
Mtunzi: Nyemo Chilongani
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Nilimuuliza kuhusu msichana yule, akaanza kunizungusha, hakutaka kuniambia ukweli.
Yeye ni Mchaga, nilijua udhaifu wake, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu kumi na kumuwekea karibu na kidirisha cha duka lake.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
“Niambie kidogo kuhusu yeye, halafu hii utakunywa soda,” nilimwambia huku nikimuonyeshea ile pesa. Ile kuiona tu, macho yakamtoka.
“Unamzungumzia msichana yupi?” aliniuliza.
“Yule aliyeingia nyumba hiyo nyekundu,” nilimjibu.
“Humo kuna wasichana watawili halafu mapacha, wewe unamzungumzia Doto au Kulwa?” aliniuliza.
“Mapacha?”
“Ndiyo!”
“Sasa kama mapacha hapo nitasema namzungumzia yupi? Wote watakuwa wanafanana...ila niambie wanaitwa nani!” nilimwambia.
“Mkubwa anaitwa Glory na mdogo anaitwa Esta.”
“Oh! Ahsante! Wanasoma?”
“Wa Ardhi yupi?”
“Esta!”
“Sawa.”
Nikampa ile elfu kumi, kwangu pesa haikuwa tatizo, nilichokuwa nikihitaji ni kumpata msichana niliyekuwa nimemfuata. Yaani kipindi hicho sikukumbuka kabisa kuhusu Halima, nilikuwa bize na huyu msichana niliyekuwa nimemfuatilia.
Nilipofika getini nikaanza kugonga hodi bila kuogopa kitu chochote kile. Niligonga kwa sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na msichana mmoja mdogo, alifanana na yule aliyeingia, bila shaka alikuwa mdogo wake.
“Shikamoo!” aliniamkia.
“Marahaba! Esta yupo?” nilimuuliza.
“Ndiyo yupo.”
“Naomba uniitie!”
“Ingia...” aliniambia, nikazama ndani.
Kwa jinsi alivyoniambia niingie ilionekana kuwa rahisi sana, wala sikuogopa, nilihisi kwamba hakukuwa na mtu, nilipozama tu, macho yangu yakatua kwa wazee wawili, nahisi walikuwa wazazi wao, walikaa kibarazani kwenye viti wakipunga upepo, nilipoingia tu, wakayapeleka macho kwangu na kuniangalia.
Nilishtuka mno, kijasho chembamba kikaanza kunitoka, nilitamani kukimbia lakini nilishindwa kabisa. Mzee huyo alikuwa akiniangalia huku akionekana kuhitaji kufahamu ni kitu gani nilikuwa nakihitaji nyumbani hapo.
Nikapiga moyo konde, nikawasogelea, nikawasalimia kwa heshima kubwa na kuwaambia kwamba nilikuja kumuona Esta.
“Wewe ni nani?” aliniuliza.
“Nasoma naye!”
“Unasoma naye wapi?”
“Ardhi!”
“Unamjua Esta?” aliniuliza kwa ukali kidogo.
“Namjua!”
“Sawa. Stela! Kawaite dada zako,” alisema mzee yule.
Tayari nilijua kulikuwa na balaa hapo, yule mtoto akaingia ndani kwenda kuwaita. Nilibaki pale nje na wazazi wao huku nikiwa na hofu mno ila uso wangu ulikuwa kwenye tabasamu pana.
Baada ya dakika moja, yule mtoto akarudi na hao dada zake, nilipowaangalia moyo ukapiga paa. Yaani kama duniani kulikuwa na mapacha waliokuwa wanafanana basi hawa walikuwa balaa. Walifanana, walikuwa wazuri kiasi kwamba nilichanganyikiwa.
Kilichotokea sasa, sikujua yule msichana ambaye nilikutana naye nje alikuwa yupi kwani hata nguo alikuwa amebadilisha. Niliwaangalia kwa makini lakini sikumgundua kabisa, nikabaki nikishangaa.
“Aya mchukue huyo Esta uongee naye, si umesema unasoma naye,” aliniambia yule mzee kwa sauti ya kutaka kunikomoa, mtu mzima nikaloa, halafu watu wenyewe nilivyokuwa nikiwaangalia, wote walikuwa wakinishangaa.
Yaani ghafla nilitamani tu ardhi ipasuke nitumbukie ndani, au niwe mchawi, nipotee na nitokezee nyumbani kwangu kwani hata huyo Esta sikumjua ni yupi kati ya wale wawili waliosimama mbele yangu.
Niliwaangalia kwa makini sana, wasichana hawa wawili walifanana kupita kawaida, kila mmoja alikuwa na kidoti na kila kitu katika mwili wao vilikuwa vikifanana.
