NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (10)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
yaani hii inamaanisha kwamba ujana wao hawakuufaidi kwa kufanya ushenzi kama huu na ndiyo maana zama hizo zilianza kujirudi kwao.

Mimi nilitaka nifanye yote ili hata siku moja mtu akinifuata na kuniuliza kama niliwahi kufanya ushenzi huu na huu basi nimwambie nilifanya na sikuona faida yoyote ile.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Wanawake wawili ndani ya kitanda kimoja, mambo hayo niliwahi kuyaona kwa Wazungu tu lakini si huku Tanzania.

Basi nikakubaliana nao, wakaniambia niwapoze tu elfu hamsini kila mmoja, chakula na pesa ya nauli, nikawaambia poa, pesa si tatizo, tatizo ni wao tu kunipa huduma ya kitu moyo inataka.

Tukaondoka na kuelekea hotelini. Nilijiona Mfalme Mswati. Niliona hotelini mbali, wakati mwingine nilitamani hata kupiga picha na kuwaonyeshea Watanzania wote kwamba si mnaona sasa nilivyo? Si mnaona jinsi ninavyoondoka na watoto wawili?

Tulipofika hotelini tukaingia, sikutaka kuchelewa, mambo yakaanza mara moja huku nikionekana kuwa na kasi kama Hussein Bolt. Nilitaka kuwaonyeshea kwamba hela ya mwanaume haiendi bure, ilikuwa ni lazima wailipie na ndicho kilichotokea. Ilichukua masaa matatu, wote wakawa hoi.

“Wewe mtu balaa!” aliniambia Doreen huku akiniangalia kwa mshangao, pamoja na mambo yake machafu lakini alikiri kwamba hakuwahi kukutana na mimi.

“Balaa langu lipi sasa?”

“Utadhani siyo mwanaume wa Dar!” alidakia Amanda.

“Kwa hiyo mnaniambiaje? Mmeshakula laki moja yangu na huduma mliyonipa ni ya shilingi elfu sitini tu, kuna ya arobaini imebaki huko kwenu,” nilimwambia.

“We kaka utatuua!”

“Basi nawaongezeni, mimi mpaka niridhike!”

“Kwani hujaridhika tu?”

“Bado hata kidogo!” niliwaambia.

Niliongea kama masihara lakini nilimaanisha, ni masaa matatu lakini ilionekana kama nusu saa kwangu. Filimbi ikapigwa tena na wachezaji kuingia uwanjani.

Watu walikuwa wakihema kama mbwa, mpira wa siku hiyo ilikuwa balaa, viungo walikuwa wakimiliki mpira kwa kasi kubwa, kila ulipokuwa ukitoka, mpira mwingine ulirushwa ndani kuonyesha kwamba siku hiyo ilikuwa ni ya kazi tu, wachezaji wasiokuwa na uwezo wa kumaliza dakika tisini hawakutakiwa kucheza mechi hiyo.

Nakumbuka tuliingia majira ya saa kumi jioni na waliondoka pale saa tano usiku, niliwang’ang’aniza walale, wakakataa kabisa.

“Nitawapeni milioni moja kila mtu!”

“Hapana! Hata ukinipa milioni hamsini silali! Mwanaume gani hutosheki!” aliniambia Doreen.

“Jamaniiiiiiii....”

“Aku! Tena usiniguse,” aliniambia Doreen manake alishaona mkono wangu ulianza kumletea shobo.

Nikaachana nao, wakaondoka na mimi kulala hotelini. Asubuhi ilipofika, baba yake na Zamaradi akaniambia kwamba siku hiyo ndiyo walitaka kuhama hivyo nilitakiwa kuonana naye.

Halikuwa tatizo, tukaonana, tukaongea na siku hiyo kuhama na hivyo kuanza kuirekebisha nyumba ile kwa kuvunja baadhi ya sehemu na kuboresha sehemu nyingine kuwa na mvuto zaidi.

Nilikuwa na pesa, niliitengeneza kwa wiki moja tu, ikawa nzuri mno kiasi kwamba kila mtu aliyekuwa akiiangalia aliipenda kupita kawaida kutokana na mapambo yake yaliyokuwa kwa nje.

Kwa ndani niliamua kufanya kufuru, nilitaka nipafanye kuvutie, yaani msichana yeyote ambaye angeingia basi awe anatamani tu kuolewa na mimi ili aishi humo.

Ilitumia siku kadhaa kila kitu kikakamilika. Nilichokuwa nikihitaji nilikipata, nilichokifanya kingine ni kununua coaster tatu ambazo zilianza kufanya biashara, nikanunua bajaj tano, bodaboda ishirini lakini pia nikaamua kuwekeza zaidi kwenye kilimo ambapo nilisafiri mpaka Mbeya na kununua shamba la hekari ishirini na hivyo kuanza kupanda mpunga.

Haikuishia hapo bali kingine nilichokifanya ni kuwekeza kwenye ardhi, nikajenga nyumba nyingine mbili na kuzipangisha kwa pesa ndefu, ndani niliwawekea kila kitu na malipo yake nilihitaji yafanyike kwa dola kwani niliweka mazingira fulani kama nyumba za Wazungu ambao ndiyo walikuwa lengo langu kuwapata ndani ya nyumba hizo mbili kubwa.

Kwa kila mwezi, kodi yake ilikuwa ni dola elfu moja, zaidi ya milioni mbili na nilianza kupata wateja wengi hasa Wazungu waliokuwa wakija huku kwa mambo yao ya utalii kwa kuwa kiasi hicho kwao kilikuwa kidogo mno. Ndiyo hivyo nikawa naingiza pesa.

“Hii nyumba itajaa dhambi sana! Yaani humu, hata mke wa mbunge akijipindua, tutalaumiana,” nilisema huku nikiwa kitandani.

Watu wa kwanza walionijia kichwani ni Halima na Shamila, sasa zake na Issa, nianze nao halafu niende kwa huyo demu wake, hata kama alikuwa amemuoa, kwanza ilikuwa ni lazima nifanye yangu.

Mafundi walianza kujenga nyumba yangu ambayo nilihitaji kwenda kuishi Tegeta. Nilikuwa na furaha tele, kwa jinsi nilivyokuwa nikiwaangalia mafundi walivyokuwa wakiijenga nyumba hiyo, sikuamini kama kweli ilikuwa ni mimi ndiye niliyewaambia wafanye hivyo.

Nilikaa pembeni huku nikifuatilia kila kitu. Nilihitaji nyumba kubwa na ya maana ambayo ndani yake kungekuwa na bwawa la kuogelea. Kwa kipindi chote hicho sikuwa nimeonana na Nurat, ilikuwa kama wiki moja hivi, tulikuwa tukiwasiliana kwenye simu tu.

Kipindi hicho nilitaka niende Kariakoo kuonana na dada zake, Issa na kuzungumza nao. Nilikuwa na ratiba yao, nilijua kabisa kwamba siku hiyo kama ningekwenda huko ningemkuta Halima na hivyo kumfanyia kile nilichotaka kufanya. Nikaondoka kwa gari langu, IST ambayo niliinunua milioni kumi na mbili showroom.

Nilipofika Kariakoo, nikaenda katika eneo ambalo lilitumika kuegeshea magari karibu kabisa na Big Bon, nikaliacha na kuelekea katika Mtaa wa Kongo kwenda kuonana na Halima.

Nilipofika, kweli nilimkuta, alishtuka sana kuniona, nilibadilika, niliondoka kwa wiki kadhaa na aliniona kama mpya. Akanisogelea, hakuamini alichokiona, yule Edward aliyekuwa amepotea kwa kipindi kirefu hakuwa huyu, nilikuwa mwingine kabisa.

Pale hakuwa peke yake, kulikuwa na msichana mwingine mzuri ambaye sikumjua, alionekana kutabasamu na kuwa na shauku ya kutaka kufahamu nilikuwa nani na kwa nini Halima alikuwa akinichangamkia kiasi hicho.

Wakati nikiwa sijajiandaa hata kumwambia lolote lile, washikaji zangu ambao nilikuwa nikilinda nao na wale walionijua wakanisogelea na kuanza kunisalimia, walinishangaa mno, nilibadilika na kuwa kama mtu fulani ambaye nilikuwa na pesa.

“Edward! Hivi ni wewe ama naota?” aliuliza jamaa mmoja aliyeitwa Fred.

“Ni mimi. Inakuwaje Fred!”

“Poa! Umebadilika, mzee baba mpaka unaanza kuota kitambi,” aliniambia na kuanza kucheka.

Kila mmoja alihitaji kufahamu ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka kuwa hivyo nilivyokuwa. Niliwaambia kwamba ni bahati tu, ilitokea nikajikuta kuwa na pesa basi nikabadilisha maisha yangu.

Kila aliyeniona hakuacha kunishangaa, Halima na yule msichana mwingine walikuwa wakiniangalia kwa macho ya kunitamani tu, yaani kama walionekana kuhitaji kitu fulani hivi.

Nilikuwa bize na washikaji, tulipiga sana stori, tulipomaliza, wakaondoka na kuniacha na wanawake hao.

“Umebadilika,” aliniambia Halima, pamoja na mapozi yake aliyokuwa akiniletea siku za nyuma, siku hiyo yalikwisha kabisa.

“Nimekuwaje? Nina mkia?” nilimuuliza kiutani.

“Hahah! Umekuwa m’baba! Aisee umependeza,” aliniambia.

Japokuwa nilikwenda hapo kwa lengo la kumpata Halima lakini yule msichana ambaye naye alikuwa mahali hapo aliniacha hoi sana. Alikuwa mrembo na nilichokifanya ni kutoleta tamaa zangu kwake kwani niliamini ningemkosa Halima na wakati alikuwa kwenye mipango yangu.

“Na huyu ni nani?” nilimuuliza Halima kuhusu msichana huyo.

“Huyu anaitwa Haijati. Ni wifi yangu kwa Issa, mtoto wa Zenji,” alinijibu Halima.

Yaani moyo ukapiga paaa! Sikuamini kile nilichokisikia. Halima aliniambia kwamba huyo alikuwa mke wa Issa, aliamua kumuoa siku chache baada ya mimi kuondoka.

Aisee nilichanganyikiwa, yaani kwa uzuri wa yule demu, namuachaje sasa? Kwa sababu alisikia juu juu tu, nikaamua kuanza kujifagilia kwanza kwani nilijua ingeweza kuwa njia nyepesi mno kumpata.

“Halima! Mtaa wa Kongo haujabadilika imenifanya mpaka gari langu nilipaki kule Big Bon,” nilimwambia, Halima akashtuka mno.

“Una gari?”

“Sasa unanichukuliaje Halima? Namshukuru Mungu kanijalia vijisenti kidogo! Nimenunua nyumba Sinza na ninajenga Tegeta,” nilimwambia Halima.

Hakuamini, kile alichokisikia kilikuwa kama ndoto. Kilikuwa ni kipindi kifupi sana kwa mimi kuwa na pesa hizo, nilizipata wapi? Uchawi ama?

“Imekuwaje?”

“Ni stori ndefu sana. Si pesa za kishetani, ni za halali kabisa. Yaani Mungu amenibariki mno. Umekula?” nilimuuliza.

“Sijala!”

“Utakula nini?”

“Chochote tu bosi!”

“Na shemeji hapo?” nilimuuliza Haijati huku nikimwangalia.

“Chochote tu!”

“Basi sawa.”

Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu kumi na kumwambia aende akanunue chakula chao. Akaichukua, akaondoka na kutuacha wawili sisi pale dukani.

Hilo ndilo nililolitaka, nilihitaji kuzungumza naye kwa dakika kadhaa, ikiwezekana hata nichukue namba yake ya simu kwa ajili ya kuitumia baadaye.

Mume wake aliutumia udhaifu wangu wa kutokuwa na pesa kumchukua msichana niliyempenda na kufanya naye mapenzi, hii ilikuwa zamu yake, hata kama alikuwa ameoa, moyo wangu ulikuwa na kisasi na nilitamani sana na yeye nimfanyie kama alivyonifanyia, mwenye pesa, muumize masikini tu.

“Ila umependeza shemeji!” nilimwambia huku nikimwangalia kwa macho ya kuita.

“Mh! Ahsante shemeji!”

“Hivi Issa yupo?” nilimuuliza.

“Yupo! Kwani huwasiliano naye?”

“Hapana! Katika maisha yangu niliwahi kuongea naye mara mbili tu. Huwa ninamjua sana huyu Halima, yeye hatukuwahi kuongea sana,” nilimwambia Haijati, ilikuwa ni lazima nimkatae Issa kwani nilikuwa na mipango mizito sana kwa huyu mke wake.

Sikutaka kuchelewa, kazi yangu muda huo ilikuwa ni kumsifia tu, niliujua udhaifu wa wanawake, unapoamua kuwasifia, mara kumuaminisha kwamba alikuwa na mzigo mkubwa kwa nyuma, alifungashia, alikuwa na kifua kizuri, macho ya goroli, uzuri wa Beyonce, niliamini kwamba ingekuwa rahisi kumpata msichana wa hivyo.

Basi ikawa hivyo. Nilimsifia sana na kumwaminisha kwamba alikuwa mzuri kuliko wanawake wote. Mwenyewe akawa anafurahi tu, akatabasamu kana kwamba nilichokiongea kilikuwa kweli.

“Umeumbika sana Haijati, u mwanamke mrembo sana,” nilimwambia kwa sauti ya taratibu.

“Mh! Asante.”

“Yaani kama ningekuwa na mwanamke kama wewe, hata kazini siendi,” nilimwambia.

“Hahah! Kwa nini sasa?”

“Unataka baba mwenye nyumba aniibie! Ningekuwa nawe muda wote ule, yaani ningehakikisha hata nikienda chooni natangulizana na wewe. Haijati u mzuri mno, unajua kupendeza, ngozi yako inang’aa sana, huo uzuri, kweli wewe ni mwanamke wa Kizanzibari,” nilimwambia.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni