NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (12)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Nikamtoa nguo zote mwilini na kwenda kwenye kabati, nikachukua pingu ya faragha na vifaa vingine na kurudi. Alibaki akinishangaa, hakujua kazi yake kwa sababu si Watanzania wengi wanatumia vitu kama hivi. Kwanza, nikamfunga pingu na kumwambia kwamba siku hiyo ilikuwa ni ya kipekee sana.

Yaliyotokea hapo, si vizuri kuyaandika hapa ila kwa kifupi ni kwamba Haijati alimsaliti mumewe,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
nilimchukua mke wa Issa pasipo mwenyewe kugundua kitu chochote kile. Nakumbuka tulichukua saa mbili kitandani ndipo tukaenda kuoga, na huko napo, tukarudia kidogo na kuelekea chumbani kuvaa.

Aliniangalia, hakuamini kilichotokea, hakutarajia kukutana na harakati za kigaidi kama zile alizokutana nazo. Nilimwangalia kwa macho ya kutaka kusikia kitu chochote kile kutoka kwake kwani niliamini kwa jinsi moto ule nilivyouwasha, asingeweza kukaa kimya hata kidogo.

“Kamwili kadogoooooo...” aliniambia huku akiniangalia, nikaanza kukenua.

“Lakini.........”

“Kanajua mambo! Yaani pamoja na ujanja wangu...sijawahi kukutana na mtu kama wewe. Umejifunza wapi?” aliniuliza huku akianza kuvaa taiti yake ya ndani kabla ya kupiga dela lake.

“Hahah! Kwani hivi tunajifunzia sehemu?” nilimuuliza.

“Si kawaida kabisa. Yaani pale uliponifunga zile pingu zako mikononi na miguuni, haki ya Mungu ungeniua...yaani nilihisi kabisa mtoa roho alikuwa akinifuata,” aliniambia.

Nikacheka mno, hilo nililijua, nilikuwa mzoefu wa kupata stori kuhusu zile pingu. Kwa mara ya kwanza nilipoambiwa, jamaa alisema kuwa unaweza hata kutaka kumuua mtu kwani inakuwa ni mara tano ya ile hali anayoisikia kikawaida.

Siku hiyo niliamini, na nilipokumbuka jinsi alivyokuwa akikileta kifua chake juu na kushuka chini, niliamini kabisa ningeweza kumuua. Haijati akachanganyikiwa, aliniambia kabisa kwamba angemsaliti mume wake kwangu katika maisha yake yote, na hata kama ingetokea siku nimeoa, bado angehitaji kupata nafasi ya kuwa nami.

“Sawa. Wewe tu,” nilimwambia.

Baada ya dakika kadhaa tukatoka na kumsindikiza mpaka Tabata Bima na mimi kurudi zangu. Nilifurahi sana, unajua unapokuwa na adui yako halafu unafanya kitu ambacho unaamini kabisa kwamba kama ingetokea siku akajua, ataumia sana, basi ungefurahi mno.

Niliporudi nyumbani, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuwasiliana na Halima, nilihitaji kumseti kwanza kwa sababu ni zamu yake ndiyo iliyokuwa ikifuata. Nikaanza kuchati naye mpaka majira ya saa tano usiku, alilegea kwa sababu alijua kwamba nina pesa, basi kila kitu nilichokuwa nikiongea, alikuwa akichekacheka tu.

“Ila nilikumisi,” aliniambia bila aibu, eti alinimisi, nilikuwa kapuku, alinimisi kwa lipi? Ila kwa sababu na mimi nilikuwa nahitaji kitu kutoka kwake, nikaunganisha.

“Hata mimi! Nimekuwa nikiota ila siku kuhisi wewe. U msichana wa ajabu sana,” nilimwambia.

“Kweli?”

“Yaah! Nikuulize swali?”

“Niulize!”

“Hivi umevaa ya rangi gani hapo?” nilimuuliza.

“Nini?”

“Acha utoto bwana!” nilisema na kuanza kucheka kile kicheko cha chini.

Alikuwa mtu mzima, alijua kabisa kile nilichomaanisha ila mwenyewe akaanza kujifanya kama mtu anayesikia aibu kubwa. Akaanza kujiumauma ila mwisho wa siku akaniambia mwenyewe.

“Rangi ya pinki!”

“Oh! Daah! Natamani sana siku nione jinsi inavyokupendeza. Unavaa kiuno namba ngapi?” nilimuuliza.

“Mh! Wala sijui! Mi nanunuaga tu! Kwa nini umeuliza?” aliniuliza.

“Nataka nikununulie kadhaa, tena nikuvalishe mimi mwenyewe,” nilimwambia kwa sauti fulani hivi ya kimitego.

“Mh! Utanichungulia!” aliniambia.

“Nitafumba macho! Kweli sitoona,” nilimwambia.

Kwenye maongezi kama haya ndipo unapogundua kuwa mwanaume raha sana. Yaani unaanza kuona mwili wako ukianza kupata hali fulani na sehemu moja kuanza kukakamaa.

Sauti yake ilibadilika kabisa, yaani nilijua alianza kuingia kwenye ulimwengu fulani hivi, na mimi ninavyopenda sifa, tena ninavyojua kuitumia sauti yangu vizuri, basi ndiyo nikaongeza na kuongea.

“Edward...” aliniita, tena kwa sauti kuonyesha kwamba alichanganyikiwa.

“Nipo hapa mpenzi!”

“Hivi ushawahi kufanya kwa kutumia simu?” aliniuliza.

Kwanza kabla ya kujibu nikanyamaza, nikaanza kujifikiria mambo mengi, swali lake lilikuwa na mitego mingi, kama ningemwambia nimeshawahi kufanya basi angegundua kama mimi nilikuwa malaya tu, na kama ningemwambia kwamba sijawahi kufanya basi angeniona boya.

Kiukweli niliwahi kufanya zamani sana wakati nasoma, kipindi hicho unajiunga na tigo saa sita usiku na kupewa dakika ishirini na tano. Kipindi hicho ndicho nilichofanya sana kwa kutumia sauti, tena nilikuwa mtu hatari.

Nilizungumza kwa hisia, nilimtega, niliongea maneno ambayo yalimfanya msichana yeyote yule achanganyikiwe na mwisho wa siku kuniambia alitaka kwenda kuoga kwani alichafuka kana kwamba alitoka kucheza mpira.

Hako kaswali kake kamoja tu kakanifanya nikumbuke mademu wengi wa kipindi kile shule, hasa Fatuma ambaye kwangu ndiye alikuwa mtu dhaifu sana.

“Edward ongezaaaa....” niliyakumbuka maneno yake hayo, yaani tulikuwa tukiongea kwenye simu lakini alichanganyikiwa.

Hakuwa huyo tu, walikuwa wengi, tatizo la Fatuma ni kwamba aliwaambia marafiki zake ambao nao walijilengesha na mimi sikutaka kuonekana mshamba, walihitaji pipi ya kijiti, mimi nikawapa ice cream wanyonye kabisa.

“Sijawahi kufanya kwa simu, huwa sipendi,” nilimjibu kabisa.

“Sawa.”

Nilijua, alichanganyikiwa mno lakini hakuwa na la kufanya. Sikutaka kuendekeza mchezo wa kufanya kwa simu kwa sababu nilikuwa nimekua, sikuwa mtoto kama kipindi kile shuleni.

Nilimwambia Halima kwamba nilitaka kuonana naye hivyo ingekuwa vizuri sana kama kesho ndiyo ningeonana naye. Akakubali na hivyo kuniambia nijipange kwani yeye alikuwa mtu hatari sana.

Nikacheka sana, mimi huwa siamini kama kuna mwanamke anakuwa hatari kama mwanaume, na kama yeye alitamba sana kwamba alikuwa hatari, nilitakiwa kumuachia nione ukali wake ulikuwa wapi.

Nawajua watoto wa kike, huwa hawana pumzi za kutosha. Wapo hivyo, tena wote duniani. Katika kipindi cha dakika kumi za mwanzo, wanaanza kucheza kwa kasi sana ila baada ya hapo pumzi inakata na kukwambia nimechoka. Hapo ndipo zamu yako inapokuja na kumwambia kwamba hutakiwi kuchoka, humu hujaja kulala, umekuja kufanya kazi tu.

“Hivi una pumzi kweli?” niliamua kumuuliza kwa meseji.

“Kwa nini umeniuliza hivyo?”

“Ninataka kujua. Una pumzi?” nilimuuliza.

“Utaona kesho. Nataka kukuonyesha kwamba kungwi wangu hakufanya kazi ya bure,” aliniandikia.

Huwa sinaga presha kabisa, baada ya kuniambia hivyo, nikachukua cd yangu ya Kamasutra na kuanza kuangalia, unajua alinitisha sana, nilihisi kwamba alikuwa mtu hatari.

Nilichukua mafunzo kabisa, sikutaka kupitwa na chochote kile, baada ya kumaliza kutazama, nikanywa maziwa na karanga nyingi nikijiandaa kwa ajili ya siku inayofuata.

Kweli bwana, siku hiyo ilipofika, Halima mwenyewe akanipigia simu na kuniambia nipange tuonanie wapi. Sijui alikuwa akinitega! Nina kwangu, nimenunua nyumba, inakuwaje twende kwenye nyumba ya wageni? Aje humuhumu, kwanza ndipo kwenye vifaa vyangu.

“Njoo kwangu!” nilimwambia.”

