
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kwa mbali alimwona Don akifanya uhakiki wa tiketi zake, jicho la Kamanda likatua kwa mwanadada aliyekuwa akiifanya kazi ile, ‘Bingo!’ akajisemea kisha akasubiri Don na vijana wake waondoke katika eneo lile ili naye akafanye yake.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Alipohakikisha Don keshaingia ndani kabisa, akavuta hatua na kuwapita baadhi ya wasafiri waliokuwa kwenye foleni huku akiwaomba samahani na moja kwa moja akafika kwenye kidawati cha Yule mwanadada.
“Habari msichana! Mimi ni mwanausalama,” akamwonesha kitambulisho ‘feki’ cha upolisi wa Afrika Kusini.
“Ndiyo nikusaidie nini?” Yule mwanadada akamwuliza, na kamanda akaeleza shida yake; bila hiyana akapatiwa maelezo yote kuwa Don anaelekea Canada katika jiji la Ontario kwa ndege ya shirika la USA, IATA Airlines. Akamshukuru na kauondoka eneo hilo.
§§§§§
“Yes! Madam S, mzigo wetu umeelekea Canada mchana huu,” kamanda akamwambia Madam kwa simu aliyompigia mara tu alipoingia ndani ya gari lake.
“Ok, sawa, nitakupigia muda si mrefu, lakini jiandae kwa safari ya nyumbani kwani nitahitaji maelezo ya kina kutoka kinywani mwako wewe mwenyewe,” Madam S akamweleza na kisha akakata simu.
Dakika ishirini baadae Kamanda Amata alifika Hoteli 77, akilini mwake alijua wazi kuwa lazima kuna wanaomsubiri hapo. Akaegesha gari mahali pa peke yake kisha akateremka. Hakupitia mlango wa siri wala njia za panya, moja kwa moja aliingia kupitia mlango wa mbele, kwa macho ya uchokozi aliweza kumuona kila mtu aliyekaa na aliyesimama, mara moja akajua nani mbaya na nani mwema kwake.
Vijana wawili waliokuwa wakisoma magazeti kila mmoja kwa nafasi yake waliyateremsha kisha mmoja akanyanyuka na kumfuata Kamanda kule alikoelekea, lakini alipoingia kwenye lifti na kusuka hakumwona, akachanganyikiwa hakujua ni mlango upi kaingia.
§§§§§
Kamanda Amata alikagua chumba chake na kugundua kuwa kilipekuliwa kwa mara nyingine lakini hakujali, alikusanya kilicho chake na kutia katika begi kisha; alipohakikisha kila kitu kipo tayari akajipanga kuondoka lakini alikumbuka kuna mmoja aliyemfuata kuja huko hivyo alijua kama si mlangoni basi kuna mahali watakutana. Akafungua mlango na kuufunga nyuma yake, akimwona Yule kijana mwisho wa korido akijifanya kuangalia nje, akaachana naye na kuondoka.
Yule kijana alimfuata kamanda na kuingia lifti ya upande mwingine huku kamanda akiwa tayari kateremka kwa lifti nyingine. Alipofika gorofa mbili kabla ya kufika chini, akateremka na kusubiri lifti ya upande ule alioingia Yule kijana, akaizuia kwa kubonyeza kitufe Fulani chenye mchoro wa pembetatu. Mlango ukafunguka, ndani ya lifti alikuwapo Yule kijana peke yake, akapigwa na butwaa na kutoa macho baada ya kumuona Kamanda akiingia mbele yake.
“Unashangaa nini? Ulifikiri huwa nafuatwa kijinga hivyo?” kamanda akamwuliza na kisha akampa pigo moja la karate lililotua kwenye paji lake la uso, Yule jamaa akajibamiza kisogo na kupoteza fahamu huku damu kidogo zikitoka puani.
§§§§§
Vijana wapatao watano walilizunguka gari la Amata pale lilipoegeshwa. Alipotoka aliwaona vijana wale akaelewa lengo lao. ‘Bado wananiandama,’ akawaza na kuvuta hatua kuelekea maegesho ya tax.
“Hii hapa mzee,” kijana mmoja alimkaribisha kwa ukarimu naye akaitikia kwa kichwa huku akiwa amesimama akiwaangalia wale vijana wa kizungu. ‘Nawahurumia sana, lakini kutokana na upumbavu wenu nitawaonesha maajabu ya Mlima Kolelo,’ akawaza na kutabasamu. Wale vijana walikuwa bado wamesimama kwa kuliegemea lile gari. Amata akatoa rimoti yake na kubofya hapa na pale. ‘Na hii ndiyo dawa yenu, pumbavu sana nyie!’ akajisemea moyoni mwake kisha akabonyeza tab iliyoandikwa OK.
Mlipuko mkubwa ukatokea, ile gari ikalipuka na kufumuka vipande vipande, milango ikirushwa juu na magurudumu vilevile.
Kamanda Amata akaingia ndani ya ile tax.
“Twende!” akamwamuru dereva, wakaondoka eneo lile na kutokomea.
“Tunaelekea wapi?” popote penye hoteli kubwa unayoona wewe inanifaa,” akamjibu na moja kwa moja akampeleka kwenye Hoteli ya Good Hope yenye hadhi ya nyota tatu. Akamlipoa na kisha akamwacha aondoke. Alipotokomea, akazunguka mtaa wa pili na kuchukua tax nyingine na kuelekea uwanja wa ndege.
DAR ES SALAAM – saa 4:09 Usiku.
MADAM S, CHIBA NA GINA walikuwa uwanja wa ndege, ndani ya gari yao bila kushuka, Chiba akiwa nyuma ya usukani. Kioo kikagongwa mara tatu na mlango ukafunguliwa na Gina.
“Karibu Kamanda, tupo kwa ajili yako,” Gina akamwambia huku akimkumbatia.
“Nashukuru, nimetoka kwenye midomo ya Mamba mwenye njaa au samba aliyejeruhiwa,” akajibu na kuketi sawia ndani ya gari hiyo kisha mlango ukafungwa.
“Kamanda Amata!” Madam S akaita, “Ni hapahapa ambapo safari yako itakwisha na kuanza, nipe tafutishi zako harakaharaka,” Madam akamwambia na Amata akatoa yale makabrasha akampatia Madam na ile hard disk.
“Ndani ya hiyo drive mtapata siri na mikakati mingi ya kishetani ya hao jamaa, zaidi ya ile tuliyokuwa tukiitarajia,” Kamanda akaeleleza.
“Ok, Chiba atapitia na kuweka vizuri taarifa zote,” Madam S akaeleza.
“Sasa Amata, ipo hivi; hauna muda wa kupoteza, kazi ipo kwenye wakati mzuri sana kwani imeonekana Robinson Quebec ndiyo kila kitu katika mpango huu kadiri ya maelekezo yako na taarifa fupi ulizonitumia. Hivyo basi, hauna budi kuondoka kwenda kumsabahi kule Canada ili hata nay eye akufahamu kwa ukaribu,” Madam aliongea huku akiwa ameivua miwani yake na kumtazama Amata kwa jicho pembe.
Wakati huo Gina alimkabidhi Amata bahasha ambayo ndani yake ilikuwa na tiketi ya safari na hati nyingine ya kusafiria ambayo ilimtambulisha kwa jina jipya, tayari ikiwa na viza ya mwezi mzima.
“Fika Ontario, kisha maelekezo utayakuta hukohuko,” Gina akamalizia na kuketi vizuri kitini.
“Kamanda, naomba urudi salama, na likizo yako utaikuta ukirudi,” Madam akamalizia na wakati huo Amata tayari alikuwa nje ya gari hiyo.
§§§§§
DURBAN, AFRIKA YA KUSINI - Saa 4:00 usiku
LERETI KHUMALO hakuamini kusoma barua pepe iliyoingia katika box lake mchana wa siku, hiyo, hii nayo ilimpa furaha ya ajabu ambayo hakuwahi kuihisi katika siku za karibuni.
‘Robinson anataka kujitoa katika ubia wa kampuni yetu, jambo jema sana, bora nijiendeshe mwenyewe,’ aliwaza mwenyewe huku akiwa kaikodolea macho laptop yake iliyokuwa mapajani wakati akisubiri kuondoka.
Mwisho wa barua ile ilimtaka kufika Canada ili kutialiana saini katika hati ya kuvunja ushirikiano huo, alitakiwa kutaja tu ni siku gani ambayo ataweza kufika huko ili wanasheria wa pande mbili wajiandae kwa tukio hilo. Lereti muda huohuo akawasiliana na katibu wake naye akakiri kuipata barua hiyo isipokuwa alikuwa hajaifanyia kazi, akaandika barua pepe kwa mwanasheria wake na kuwaambia wajiandae kwa safari na siku ya tatu yake wakutane Ontario Canada.
Lereti alivunja mapumziko ya Dar es salaam na kuona kuwa atakaa siku moja tu kwa kujiandaa kwa safari hiyo kisha aungane na watu wake huko Canada.
Dakika chache baadae alikuwa ndani ya ndege kuelekea Tanzania ambako sasa si mapumzikoni tena bali ni kupita tu.
Kichwa chake kilikuwa kikitawaliwa na wazo moja kubwa; jinsi ya kuendesha kampuni ile peke yake kwa manufaa ya familia yao, kuhakikisha jina kubwa la Khumalo linarudi katika hadhi yake. Akiwa katika wimbi la mawazo akapitiwa na usingizi na kuzama katika ndoto za moyoni, mara alicheka, mara alihuzunika ilimradi tu ndoto ilinoga.
Alishtushwa tu mara chache alipotakiwa kuamka ili apate chochote naye akafanya hivyo, na saa tano baadae alishtuliwa na sauti ya mwanadada iliyomtaka kufunga mkanda kwani safari ilikuwa imefika mwisho wake; akafanya hivyo.
ONTARIO – CANADA
WAGENI wa Robinson Quebec waliwasiri katika jiji hilo ndani ya muda mchache tu tangu wapewe wito huo. Hawakuwa wengi, ni watu takriban kumi na sita hivi, kila mmoja alikuwa na ham,u ya kujua ni nini hasa mkuu wao amewaitia tena ghafla hivyo. Kila mmoja alifikia kwenye hoteli aitakayo kadiri ya matakwa yake isipokuwa tu walijua wazo kuwa usiku wa siku inayofuata ndio kikao hicho kitaanza kwa ibada maalumu na kutoa kafara ya damu mbichi ya mwanadamu kisha ndio wazungumze yaliyowapeleka. Daima mikutano yao ilifanywa usiku wa manane kwatika hali ya siri na ulinzi mkubwa.
Siku hii tayari walinzi wao walitapakaa sehemu mbali mbali ya jiji la Ontario ili kujua kama kuna lolote linalozungumzwa na ikijulikana basi we uliyesema umekwenda na maji.
Don Angelo moja kwa moja alifikia katika hoteli kubwa ya kifahari ambayo mara nyingi hufikia hapo, moyoni mwake alikuwa na wasiwasi sana, hakuwa na amani na kikao hicho. Mara tu alipoketi juu ya kitanda kikubwa na kujibwaga juuye ili kupata pumziko mara simu yake kubwa ikapokea ujumbe uliomuwacha kakodoa macho, akaitupa simu ile ukutani kwa nguvu na yeye kujitupa kitandani huku akitoa tusi la nguoni. ‘Tumekosea wapi? Na huyu jamaa anajiamini nini hata atufanye hivi?’ Don alijiuliza pasi na majibu.
§§§§§
“Mimi sio mjinga hata niuache mgodi ule uende hivihivi, kumbuka kati ya migodi inayoingiza hela kwetu ule unaongoza,” Robinson aliwaeleza watu wake wa karibu ambao alikuwa ameketi nao katika chumba cha siri ndani ya jingo lake kubwa lililobeba maofisi na mambo mbalimbali.
“Hii ni janja yangu tu na najua kuwa atanasa, na ameshahakikisha anakuja, sasa kazi kwetu jinsi ya kumwondoa na kisha tunaanza michakato mipya, kule Afrika ya Kusini tayari kuna viongozi wa serikali wanasubiri tu wasikie juu ya hili,” Robinson aliendelea kunadi sera.
“Sasa, kwani jaribio la kwanza lilishindikana vipi wakati kila kitu kilikuwa sawa na tulipeleka mtu mwenye taaluma hiyo?” Mjumbe mmoja mnene aliyekuwa akivujwa jasho mara kwa mara aliuliza swali hilo.
“Aaaaa pale tumefeli, kuna mtu katumwa kutoka Tanzania huyu ndiye mwiba katika harakati zetu, ametuharibia kwa kumuua Tracy mwaka uleeee pamoja na McField, sasa sijajua kajipeyeza vipi katika hili, viongozi wa idara za usalama pale wamekiri kutokuwa na habari na mtu huyo,” akaendelea kujibu.
Ukimya ukatawala kila mmoja akiwa anaangalia anakokujua, ‘Mkono wa Jasusi!’ mmoja wao akawaza, kisha akageuka kumtazama Robinson.
“Huyu bwana nahisi atatuharibia kila upande, kwa nini hasimalizwe?” Yule bwana akaongea huku amekunja sura.
“Tungemmaliza lakini sijajua anatuzidi vipi akili, kila tukipanga hili, yeye yupo sekunde kadhaa mbele,” Robinson akaeleza. Kikao hicho cha dharula kikaendelea kwa dakika kadhaa na kumalizika kisha kila mtu kurudi katika shughuli zake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi