NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (13)

Zephiline F Ezekiel
NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (13)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... Nilimuuliza kuhusu msichana yule, akaanza kunizungusha, hakutaka kuniambia ukweli. Yeye ni Mchaga , nilijua udhaifu wake, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu kumi na kumuwekea karibu na kidirisha cha duka lake. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Niambie kidogo kuhusu yeye, halafu hii utakunywa soda,” nilimwambia huku nikimuonyeshea ile pesa. Ile kuiona tu, macho yakamtoka. “Unamzungumzia msichana yupi?” aliniuliza. “Yule aliyeingia nyumba hiyo nyekundu,” nilimjibu. “Humo kuna wasichana watawili halafu mapacha, wewe unamzungumzia Doto au Kulwa?” aliniuliza. “Mapacha?” “Ndiyo!” “Sasa kama mapacha hapo nitasema namzungumzia yupi? Wote watakuwa wanafanana...ila niambie wanaitwa nani!” nilimwambia. “Mkubwa anaitwa Glory na mdogo anaitwa Esta .” “Oh! Ahsante! Wanasoma?” “Mmoja anasoma Ardhi na mwingine anasoma IFM ,” alisema. “Wa …