“Kwako?”

“Yaap! Wewe njoo, usiogope, timu nzuri inacheza uwanja wowote ule,” nilimwambia.

“Sawa! Ngoja nijiandae.”

Hii ni kwa wanaume wote. Kitu cha msingi ni kutafuta pesa. Achana na kunyanyua vyuma, haisaidii hata kidogo, utaonekana kama mlinzi tu lakini pesa ndiyo kila kitu.

Wanawake wanapenda pesa, wanapenda kutunzwa, wanapenda kununuliwa zawadi za kila aina na ndiyo maana kwa mtu kama Halima hakuwa akinisumbua hata kidogo kwa kuwa alijua kabisa nilikuwa na pesa.

Nikafungua friji na kuangalia vinywaji, vilikuwa vimepungua sana na hivyo nilitakiwa kuongeza kidogo. Nikatoka na kwenda kwenye duka moja la vinywaji lililokuwa Sinza Kijiweni.

Nilipofika hapo, macho yangu yakatua kwa msichana mmoja hivi, alikuwa mdogomdogo tu, alibana nywele zake kwa nyumba na kuvaa kisketi fulani kilichokwenda mpaka juu ya magoti yake kidogo.

Alikuwa mzuri, pembeni ya pua yake kulikuwa na kidoti. Wanaume walikuwa wakimwangalia, si kwamba alifungashia, bali ule uzuri wake ilikuwa ni balaa. Nililiacha gari nyumbani, hapo nilikwenda kwa bodaboda kwa kuwa hakukuwa mbali kabisa.

Nilimwangalia, nikasema haiwezekani, nikaanza kumfuata kwa nyuma, sikuona aibu yoyote ile, watu walikuwa wakimwangalia lakini nilijiamini mno.

“Hey Miss...” nilimuita lakini hakugeuka, aliendelea kwenda mbele huku akiwa na mfuko uliokuwa na boksi la soda.

Nikamfuata kwa kasi kidogo, nilipomkaribia, nikamshika mkono. Najua hakupenda lakini hakuwa na jinsi, akautoa mkono wake, akageuka na kuniangalia huku akionekana kuwa na hasira na mimi.

“Niache huko,” aliniambia huku akiniangalia.

“Samahani dada!" nilimwambia. Akageuka na kuendelea na safari.

“Unakuwa mkali sana, kwa nini? Au kwa sababu hunifahamu?” nilimwambia huku tukipiga hatua.

Hakunijibu, alikuwa kimya kama bubu na alivimba mno. Sikutaka kukata tamaa, niliwajua mademu, huonekana wagumu wakati mwingine kwa kuwa wanahitaji lugha fulani tamu, si ile ya kuonekana mhuni.

“Najua hunijui! Najua unaniona mtu wa ajabu kabisa, ila naomba nikwambie kitu kimoja,” nilimwambia kwa sauti ya chini. Hakujibu.

“Umependeza sana, yaani kama Tiwa Savage,” nilimwambia. Akabaki kimya tu.

“Jamani! Yaani pamoja na kukusifia hata asante! Niambie ahsante tu niridhike nirudi,” nilimwambia. Akabaki kimya.

“Miss! Naomba niambie niridhike nirudi, sihitaji kukupotezea muda wako,” nilimwambia kwa sauti ya chini lakini bado hakutaka kuzunguma lolote lile.

Baada ya muda fulani akafika kwenye nyumba moja na kufungua geti na kuingia ndani. Mtu mzima nikabaki nje, sikujua ni kitu gani nilitakiwa kufanya.

Nikaanza kujiuliza kama ilikuwa ni sahihi kuondoka ama kubaki hapohapo. Kiukweli yule msichana nilimpenda kwa kuwa alikuwa na sura nzuri, nilijisemea kwamba endapo ningeondoka basi ningemkosa, ili kuonyesha kwamba nilihitaji sana kuzungumza naye, nilisubiri kama dakika tano hivi, nikapanga kupiga hodi kumuulizia.

“Mh! Subiri kwanza,” nilisema.

Kwa wanawake kupo hivi, endapo tu ungeanza kuzungumza naye kwa kumtaja jina lake basi ungefanikiwa kumpata, kitu cha kwanza angekuwa anajiuliza umemjuaje, hiyo ingekuwa nafasi kwako kuanza kumchambua kama karanga.

Pembeni kulikuwa na duka, nikalisogelea, nikamuona mshikaji fulani akiuza, kwa kumwangalia tu nilijua kwamba alikuwa Mchaga, hivyo nikaanza kuongea naye. Nilimuuliza kuhusu msichana yule, akaanza kunizungusha, hakutaka kuniambia ukweli.

Yeye ni Mchaga, nilijua udhaifu wake, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu kumi na kumuwekea karibu na kidirisha cha duka lake.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni