NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (15)

Zephiline F Ezekiel
NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (15)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... Aliniangalia, alikuwa na hamu ya kuniuliza maswali mengi ambayo aliamini majibu ambayo ningempa yangemshangaza mno. “Imekuwaje?” aliniuliza huku akiniangalia. “Kuwaje kivipi?” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Sikuelewielewi ujue!” aliniambia. “Kivipi?” “Umependeza sana!” “Ooh! Kumbe sitakiwi kupendeza?” nilimuuliza huku nikitoa tabasamu pana. Naye akatabasamu. Akaniambia kilichokuwa kimemleta mahali pale, alinitafutia kazi katika supamaketi fulani iliyokuwa Upanga ambayo aliniambia kila kitu kwamba mshahara wake ulikuwa ni laki tatu. Alipanga kila kitu, aliwaseti wenye supamaketi hiyo na kuwaambia kwamba mimi ni kijana mwaminifu na sikuwa na tatizo lolote lile. Nilimwangalia, alikuwa msichana wa tofauti sana ambaye alionyesha ni kwa jinsi gani alinijali. Ila kazi ya supamaketi ningeifanyaje na wakati nilikuwa milionea? N…