Nilishindwa kuelewa yule Esta alikuwa yupi kati ya wale wawili waliosimama mbele yangu. Niliwaangalia kwa sekunde kadhaa na mmoja kati yao kutoa tabasamu la ghafla, nikaamini kama huyo ndiye alikuwa Esta.
“Huyo hapo!” nilimwambia mzee yule na kumuonyeshea mmoja wa mabinti zake, wakaangaliana na mkewe na kutoa tabasamu.
Sikuwahi kuonana nao hata kidogo, waliniruhusu kuzungumza naye na kuingia sebuleni, hawakunihofia kwa sababu walijua kwamba endapo ningekuwa mtu mbaya basi nisingeweza kwenda nyumbani pale kwa kujiamini kiasi kile.
Tukaingia sebuleni na Esta na kuanza kuzungumza naye, yule pacha mwenzake akaelekea chumbani. Esta alinichangamkia mno kiasi kwamba mpaka nikabaki nashangaa kwani kule nje alininyamazia ila humu ndani alikuwa muongeaji mno.
“Unajua mimi sikufahamu kabisa, ndiyo kwanza nakuona leo,” aliniambia.
“Najua! Mwanzo nilitamani sana kuongea nawe ila ukaninyamazia, kwa sababu nilitokea kukupenda, nikaamua kuja mpaka ndani,” nilimwambia huku nikimwangalia.
Alionekana kufurahi mno, tuliongea kwa dakika kama ishirini hivi, tukabadilishana namba za simu na kuwaaga nyumbani pale na kunisindikiza mpaka barabarani.
Muda wote huo Halima alikuwa akinipigia simu, sikutaka kupokea kwani niliamini ningeharibu kila kitu. Esta alipoondoka tu, nikachukua pikipiki na kurudi nyumbani.
“Mbona hukuwa unapokea simu zangu?” aliniuliza Halima mara baada ya kumpigia.
“Aiseee wewe acha, nimefanya ujinga mmoja mkubwa sana,” nilimwambia.
“Ujinga gani?”
“Nilikwenda kununua vinywaji, halafu simu nikasahau nyumbani. Upo wapi?” nilisema na kumuuliza.
Aliniambia alipofika na kumfuata huko. Siku hiyo alivyovaa aliniacha hoi sana. Alivalia juba jeusi lakini lile la kishetani zaidi, yaani namaanisha lililokuwa likionyesha maungo yake ya ndani na kuona kila kitu.
Nahisi alivaa kama kunitega kwani mpaka michoro ya nguo yake ya ndani nilikuwa nikiiona kitu kilichonifanya kugundua kwamba shetani alikuwa na nguvu sana kwani yale mavazi ya heshima ambayo kwa kila aliyoyavaa ulimuona mtu mwema yalibadilishwa na kuwekewa manjonjo ilimradi tu mwanaume akiyaona basi asisimke mwili, tena yalimbana kiasi cha kuyachora maungo yake.
“Leo ni vita,” nilijisemea moyoni huku nikiangalia wezere zake zilivyokuwa zikipishana.
Baada ya dakika kadhaa tukafika nyumbani. Niliibadilisha kwa kiasi kikubwa sana, ilikuwa kama nyumba ya bilionea fulani kumbe alikuwa akiishi mzushi kama nilivyokuwa.
Sebuleni hapo tukapiga sana stori, aliniambia mambo mengi, akajichekesha wee lakini nikasema wewe cheka tu, tabasamu lakini mwisho wa siku safari yako inaishia katika mlango ule paleeee.
“Ila Mungu ameyabadilisha maisha yako, yaani si kama ulivyokuwa,” aliniambia huku akiiangalia ile nyumba.
Muda wote huo kichwa changu kilikuwa kikipiga hesabu kubwa kuhakikisha namuondoa pale kwenye kochi na kumpeleka ndani, tulizungumza lakini baada ya dakika chache, nikamsogelea na kumwangalia lile jicho la nipe nikupe.
“Una kinywaji gani?” aliniuliza.
“Kuna kila kitu, wewe unataka nini?” nilimuuliza.
“Nahitahi yogurt,” aliniambia.
Kiukweli sikuwa nayo, nilimwangalia, ni kweli alihitaji yogurt, nikahisi kuna kitu kwani isingekuwa rahisi mgeni kuja na kuomba yogat. Kwa sababu zilikuwa zikipatikana madukani nikamwambia anisubiri na mimi kwenda huko.
Nilikuwa na haraka, yaani kama ungeniona jinsi nilivyokuwa natembea kwa kasi kuelekea dukani ungesema muda wowote ule ningeanguka. Nilipofika, nikanunua na kuanza kurudi nyumbani. Nilipoingia tu, nikamkuta amebaki na khanga tu.
