Ndani ya disk ile kulikuwa na mafaili mengi ya ajabu ambayo yalkimfanya Kamanda kusisimkwa na mwili, mipango michafu ya kuua na kupoteza, mipango ya ibada za kishetani za kundi hilo, mikataba ya ulaghai walioifanya na makampuni mbalimbali pale Afrika ya Kusini na kuwadhulumu kwa mtindo huohuo wa kuua na kubadilisha mikataba wakitoa vitisho na rushwa kwa watendaji wa serikali. Kulikuwamo na mafaili ya sauti ambayo yalirekodiwa ama katika mikutano Fulani au vikao vya siri, yaliyozungumzwa humo yalikuwa ni mazito, …