Hapo ndipo nikapata jibu juu ya kwa nini aliniambia anahitaji kitu ambacho hakikuwepo humo ndani, nilimwangalia, nilisimama huku kama nimepigwa na shoti ya umeme, sikutaka kujua alihitaji nini hapo, haraka sana nikaweka yogurt mezani na kumsogelea.
Nilipofikia tu, yakatokea mambo machafu kidogo, nikambeba na kumpeleka chumbani kisha kumuweka kwenye kitanda na kurudi sebuleni. Pale sebuleni nikafungua friji na kutoa barafu ambalo nikalipasuapasua na kuchukua kipande kikubwa na kukiweka mdomoni na kurudi chumbani.
Nilipofika, nikaitoa ile khanga na kuanza kushughulika na mwili wake kwa kuweka mdomo wangu kila kona huku nikiugusa kwa kutumia kile kipande cha barafu kilichokuwa mdomoni mwangu.
Nilimsikia akibadilika kabisa, alikuwa mweupe lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele niliyaona mabadiliko kabisa, mwili wake ulikuwa unaelekea kwenye wekundu na sikutaka kumuacha kabisa.
Alilalamika, si kwa maumivu bali kwa raha aliyokuwa akiisikia. Kile kipande cha barafu kilikuwa na nguvu ambayo sikuitegemea kabla, ulikuwa ni kauchawi ambacho si watu wengi sana walikuwa wakiujua.
Niliufanya utundu huo mpaka kipande kile cha barafu kilipokwisha, sikuridhika, nikakichukua kingine na kuendelea. Nilihitaji kumaliza kila kitu ndani ya dakika chache, faragha, kutumia muda mrefu si sifa bali unaweza kutumia muda dakika ishirini tu lakini utalii wako ukawa mkubwa kuliko hata yule ambaye angetumia masaa mawili.
Sihitaji kukuandikia yote hapa, ila kwa kifupi jua nilifanikiwa kwa asilimia mia moja kiasi kwamba akahitaji kulala hapohapo. Sikuhitaji hilo, kwenye kitu ambacho siwezi kufanya ni kulala na mwanamke, hasa katika nyumba kama hiyo.
Kama ningelala naye, nilijua kabisa baadaye Esta angeanza kunisumbua, sikutaka ajue kama nilikuwa na mtu, nilihitaji kumuonyeshea kwamba nipo singo na ndiyo maana usiku nilihitaji kuwa huru kabisa.
Basi baada ya kumaliza kila kitu, tukaelekea bafuni, tukaoga na kutoka. Hakunimaliza, kila aliponiangalia, nilijua alikuwa akijiuliza ni kwa kiasi gani nilikuwa nayafahamu hayo yote!
“Barafuuuu...” aliniambia huku akiniangalia.
“Unamaanisha nini?”
“Umejifunza wapi? Sikuwahi kufanyiwa kitu kama hiki, na sikuwahi kufikiria maishani mwangu,” aliniambia.
“Hahaha! Kawaida tu, kuna siku ukija, nitakupaka asali,” nilimwambia.
“Unipake asali?”
“Ndiyo!”
“Kwa nini?”
“Nataka niilambe mpaka yote iishe mwilini mwako,” nilimwambia, nilimwangalia, niliona jinsi alivyosisimka.
“Mh!”
“Ila si kwa leo, usijali, kuna mambo mengi sana yatakuja,” nilimwambia huku nikimwangalia usoni.
Tulizungumza mambo mengi sana na baada ya dakika kadhaa tangu atoke kuoga akavaa na kuondoka zake. Nilimsindikiza kwa gari mpaka karibu na nyumba yao na kurudi zangu.
Moyo wangu uliridhika sana, nililala na mke wa Issa, haikuisia hapo, nikalala na mdogo wake. Kutembea na demu wangu lilikuwa jambo dogo sana, unaweza kuona hivyo lakini moyoni mwangu lilikuwa kubwa mno kiasi kwamba sikuwa radhi kuvumilia.
Usiku wa siku hiyo nikaanza kuchati na Esta. Nilitokea kumpenda, nilikumbuka kwa jinsi alivyokuwa mzuri, alivyopendeza na hata kutembea kwa maringo.
Kwenye chatting zangu nilikuwa noma, nilijua kucheza na maneno, nilijua kumsoma mtu kwa kutumia maneno yangu matamu kabisa. Nilimchangamsha mni, nilitaka ajisikie vizuri kabisa na aone katika dunia hii hakukuwa na mtu aliyekuwa akimpenda kama nilivyokuwa mimi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi